Mazingira yanaonesha hivyo, labda kama wapinzani walijipa muda kutaka kutafakari kwa kina nini hatma yao baada ya kuingia madarakani kwa awamu hii ya CCM. Tulisikia kauli za Dikteta uchwara mwanzoni mwa utawala huu.
Kulikuwa na viashiria vya Bunge kuingiliwa na kuvurugwa sheria mbali mbali za nchi kulikohusishwa kwa utawala huu. Vita vilivyoko bungeni vya kunyamazisha mawazo ya upinzani vimekolea sasa.
Siasa imepigwa marufuku na rais hadi 2020., Maandamano yamezuiliwa na vyama vya upinzani vinavurugwa kwa makusudi. CCM imelewa madaraka, inawaona wapinzani wamewadhibiti na kujisifu eti kweli dawa imepatikana. Hapana Nadhani subira ya kujiridhisha imetosha.
Nani hatawaelewa mkidai uhuru wa demokrasia? mnahofia nani viongozi wa dini ? taasisi za kidemokrasia? jamii ya kimataifa au nani ? Au ndio CCM imewadhibiti kweli ?
Mnasubiri mmalizwe ndio mupige yowe ?
MUDA MUAFAKA.
Mmesahau ajenda za Katiba mpya, tume huru na ustawi wa demokrasia kuwa hayo yanahitaji kupiganiwa ? Mnasubiri 2020 ndio mdai Tume huru ? Hatuwafundishi lakini nakumbuka neno MZIKI WA DEMOKRASIA. Labda siku hizi neno hili nalo limezuiliwa.
Tathmini ya utawala wa kidemokrasia imepwaya sana, Kazi ya upinzani ikidhibitiwa inafifisha Taifa Labda mtwambie Neno MIKAKATI (strategies) zinafanikiwa vipi huko gizani mnakoandaa. Jee hio mikakati kweli ipo na iko hai ?
Hatutawaelewa WAPINZANI IKIWA WAKATI WA KIKWETE MLIFIKA WAKATI KUJITOA MUHANGA kupigania demokrasia na kufika wakati hadi watu kuumizwa kule Arusha, waandishi kuteswa na kuumizwa leo hii ni maradufu eti mko kimya hatutawaelewa kamwe. Yaani jitihada mlizofanya kujijenga na kujiiimarisha hali iliyopelekea kupata nguvu za wabunge , na kuungwa mkono leo mshirikiane na CCM kuuwa jitihada hizo kweli ?
Ndio mnashirikiana nao kwa nini mnyamaze na kuridhia kunyimwa huku kwa demokrasia ?
Kwa maoni yangu sasa ni wakati muafaka wa kusema " NO", sasa imetosha.
Kishada.