Ni wapi Kituo halisi Cha Daladala cha Makumbusho - Kariakoo?

Kenney

JF-Expert Member
Dec 8, 2013
294
165
habari za Asubuhi wanajamii? nina kero moja ambayo kwakweli kila ninapo ifikiria sipati jibu, sijui kwa maeneo mengine imekaaje, lakini mie nazungumzia Usafiri wa Daladala kutoka Makumbusho kwenda Kariakoo. magari haya maranyingi utayaona tu Katikati ya Route lakini ukifika mwisho wa vituo hauyakuti, kiasi kwamba tunashindwa kuelewa huwa yanaanzia wapi safari na yanaishia wapi. Na siku hizi Daradara nyingi za njia hiyo yameandikwa Makumbusho - gerezani yakifika Kariakoo yanashusha abiria kabla ya kufika mwisho wa kituo ili wakapandishie abiria sehemu wanayoijua wao na kubadirisha Njia halkadharika wakifika Makumbusho utaratibu ni huohuo hawafiki mwisho kabisa kituoni. kibaya zaidi sasa hivi kutoka kariakoo wanapiga debe la Tandale hadi darajani( Mahali ambako siyo njia yake ili wakifika hapo Darajani waanzishe Njia nyingine ya kutoka hapo Darajani mpaka Makumbusho. mambo haya yanafanyika wakati mamalaka za kusimamia masuala ya usafiri zipo Nashauri mamlaka hizo zingejikita pia kwenye vituo vya daladala pia badaya ya kuvizia tu mabarabarani ili kulinda haki za abiria (Mamlaka ninazozungumzia ni sumatra na Trafiki) Naomba kuwasilisha.
 
dah umenikumbusha kuna siku nilizunguka sikuyaona na bigbon kituo kilihamishwa ikabidi niende fire. imekuwa ni kero sana. ngoja tuwasubiri wanaojua waje
 
dah umenikumbusha kuna siku nilizunguka sikuyaona na bigbon kituo kilihamishwa ikabidi niende fire. imekuwa ni kero sana. ngoja tuwasubiri wanaojua waje
Waliponiuwa kabisa ni pale magari ya Tegeta walipoamua yaishie Muhimbili sasa sijui mtu wa Kkoo ashuke pale atembee kwa miguu mpaka kariakoo na mengine ya kawe yapitie boma mpaka karume mpaka gerezani sasa mtu wa jangwani, na faya anaetaka kwenda muhimbili nae atembee kwa miguuu hawa wasomi wa siku hizi ni pasua kichwa kweli aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa.
 
sasa yeye anaprivate halafu ndiyo anayepanga ruti lazima tuumie tu
 
Back
Top Bottom