Sheria ya utoaji mimba iangaliwe upya

Oct 5, 2015
88
476
NI WAKATI WA SERIKALI KUANGALIA UPYA SHERIA YA UTOAJI MIMBA.

Dr. Christopher Cyrilo .

Kwanza kabisa nitangulie kusema andiko hili linaweza kuibua mjadala mkubwa na malumbano. Lkn itapendeza kama mjadala huo utakuwa wa kujenga, na malumbano yatakuwa ya hoja na sio hisia.

Mimi, kama mkristo mkatoliki natambua kuwa kanuni za kanisa haziruhusu utoaji mimba angalau katika mazingira fulani, nitaeleza. Vilevile sheria za nchi haziruhusu utoaji mimba isipokuwa katika mazingira hatarishi kwa mama, pia nitaeleza. Hata hivyo, kama binadamu natambua haki na uhuru wa binadamu wengine, naheshimu hisia zao, mipango yao na harakati zao za kuboresha maisha yao bila kufungwa na minyororo ya imani yangu.

Nimewahi kufikiria kuandika jambo hili muda mrefu kidogo, lakini umati wa wanawake waliohudhuria kwenye ofisi za mkuu wa mkoa, Dar es salaam kwa madai ya kutelekezwa watoto wao, umekuwa chachu ya mimi kuwahi kuandika andiko hili.
Mimba.

Mimba au ujauzito ni hali ya kuwapo kwa kiumbe kisicho kamili kinachoendelea kukua na kuimarika ndani ya mfuko wa uzazi wa kiumbe cha kike, hadi kuwa kiumbe kamili wakati wa kuzaliwa. Ni tukio linalofuta baada ya kujamiiana, endapo mbegu timilifu za kiume zitarutubisha yai timilifu la kike.

Mimba inaweza kutungwa lakini isiendelee na isijulikane kama imewahi kutungwa. Lakini yai la mwanamke linaweza kurutubishwa na mbegu za kiume ila mimba isitungwe, ikiwa mfuko wa mimba hautakuwa dhahiri. Pia, mimba inaweza kutungwa lakini isiendelee ikiwa maumbile ya mfuko wa mimba si rafiki.

Kwa maana hiyo, kurutubishwa kwa yai la mwanamke au hata kutungwa kwa mimba pekee, sio lazima iwe ndio mwanzo wa maisha ya kiumbe.

Hata mimba inapokuwa ya umri mkubwa, yapo mazingira ya asili yanaweza kupelekea kutoka kwa mimba hiyo (miscariage/spontenous abortion).

Kutungwa kwa mimba.
Mwanamke mwenye rutuba huweza kupata mimba anapokutana na mwanaume mwenye rutuba wakati yai lake (ovum) linapozalishwa na kuruhusiwa kutoka kwenye ogani za uzazi (ovaries). Ogani hizi zipo upande wa kushoto na kulia, chini tumboni, na hupokezana kuzalisha yai kila baada ya siku 28 (mara nyingi) au kwa wanawake wengine huchukua hadi siku 36.

Ikiwa yai hilo halitakutana na mbegu za kiume basi halitarutubishwa. Na kwa hiyo litaharibika na kutolewa nje kupitia ukeni (hedhi). Inaweza kuchukua siku 2 hadi 7 kwa mabaki ya yai hilo kutolewa kabisa. Huu ndio wakati wa hedhi au 'period'.

Wakati yai likiwa limeharibika kwa kukosa mbegu ya kulirutubusha, ogani za uzazi za mwanamke(ovaries) huanza kutengeneza yai lingine na mzunguko ule ule huendelea.

Mara nyingi yai lilokamililka hutolewa siku ya kati kati ya mzunguko. Kwa mfano, kwa mwanamke ambaye mzunguko wake ni siku 28, basi yai hutolewa siku ya 14. Hata hivyo linaweza kuwahi kidogo (siku ya 12 au 13) au kuchelewa kidogo (siku ya 15,16).

Yai hilo (ovum) linaweza kuishi kwa masaa 48 na mbegu za kiume zinaweza kuishi kwa masaa 48 (siku 2) hadi masaa 72 (siku 3)
Kwa hesabu hizo, ikiwa mbegu za kiume zitakuwapo kwenye eneo la uzazi tangu siku ya 9 ya mzunhuko, (siku ya 9 baada ya kumaliza hedhi) zinaweza kurutubisha yai la mwanamke kama litatolewa siku ya 12 (siku 3 baadae) na kama zitakuwapo siku ya 18 zinaweza kurutubisha yai lilotolewa siku mbili nyuma (siku ya 16) kwa kuwa bado lipo hai.

Kwa ufupi, mimba kutungwa ikiwa mbegu za kiume zitakutana na yai la kike, na uwezekano wa jambo hilo hutokea siku ya 9 hadi ya 19 ya mzunguko wa siku 28, Wadada wanaojua wanaita siku hizo, siku za hatari.

Angalizo; mzunguko wa hedhi unaweza kubadilika kwa sababu kadhaa; safari ndefu, kazi nzito, maradhi, kufanyiwa upasuaji, msongo wa mawazo (stress) au matumizi ya dawa mbalimbali zikiwemo dawa za uzazi wa mpango.

Sheria za utoaji mimba.
Hadi kufikia mwanzo mwa karne ya 19 (1800's) hakukuwa na sheria yoyote katika nchi yoyote wala dini yoyote iliyozuia utoaji mimba. Sababu inaweza kuwa kwamba, vitendo hivyo havikuwa changamoto au havikuwa vimeshamiri kwa sababu ya kukosa njia salama (za kitabibu) za kutoa mimba, au hakukuwa na upatikanaji mimba holela kama ilivyo leo.

Mwaka 1869, Papa Pius wa tisa (Pope Pius IX) alianzisha mchakato wa kuweka sheria za kukataza utoaji mimba. Papa alisema kwamba roho ya binadamu huanzia pale urutubishaji (conception) unapotokea, mbegu ya kiume inaporutubisha yai la kike. Tamko hilo likapalekea kuwekwa kwa sheria za kupinga utoaji mimba katika mazingira yoyote.

Karibu Mataifa yote ya ulaya yakaweka sheria ya kuzuia utoaji mimba kwa namna yoyote (Restrictive abortion laws).
Wakati wa ukoloni sheria hizo zilihamishwa pia katika makoloni huko Afrika, Asia na Amerika ya kusini.

Baada ya ukoloni kufikia ukingoni, kuanzia mwaka 1950 hadi kufikia mwaka 1985 mataifa yote yaliotawala wengine (wakoloni) yalifanya marekebisho ya sheria ya kuzuia utoaji mimba katika mazingira yoyote. Leo hii, barani Ulaya ni nchi tatu tu, Ireland, Poland na Malta, zote za kikatoliki, ambazo bado zinasheria ya kuzuia utoaji mimba katika mazingira yoyote isipokuwa tu kama uhai au Afya ya mama ipo hatarini.

Tanzania na Afrika.
Mataifa 35 ya Afrika yameweka sheria ya kuzuia kutoa mimba isipokuwa tu ikiwa uhai wa mama upo hatarini na/au afya ya mama ipo hatarini.

Sheria ya Tanzania inakataza utoaji mimba kwa namna yoyote isipokuwa tu kama uhai wa mama upo hatarini, haijalishi kama afya ya mama ipo hatarini.

Sheria hizi zinakinzana kiasi na makubaliano kadhaa ya kimataifa kama vile UN International Conference on Population and Development - Cairo, Mkutano wa nne wa dunia wa kinamama huko Beijing, moja wa viongozi akiwa Mama Getrude Mongella wa Tanzania (World Conference on Women in Beijing) na Azimio la haki za binadamu (The Universal Declaration of Human Rights (ibara za 1 & 3 &12 &19 & 27.1).

Takwimu.
Takriban mimba milioni 205 (205,000,000) hutungwa kila mwaka duniani kote. Lakini katika kila watoto 100 wanaozaliwa kuna mimba 31 zilizotolewa kwa kukusudia (induced abortion).

Kutoa mimba kunachangia vifo vya kinamama vinavyotokana na ujauzito kwa asilimia 13 duniani kote.

Kwa mujibu wa Taarifa za Shirika la afya Ulimwenguni (WHO), Kiwango cha utoaji mimba katika nchi zenye sheria ya kuzuia utoaji mimba hakina tofauti na kiwango cha utoaji mimba katika nchi zisizokuwa na sheria hizo (Geneva and Guttymacher, New York).

Zaidi, Dr. Paul Van Look wa WHO (October 2007) anaeleza kuwa utoaji mimba katika nchi zenye sheria ya kuzuia kitendo hiko, ni hatari zaidi kuliko katika nchi zilizoruhusu kwa kuwa, katika nchi zinazozuia utoaji mimba, wanawake hufanya kwa njia za siri zisizo salama na wataalam wasio na uwezo wa kutosha. Vifo na mdororo wa afya unaotokana na utoaji mimba hutokea zaidi katika nchi zinazopinga utoaji mimba.

Hata hivyo, tafiti hii ilipingwa na Dr. Randall K O'Bannon, wa mfuko wa elimu ya haki ya kuishi wa mjini Washington akidai kwamba vifo na mdororo wa afya hutokea zaidi katika nchi masikini sio kwa sababu ya sheria zinazopinga utoaji mimba bali kwa sababu ya huduma duni na kukosa vifaa tiba vya kuwasaidia akina mama wanaojaribu kutoa mimba.

Hata hivyo katika tafiti zingine, inaonekana nchi zenye sheria za kuzuia utoaji mimba (hasa nchi masikini) ndiko ambapo vitendo hivyo vinafanyika zaidi kuliko katika nchi zinazoruhusu kutoa mimba.

Nchini Uganda, ambako sheria zinakataza utoaji mimba, wanawake 54 kati ya 1000 wenye ujauzito hutoa mimba kwa kukusudia.

Marekani sheria zinaruhusu utoaji mimba, wanawake 21 kati ya 1000 hufanya hivyo.
Katika Ulaya magharibi ambako sheria zinaruhusu kutoa mimba, ni wanawake 12 tu kati ya 1000 wanafanya hivyo.
Nchini South Africa, baada ya kuruhusu utoaji mimba mwaka 1996, vifo vya kina mama vilipingua kwa asilimia 90.

Nchini Ethiopia, ni kinyume cha sheria kutoa mimba lakini vitendo hivyo hushika nafasi ya pili kwa kusababisha vifo vya kinamama.

Nigeria, utojai mimba ni kinyume na sheria na asilimia 13 ya vifo vya kina mama hutokana na utoaji mimba.

Tafiti zilizofanywa na watafiti kutoka taasisi ya Guttmacher ya Marekani kwa kushirikiana na taasisi ya tafiti za kitabibu ya Tanzania (National Institute for Medical Research/NIMR) na chuo kikuu cha afya na sayansi shirikishi cha Muhimbili (Muhimbili University of Health and Allied Sciences/MUHAS), zilionesha kuwa idadi ya wanawake laki nne na elfu tano (405,000) walitoa mimba kwa mwaka 2013 pekee nchini Tanzania.

Aidha wanawake zaidi ya milioni 1 (1,000,000) walipata mimba zisizotarajiwa na asilimia 39 (405,000) walitoa mimba hizo.
Katika hao waliotoa mimba, kinamama 166,000 walipata madhara yaliyotokana na utoaji mimba, huku 66,000 walitibiwa na 100,000 hawakutibiwa.

Taarifa zinaonesha kwamba utoaji mimba Tanzania huchangia kwa kiasi kikubwa vifo vya kinamama wajawazito lakini hakuna takwimu kamili.

Pia kuna tofauti za kitakwimu baina ya kanda na kanda.
Kanda ya ziwa inaongoza kwa kutoa mimba, Wajawazito 51 kati ya 1000 hutoa mimba huko kanda ya ziwa. 47 kati ya 1000 huko nyanda za juu kusini, na Zanzibar hushika nafasi ya chini kabisa kwa kutoa mimba, 11 kati ya 1000.
Wastani wa kitaifa ni 36 kati ya 1000.

Kwa hiyo ukijumlisha mimba zote zilizotarajiwa na zisizotarajiwa, ni aslimia 3.6 pekee ndio hutoa mimba. Wakati kwa mimba zisizo tarajiwa ni asilimia 39 (405,000 kati ya >1000000) hutoa mimba.

Mjadala.
Suala la utoaji mimba ni suala lenye sura kuu tatu, Kisheria, Kiimani na Kitabibu. Aidha katika sheria tunaweza kuingiza mambo ya kisera kama kidhibiti au kuongeza kasi ya ongezeko la watu, mambo ya kiuchumi na mambo ya uhuru wa kujiamulia namna ya kuishi.

Kwenye imani, binafsi sioni nguzo yoyote ya kusimamia hasa ninapojadili kuhusu masuala ya kitaifa. Taifa letu ni la kisekula (halina dini), isipokuwa watu wake wana dini. Ni vema mambo ya Kiimani yasijadiliwe kitaifa bali yabaki kwenye imani ya mtu binafsi bila kuingiliwa kisheria, na bila kuathiri sheria. Serikali inaweza kuruhusu mambo yaliyo kinyume na imani za kundi fulani huku kundi hilo likaendelea na msimamo wake wa kiimani na wengine wakanufaika na sheria hizo bila kuathiri wenye imani zao.

Mathalani suala la utoaji mimba, ikiwa litaruhusiwa, haina maana kwamba itakuwa lazima, bali ambaye anaona ni kinyume na imani yake hatafanya hivyo. Hiyo haitaathiri upande wowote. Ni kama vile kula nguruwe, kufunga kwaresma au mwezi wa Ramadhani, kunywa pombe, kuvuta sigara nk. Mi matakwa au mazuio ya kidini lakini 'wanadamu' wanafurahia uhuru wao bila kuathiri wengine.

Katika utabibu, wataalam wa afya ni mashahidi wazuri kwenye hili. Karibu kila siku, wasichana wawili au watatu au zaidi kufika hospitalini kwa sababu zinazohusiana na utoaji mimba. Wengi wao wakiwa wameshafanya lakini kukatokea madhara na kwa hiyo kufika hospitali kwa matibabu. Hospitalini sio kituo cha polisi na hakuna mtu anayeweza kukamatwa eti kwa sababu mimba imetoka/imetolewa. Pamoja na sheria kukataza lakini sijawahi kusikia mtu anashtakiwa kwa kosa la kutoa mimba. Na sitarajii.

Ni vema sasa, serikali iangalie namna ya kurekebisha sheria za utoaji mimba kuepusha changamoto nyingi za kijamii kama hili la kutelekeza watoto, changamoto za kiuchumi, kielimu na hasa ki-afya.

Tumeona pamoja na sheria kukataza, lakini vitendo hivyo hufanyika sana. Na kwa sababu ya kikwazo cha sheria, vitendo hivi hufanywa kwa siri na katika mazingira hatarishi.

Sheria iangaliwe upya kuwasaidia hawa kinadada. Wapo wanaopata mimba kwa kubakwa au kulaghaiwa kwa kuombwa Rushwa ya ngono na maboss, na wengine kwa sababu ya ujinga wa elimu ya uzazi, shida ni kwa wanawake.

Serikali imekuwa ikiboresha huduma za uzazi na uzazi wa mpango, elimu ya uzazi na hata huduma kwa mimba zilizotoka/tolewa (post abortal care) lakin bado haitoshi. Nguvu zaidi inahitajika na endapo sheria itarekebishwa maana yake vitendo hivyo vitafanyika katika mazingira salama tofauti na sasa.

Si lazima hata hivyo, kuruhusu utoaji mimba katika mazingira yoyote. Nchini Uingereza, hairuhusiwi kutoa mimba zaidi ya miezi saba (wiki 28) Kwakuwa katika umri huo kiumbe kinaweza kuishi chenyewe.

Kwa hiyo utoaji mimba ni chini ya wiki 28.
Tanzania hairuhusiwi hata kama mama anaweza kupata shida ya kiafya isiotishia uhai. Hadi pale uhai wa mama (sio afya) uwe hatarini ndio inaruhusiwa. Nchi nyingi za Afrika na Amerika ya kusini zina sheria hiyo, zimerithi kutoka ukoloni na hazijarekebishwa. Ni wakati wa kurekebisha.

Serikali hata isipoondoa sheria hiyo, inabidi ilegezwe ili kuwasaidia akina mama. Tunaweza kuanza na kuruhusu chini ya miezi mitatu ambapo mifupa ya kiumbe bado haijajengeka na kuruhusu akina mama wenye shida ya kiafya na si lazima iwe tishio kwa uhai.

Matatizo ya kiuchumi, kijamii na kielimu na migogoro ya mahusiano pia vifikiriwe. Namna mimba ilivyopatikana kama kubakwa au kwa kuombwa Rushwa ya ngono pia ziangaliwe.

Tutawasadia maelfu ya kinamama wanaotaabika na wengine waliopoteza ndoto na matarajio yao na kuepuka kujaza machokoraa mitaani.

Shirika moja lisilo la kiserikali lina msemo wake, "Children by choice, not by accident" (watoto kwa kuchagua sio kwa ajali)

Msimamo
Pamoja na maoni yangu haya, nitoe msimamo wangu kwa sasa. Kama Daktari, bado nafuata maadili yangu ya kitabibu yanayoambatana na sheria za nchi. Nitafurahi ikiwa Mapendekezo niliyotoa yatapokelewa lakini kabla ya hapo, nafuata sheria zilizopo. Tusitafutane.

Nafungua mja mmdala!
 
Nakubaliana na hoja zako, kimsingi hili linaweza kuwa kosa linalofanyika kwa wingi kila leo, natambua kuwa pamoja na kiapo cha taluma yako, umeyaona mengi yaliyonyuma ya kapeti kwenye hili.

Je hakuna utaratibu uliowazi kuwasilisha maoni haya kwenye mamlaka yenye uwezo wa kuyafanyia kazi maoni yako haya?
 
mr mkiki.
 
Kwa kweli Mkuu umezungumza vitu vizito sana ktk jambo hili, wakina mama na wadada wamekuwa waathirika zaidi wa jambo hili hasa wanafunzi.

Binafsi nawashauri mabinti kuwa wakijiona tu mwanzoni wana dalili za mimba hususani kuvuka siku yao ya period, kama wanataka kutoa basi watoe mapema kabla mimba haijazidi miezi 2, kadri muda unavyozidi kwenda ndivyo risk inavyozidi kuwa kubwa.

Kutumia vidonge vya Misoprostol viwili chini ya uke na vingine kumeza ni hatari japo wanawake wengi wanatumia njia hii na sijawahi kumsikia hata mmoja akisema mimba ilishindwa kutoka kwa njia hii ila nasema ni hatari sababu mwanamke anaharibu kizazi chake kwa sehemu.

Unachopaswa kufanya ni kumeza mifepristone kwanza, mifepristone itafanya kuzuia urutubishwaji wa kiumbe tumboni, mimba haitaendelea kukua sababu mifepristoni ikizuia urutubishwaji huu ina maana mtoto anakufa. Baada ya kumeza mifepristone ndipo mwanamke anapaswa kuweka kidonge cha mistoprostol kimoja chini ya uke baada ya masaa 24 tangu alipomeza Mifepristone. Misoprostol itasababisha mwanamke atoke damu ambayo itaashiria kutoka kwa mimba rasmi. Mwanamke anaweza akatumia Buscopan ili kutuliza maumivu ya tumbo la chini au wengine hata fragly wanazitumiaga na zinawasaidia kutuliza maumivu.

Ushauri wangu wa Mwisho ni kwamba kama unajijua umefanya mapenzi siku ya hatari, jaribu kwenda famasi tafuta dawa inayoitwa p2 ama kwa jina lingine inaitwa plan b, pia inaitwa The Morning After Pill. Kidonge hiki/Vidonge hivi ni Levenogrogel, ni dawa ya uzazi wa mpango ila chenyewe unatumia pale tu unajua umesex ukiwa ktk hatari, na vingi vilivyopo Tanzania ni kwamba unameza ndani ya masaa 72, yaani ndani ya siku 3baada ya ngono ukiwa ktk siku ya hatari.

Kazi ya hii dawa ni kuzuia yai ambalo limekamata mbegu lisijikite ktk mfuko wa uzazi ili mimba kuanza kukua. Na kama yai bado halijatoka ktk Ovar, lenyewe linakausha ute ambao yai hulitumia kuteremka ili kusubiria mbegu. Kwangu sijawahi kushuhudia P2 ikifeli labda kama imetumiwa nje na utaratibu mzuri, ni moja ya dawa ambayo ni effectiveness.

Dawa hii zimegawanyika ktk sehemu mbili, zipo ambazo kuna kidonge kimoja na zipo ambazo zinakaa mbili. Hizi zinazokaa mbili wengi wanazimeza zote kwa wakati mmoja, japo bado itaendelea kukusaidia kwa asilimia kubwa ila sivyo inavyotakiwa, kidonge kimoja utakimeza kisha cha pili utasubiri masaa 12 tangu ulipomeza cha kwanza ndo umeze hiko kingine ila endapo ukauziwa p2 yenye kidonge kimoja, meza hikohiko kimoja tu inatosha.

Mwisho kabisa kwa kuwa natumia simu nimalizie kusema kwamba, ngono nzuri ni ile ambayo utaifanya ukiwe kwenye ndoa tu, mbali na hapo ni matatizo.
 
hapa ndo penyewe, Jamani hii sheria ipoje kuna binti anadaiwa katoa mimba na walimu wake yeye amekataa walimu wamempeleka kituoni siku ya 3 sasa bila kumshirikisha mzazi mtoto ni wa kidato cha nne na yupo under18. swali je hawa walimu wanaweza kumpima mtoto kama ameabort ama la bila kumshirikisha mzazi ama mlezi? wanadai docta amedhibitisha kuwa mtoto ametoa mimba picha za utrasound zipo mtoto anakataa hajatoa mimba? kisheria hii imekaaje.
 
Back
Top Bottom