NTAMBIRWEKI KATO
Member
- Mar 28, 2015
- 45
- 15
Nimesoma uzi mmoja ulikuwa ukiuliza ni kwa nini wana jamii f hawatangazi nia za kugombea udiwani. Sasa niweke bayana kuwa binafsi nilisha tia nia ya kugombea udiwani kata ya Businde iliyoko jimbo la Kyerwa mkoa wa Kagera. Nimejipanga vizuri kuwatumika wananchi wangu kwa tiketi ya CHADEMA na endapo sitopata nafasi hiyo basi nitashirikiana bega kwa bega kumnadi atakayepitishwa na chama pamoja na UKAWA kwa ujumla. Pia iwe nimepata fursa ya kupeperusha bendera ya chama changu au la, nitashiriki kikamilifu katika kampeini ya kuwanadi wagombea ubunge wa majimbo ya Karagwe na Kyerwa kupitia UKAWA. Nawaombeni nguvu yenu ya hali na mali, mimi namaliza shahada yangu ya kwanza mwaka huu katika chuo kikuu cha Dar es Salaam na ni kijana mdogo sana niliyenuia kuwatumikia watanzania kupitia udiwani. Tayari nimesha chukua fomu ya chama changu na kuijaza, mawsiliano ni jacksonikato@gmail.com. Nawatakieni siku njema watanzania wenzangu.