Ni wakati wa Watanzania kusimama Wenyewee!!

Ni wakati wa Watanzania kusimama Wenyewee!!

General Mangi

JF-Expert Member
Joined
Dec 21, 2013
Posts
15,317
Reaction score
23,192
Baada ya kuzitazama siasa zetu, nimetafakari na kugundua haya.

1. Sio ccm, chadema wala chama chochote cha siasa chenye dira na chenye nia njema na watanzania.
Viongozi wote wanawaza kushika dola kujaza matumbo yao.

2. Chadema sio chama cha kuaminika tena.
Ni ngumu kwa mtu aliye mfuasi wa hiki chama kuelewa hili kama hatakuwa free mind.
Hakuna chadema wanachokisimamia. Mbaya zaidi sisi tuliokuwa wafuasi wake badala ya kusimama na kuwakosoa pale wanapoboronga basi ndo tunawaunga mkono na kuwapa kichwa zaidi.
Chama cha upinzani hakisimami kama mpinzani kweli, nikiangalia S. Africa pamoja na upinzani kuwa wachache bungeni lkn angalieni Zuma anavyo zungushwaa.

3. Serikali ya Magufuli nayo haina dira.
Hili linaonekana wazi, hatuna vipaumbele, tunapenda kuanza kununua vitu vya anasa wakati watanzania wana matatizo lukuki. Sikuona haja ya kununua mindege ambayo najua mwisho wa siku itafia pale uwanjani.

Vijana tunashindwa kuwezeshwa tujiajiri, benk hazikopeshi, riba kubwa na mashart mengi.

Kama serikali imeshindwa kuajiri basi wekeni mazingira wezeshi kwa vijana kujiajiri, lkn haya hamuyaoni, mnaongeza makodi mengi kwenye mishahara ya watumishi, mnauwa purchasing power hatimae hata hivyo viwanda vitakuja kufa kwa bidhaa kudorora sokoni bila kununuliwa.

4. Watanzania wengi tumekosa ujasiri wa kuhoji, hatusimamii pamoja kuishinikiza serikali.
Leo wenzetu huko Kagera misaada yao haikuwafikia walengwaa, lkn mliopo Dar hata hili haliwagusi, kwingine wananchi washaingia barabarani kupinga ukatili huu.

NIWAKATI WA KUAMKA KAMA WATANZANIA, TUNASIMAMA KAMA WATANZANIA NA SIO CHADEMA, CCM WALA ASIYEKUWA NA CHAMA.

NIWAKATI WAKUSIMAMA KAMA WATANZANIA KUANGALIA MASLAI YETU NA SIO KUWAACHIA KIKUNDI FULANI.

NAOMBA MOTO HUU UANZIE HAPA JF.

IMETOSHA.
 
Tuanze na maandamano ya kupinga ufisadi wa pesa za rambirambi za wahanga wa kagera.
Upo sawa kabisa ila m7 unazoo? Mwenzio nina 6,970,000 ninasubiri serkal inirudishie 3000 zangu nilizochangia maafa ya kagera.

Kuwa makini mwanzilishi wa huu uzi mnafiki sana.
 
Upo sawa kabisa ila m7 unazoo? Mwenzio nina 6,970,000 ninasubiri serkal inirudishie 3000 zangu nilizochangia maafa ya kagera.

Kuwa makini mwanzilishi wa huu uzi mnafiki sana.
Onesha unafiki wangu mkuu,
Naomba uwe mkweli na sio taarabu za kitoto
 
Ivi hizi za wahanga wa tetemeko la bukoba zimeenda wap
 
Nimesema Tanzania ni muda mujarabu wa kuanza mapinduzi ya amani, mapinduzi ya wananchi hayawezi kuwa haramu. Wananchi tunaweza tukiamua make kuacha wahuni fulani watuamlie mambo yetu kwa staili za kizandiki namna hii ni utumwa
 
Huu ndio mkweli mchungu, mapinduzi ya amani kuipindua tanzania na kuirudisha kwenye mikono ya watanzania hakuna mwingine wa kutuokoa ni sisi wenyewe. Rais wa Trump atatuunga mkono katika hili tunahitaji ukombozi...
 
kichwa kinaniuma sana kwa mambo yanayoendelea
. NAUNGA MKONO HOJA
 
Back
Top Bottom