Ni wakati wa Z’bar kusonga mbele, na CUF kujitafakari

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
UCHAGUZI wa marudio Zanzibar umeshafanyika. Kwa kilichotokea, na kwa hakika kabisa, kulikuwa hakuna namna yoyote ya kufanya isipokuwa kurudi kwenye uchaguzi. Ni bahati mbaya sana chama kikuu cha upinzani Zanzibar, CUF kilisusia zoezi hilo la uchaguzi lenye tafsiri ya njia ya kidemokrasia katika kuitafuta ridhaa ya umma kwenye kuongoza.

Kwa CUF ulikuwa ni uamuzi wa kimakosa kususia uchaguzi. Ni uamuzi wenye gharama kubwa zaidi kisiasa. Siasa haipaswi kuwa uadui. Kilichobaki ni kwa CUF kuisogelea meza ya mazungumzo na wenzao CCM ili kuona ni namna gani wataweza kushiriki siasa za ndani ya Zanzibar na zaidi watakavyoshiriki chaguzi zijazo kwa namna ambavyo wanaamini zitakuwa huru na haki.

Na michakato ya namna hii ingelikuwa na maana na nguvu zaidi kama CUF kupitia wawakilishi wake nao wangeingia kwenye Baraza la Wawakilishi kupitia masanduku ya kura. Hivyo, wakati Wazanzibar wanahitaji kuyafukia yaliyopita kwenye kaburi la sahau na kusonga mbele kwa pamoja kuijega Zanzibar yao, ni wakati pia wa CUF kujitafakari upya na kujipanga kwa kushiriki siasa ikiwamo kujiandaa na chaguzi zijazo. Maana, hakuna faida yeyote kwa CUF kujiweka kando na kuwaachia CCM peke yao waendeshe siasa za Zanzibar. Si jambo la tija pia kwa watu wa visiwani na bara.
 
Ishii kumbe hili ni jukwaa la uvccm, ngoja nikimbie haraka kabla hawajanitumbua utumbo
 
Kunahitajika kufanywa uchaguzi mpya na si kurudia uchaguzi ,Jecha angesema uchaguzi unafanywa upya kidogo kungekuwa na mvuto lakini amesema anarejea uchaguzi ,katoka patupu na lana imewapata ,sasa hivi wakisali miccm wengine wote wanatoka misikitini ,jana Ijumaa ilikuwa ni tabu kubwa kwa viongozi wa CCm kujitokeza misikitini. Wanasema wanaharibu swala.

Kunahitajika uchaguzi ufanyike upya na sio chini ya usimamizi wa jecha wala jucha ,United Nation ndio atakuwa msimamizi tayari mipango ipo mbioni ,huu wa juzi ni hasara tu haujulikani hautambuliki ni igizo kama maigizo mengine na wao wanajua .
 
Kilichobaki ni kwa CUF kuisogelea meza ya mazungumzo na wenzao CCM ili kuona ni namna gani wataweza kushiriki siasa za ndani ya Zanzibar na zaidi watakavyoshiriki chaguzi zijazo kwa namna ambavyo wanaamini zitakuwa huru na haki..
The winner takes it all, the looser losses all!, aliyepata kapata yote na aliyekosa kakosa yote!, this time around hakuna tena fursa ya mazungumzo ya aina yoyote, bali kusubiri miaka 5 na kujaribu tena!.

Uchaguzi wa Marejeo Zanzibar ni Huru na Haki!.

Pasco
 
Back
Top Bottom