OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 52,074
- 114,584
Katika sakata la vyeti na utekaji wa kituo cha habari cha Clouds Media linalomuhusu Mkoa wa Mkoa wa Dar Mh.Daud Bashite kumekuwa na utetezi kwamba hastaili kutenguliwa kwa sababu ni mchapakazi sana.
Utetezi huu sio tu imekuwa ukitoa kwa mashabiki wake(maana kuna watu hulipwa kwa kushabiki) bali hata kwa taasisi ya urais. Ukimya wa mashabiki hawa kuhusu uvamizi na utekaji wa Clouds Media na kughushi vyeti maana yake ni kwamba wanakubaliana na ukweli kwamba Makonda au Bashite amefoji vyeti na kafanya makosa kuvamia kituo.
Hata katika hotuba za rais ameshindwa kuzungumzia wajibu wake kwa mteule wake kuhisiwa kufoji vyeti matokeo yake ameishia kumkingia kifua tu kwamba yeye achape kazi. Ikumbukwe kwamba wakati wa teuzi za wakurugenzi wa wilaya kuna mmoja kati ya wateuzi waliohisiwa kuwa na kiwango cha chini sana cha elimu. Rais aliwaamuru wote waje na vyeti ili kuudhibitishia umma kwamba hakuna ujanja ujanja.
Turudi kwenye hoja kwamba ni mchapa kazi. Watu hawa pia wameshindwa kujibu hoja kwamba je,uchapakazi ni tiketi ya kufanya makosa ya jinai?Kwamba kama unachapa sana kazi hata ukiua ni sawa tu uchapakazi unakulinda? Lakini hata ukija kwenye hoja yao ya uchapakazi mimi binafsi sijaona uchapakazi huo wa kipekee anaoufanya Mh.Makonda zaidi ya stunts za kwenye media.
Au hizo kazi anachapia uvunguni wachache tu ndio wanauona? Tunaomba tuzifahamu hizo kazi mahususi na za kipekee alizochapa au anazochapa Makonda kiasi cha kuonekana yeye ni bora sana. Au tuseme anachapia gizani akiwa kazima taa ndio maana hazionekani kirahisi
Mimi nitaorodhesha "Uchapaji kazi" wake hapa kwa uchache
1. Ametuhumiwa kutumia cheti cha mtu mwingine. Tuhuma hizi zinamaliza mamiaka sasa bila kupata majibu stahiki wala kuwajibishwa kwa wahusika
2.Ametuhumiwa kutumia madaraka vibaya ikiwa ni pamoja na umiliki wa magari kiutata. Mitandao ya kijamii imemtuhumu kutumia na hatimaye kujimilikisha gari la Nas Haulige ambaye alimtaja kama mtuhumiwa na madawa ya kulevya. Tuhuma hizi hajazijibu
3.Imedhibitika kukivamia na kukiteka kituo cha Clouds Media kwa masaa kadhaa
4.Amepeperusha ushahidi wa aliowaita wauza madawa ya kulevya kina Mbowe,Gwajima nk kwa kuwataja na kuwapa mda wa kupoteza ushahidi. Katika uchapakazi wake amefanikiwa kukamata msokoto mmoja tu wa bangi
5. Ametuhumiwa kukashifu muhimili wa bunge na watumishi wa umma kwa ujumla
OMBI MAHUSUSI
Kumbuka kumpigia kura Mkuu Maxence Melo katika ile tuzo ya Human Rights Tulip