Ni wazi kuwa CCM wamejipanga kubadili ajenda zilizopo

REAGAN C.MABOGO

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
1,269
1,007
Kila inapotokea ajenda yoyote, CCM wanafanya jambo linalolenga kufunika ajenda na kuwatoa wananchi kwenye mstari.

Mfano, LUGUMI, Kitwanga akajifanya amelewa na kufukuzwa ili taifa lihame kutoka kujadili ufisadi wa serikali hii na kuanza kumjadili KITWANGA juu ya ulevi huku kimtindo (wale wenye akili finyu) wawe wakimsifu John Magufuli.

Na kwa hiyo CCM wawe wamelamba dume. Mfano mwingine ni huu unaoendelea sasa, " LOWASSA APOKWA MALI ZAKE" ,hili nalo linalenga kubadili ajenda nyingi zilizopo ikiwemo ya namna BUNGE linavyoendeshwa kibabe na kihalifu.

Naomba niwambie CCM na rais wao kuwa hatujasahau kuandika na mpaka sasa tunaorodha hii:

1. Kubomoa nyumba za watu huku mvua kubwa ikinyesha.

2.Kufukuza hovyo watumishi bila kufuata sheria.

3. Kushuka kwa mapato ya nchi mfano bandarini.

4. Kupanda kwa sukari kiasi cha kutisha na kukosekana kabisa maeneo mengine.

5. LUGUMI.

6. Ajira mbalimbali kupotea na nyingine kuwa ngumu kuendesheka.

7. Kukanyaga haki za binadamu.

8. Kukandamiza BUNGE.

9. Kupanda kwa gharama.
 
Back
Top Bottom