Wakuu,
Kuna
msichana yupo njia panda. Ana umri wa miaka 23. Ana mpenzi wake
ambaye wana undugu pia. Dada yake huyu msichana kaolewa na anko wa huyo
mpenzi wake. Wanapendana kwa dhati na hayo mahusiano ni ya siri sana,
ila kuna baadhi ya nugu zake msichana huyo wamegundua na hawakubaliani
na hayo mahusiano.
Tatizo linakuja kuwa huyo msichana anampenda sana na wana mipango kabisa
ya kufunga ndoa.
Naomba ushauri kwenu wadau la kufanya kwa hao wachumba. Suala lenyewe ni
kwua huyo msichana hakubaliki upande wa huyo mpenzi wake na hali huyo
mpenzi wake anakubalika kwao. Ushauri tafadhali.
Nawasilisha.