Niaze na Daima Mbele Nyuma Mwiko kisha niseme Samahanini wana Yanga

moodykabwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
625
602
Nianze na DAIMA MBELE NYUMA MWIKO
____________Jina
MOODY KABWE

NI MWNACHAMA WA YANGA TANGU
Tarehe 7/11/2009

Kadi No 006259
Na kadi yangu ni halali mpaka mwaka 2018

Nikiwa Ni mwanachama Ninaetambuwa wajibu wangu wa kimwanachama Wa kikatiba

1) Kuwa wakati wote Mkweli na Mwaminifu kwa klabu;

2) kuwa wakati wote sidaiwi ada zozote za uwanachama

3) kuhudhuria mikutano ya klabu inayonihusu

Hovyo ndiyo vipengele muhimu vya uwanachama halali wa YANGA AFRICA

_______>>>Napenda kutoa masikitoka yangu kwa Baazi ya wanachama wa Yanga waliotumia Mbinu chafu kunitolea uwaminifu wangu katika klabu kama kipengele namba moja kinavyonituma!! Niwe muwaminifu katika kalabu lakini kuna watu ama kwa kwa Makusudi ama kwa Maslahi yao binafsi wamenichafulia jina langu na kuniondolea uwamnifu katika klabu yangu pendwa

Ndugu wanachama na wapenzi na mashabiki na Marafiki zangu nyote kwa hekima na busara kabisa


hekima za ulimwengu upande wa kushoto na hekima za Mungu upande wa kulia. Ninapenda kuwaomba Radhi wale wote walioguswa na sakata lililonipata mimi MOODY KABWE la kuchonganishwa na Viongozi wangu wa YANGA AFRICA NA WADAU MBALI MBALI WALIOKUWA WANANIAMINI NA KUNIPENDA SANA NA KUNILEA KAMA MTOTO WAO KATIKA FAMILIA BORA YA YANGA AFRICA


Ninapenda kusema watu hao walionichafua na kunichonganisha na marafiki zangu na viongozi wangu wamekosa akili

Hapana shaka kuwa akili ni miongoni mwa atia na zawadi kubwa za Mwenyezi Mungu kwa mwanadamu. Mtume Muhammad SAW anasema: "Kudumu kwa uhai wa mwanadamu kunafungamana na akili yake, na hana dini mtu asiye na akili."Maana ya hadithi hiyo ya Mtume SAW ni kuwa akili ina umuhimu mkubwa katika mafundisho ya Kiislamu kwa kadiri kwamba, Bwana Mtume ameitaja kuwa ndio wenzo muhimu wa kutambua misingi na mafundisho ya Uislamu. Hadithi zilizopokewa kutoka kwa Mtume SAW na Ahlul Bait AS zinasisitiza kuwa, utukufu wa mwandamu na hadhi yake ya kuwa Khalifa wa Mwenyezi Mungu katika ardhi, una uhusiano wa moja kwa moja na ukamilifu wa akili yake. Uislamu na kitabu kitukufu cha Qur'ani vinasisitiza sana juu ya umuhimu wa kutumia akili na hekima. Aya za Qur'ani Tukufu daima zimetumia neno akili kwa sura ya kitendo na si kwa sura ya jina ili kusisitiza kwamba, suala muhimu zaidi ni kutumia akili na hikima na si kuwa na akili isiyotumiwa. Kuna aya nyingi sana za Qur'ani Tukufu zinazothibitisha hiyo. Katika Surat Muhammad aya ya 24 Mwenyezi Mungu anasema:

Ama watu hao wamekosa hekima na busara katika kunichafua kwao kama walivyokosa akili pia katika kinichafua kwao

Mimi Moody kabwe Kwa kipindi sasa nimekuwa sionekani. ila naamini maandiko yangu mengi hupanua ufikiri wa watu wengi. napenda kujifunza na kuelimisha wengine ili ninachojua kiwafikie wengine. Nasema hili kwasababu jamii bora na klabu bora ni ile ambayo watu wake wameelimika na wanaoweza kujiongoza wao binafsi kwa kutumia akili zao. ( self government )

hakuna elimu yeyote ambayo itamuokoa na kumuondoa mtu yeyote kutoka alipo zaidi ya ya kujitambua. Kuna kitu ndani na katika roho ya binadamu. Kitu hiko ni kikubwa zaidi ya binadamu kazi yangu ni kukifunua.

Binadamu wa miaka elfu hamsini iliyopita sio binadamu wa sasa. Binadamu kwa asili yake ni kama mnyama mwingine yule. lakini kitu kinachotutofautisha wao ni uwezo wa akili yetu kukua. Ni mawazo yetu ambayo hujenga na kubomoa, kila kitu unachoona ni zao la wazo. uovu au wema ni zao la mawazo yetu. Mawazo yetu huzaa matendo

Kwahiyo ni muhimu kuangalia jinsi mnavyofikiri kwasababu mawazo yenu ndiyo ambayo hunijenga.

Akili ya binadamu hukua kadiri unavyoitumia KWAHIYO ni muhimu kuwa na mawazo yanayojenga akili yako kila wakati. Klabu yetu itajengeka pale tu tutakapokuwa na mawazo bora na kuwa tayari kuyafanyia kazi mawazo hayo.

Baada ya kusema hayo Napenda kusisitiza kuwa Kwale wote Mliokwazika na uongo na uzushi uliozushwa kuhusu kabwe naomba mnisamehe na mm nimewasamehe wote mlionitukana bila kumjua huyo mnaemzungumzia

Na pia Sina ndoto ya kumpinga MANJI wala mpango wa Kumkataa Manji

Kwakua mm Mwenyewe ni mmoja ya washirika waliohakikisha manji anaendelea kuwa Yanga

Nimalizie kwa maneno haya

Hatutaweza kama hatutatumia nguvu zetu zote kujaribu, kama hatutatumia akili zetu zote kujaribu na tutakapoendelea kujaribu; ninaamini ndani ya kiza kinene macho yetu yataanza kuona jua taratibu kama linavyochomoza kutoka angani na kuonekana dhahiri machoni kwetu. Na lile wazo la klabu yetu kukua na kuwa kubwa litakuwa dhahiri. Without perseverence, without faith. Hatuwezi kufanikiwa kama klabu. Uzalendo ni muhimu sana. Ni muhimu kuwaweka watu wetu pamoja. Lakini hii yote inahitaji uongozi pasipo uongozi bora hatutaendelea. NA UONGOZI bora wa MANJI ndiyo wenye uwezo wa kufanya hayo

Mwisho Poleni sana mliokwazika kuhusu MOODY KABWE

MARAFIKI,WANACHAMA,WAPENZI, NA WALE WENYE KUNIONEA WIVU WOTE

BY MOODY KABWE COMREDY
mwanachama kadi namba 006259
DAIMA MBELE NYUMA MWIKO
 
Yeah, kwa hiyo uchaguzi huu ni kiini macho tu? Kwa lugha nyingine "Rubber stamp?".
 
Unatafuta kiki
Kiki ninayo ndiyo mana wana presha na mm kaka

Ila kwakuwa naijua katiba na naiheshimu nimesema ukweli na nitaendelea kuwa mkweli

Hao wote waliokuwa wanasema hata ukiwauliza kipengele kimoja tu cha katiba hawana
 
kama sijakuelewa vizuri ,maana hao unaowazungumzia sijui ni akina nani na kuna nini?
 
Manji ni binadamu na ni kiongozi, hawezi kukosa watu wa kumpinga, so wala usione shida wala aibu kumpinga, ila tuu uwe una sababu za msingi ambazo mtu yeyote reasonable ata zielewa, otherwise hapo ndo zitakuwa chuki binafsi sasa

Hahaa nimekumbuka kale ka clip flani hvi
 
yaa.jpg
 
Back
Top Bottom