Niambie shairi hili linahusu nini has a ??

Dr leader

JF-Expert Member
Jun 28, 2016
797
896
Bissimillah ya raufu kalamu nakamata
Nayaandika makovu kwa shauku ya kalamu
Shida ni za mwanadamu futa yangu matozi
Usitake mengi kwa pupa tamaa muachie juha
Ni ww pekee manani wakunitoa mashakani

Ni ww pekee manani wa kunitoa mashakani
Nikishika funda ,wanizoda majirani
Nitoe taabani na Mimi nifurahi maishani
Si wema wanadamu, hufurahi kwa kalamu
Ni ww pekee manani wakunitoa mashakani

Matozi yanitoka nikikumbuka zamani, Leo sina thamani waniteta vibarazani
Sitakukufuru raufu, ww hutoa kwa mafungu
Yuwanivuta shetani kuniita kwa makuhani
Sitofika handeni au pangani kwa wajadi
Ni ww pekee manani wa kunitoa mashakani

Nafika yangu tamati salamu kwako KIMWERI
Nayafiki ya mungu katu sitamshiriki
Ya rabi tuongoze, tudumishe kuifuata haki
Ni ww pekee manani wa kunitoa mashakani

Abuuabdillah
√√√√π√√ #kazi_ya_mnyonge_malipo_ni_kwa_MUNGU_pekee
 
Back
Top Bottom