NIA THABITI:VIPI NITAITEKELEZA?

NIA THABITI:VIPI NITAITEKELEZA?

Abuu Saad

Member
Joined
May 19, 2017
Posts
94
Reaction score
139
Habari zenu wakuu!
Hongera zao wale walokuwa ibadani leo. Pole zao wale walokuwa katika harakati za kutafuta mkate wa kila siku.
Natumia kiswahili ili kila msomaji aelewe ili kuepuka lugha za kejeli,dharau,fedheha na zenye kuudhi!!
kama nitawakwaza mnisamehe kwa kweli.
Mimi ni kijana mwenye umri wa 28 kwa sasa,lakini sina lolote nalofanya,sina chochote nachomiliki,sina kazi wala shughuli ya kuniingizia kipato.
Nimemaliza chuo mwaka jana lakini kila nipambanapo nimekuwa nashindwa Kutimiza ndoto zangu.
Kila niamkapo asubuhi lazima nishike shavu na kujiuliza hivi ni lini nami nitakuwa na japo cha kumiliki?
KWA hali yangu ya sasa nahitaji sana msada kutoka kwa yeyote Yule mwenye kujiweza.
Imani yangu ni muislamu,najitahidi sana kufuata maamrisho na kuyakwepa makatazo ya MUNGU lakini kwa sasa wakati umefika Mimi kuwa na mwenza nafsi iko radhi kuoa lakini najiuliza ni vipi mwenza wangu atakula ,atalala na kuvaa ikiwa ni mahitaji ya msingi kwa kila kiumbe hai?
Tumekatazwa zinaa lakini cha ajabu nimekuwa nikitamani kujua nini huwa kinatokea watu wanapokuwa wawili ndani,hali inayopelekea nione kila mwanamke ni mzuri mbele ya macho yangu!
Tafadhali wakuu mwenye msaada wowote ili nami nianze kujipanga.
Msaada:kazi,kibarua au mtaji na hata aliyetayari kuolewa lakini hali ndo hii
 
Mkuu humo ndani umechangachanga vitu ila ni haraka tu kufikisha jambo kweli una nia.
 
Back
Top Bottom