Ni wakati wa kula bata

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,782
699,225
Kufa kufaana walinena wahenga! Muuza majeneza akisema leo biashara nzuri ujue kuna vilio vingi mitaani yani watu wamekufa sana.....

Tulipiga sana kelele kipindi cha pili cha uongozi/utawala wa awamu ya NNE...tuliona kabisa nchi ikiyumba na kukosa dira na mwelekeo! Watu walikuwa wanapiga ndefu ndefu bila woga wala haya

Tukasema tunahitaji kichwa kimoja kilichodata kije kinyoroshe nchi, kwa tulipokuwa tumefikia tulihitaji complete n total overhaul... I mean major overhaul
Tumeona mafisadi papa wakipandishwa karandinga na kuchuchumalishwa kama vibaka na watu ambao enzi zile wasingethubutu hata kuwasogelea! Vidagaa kama bashboy na lugman wala sio kipaumbele kwa sasa ngoja vinonenone!
Anapotibiwa kibopa fulani hospital fulani manesi na madokta siku hiyo wataondoka nyumbani si haba....
Huu ni msimu wa mavuno kwa bwana kokoroni wote! Wazee wa heshima zao na pesa zao na umaarufu wao wako lupango...unafikiri wanakula dona na nyama ya mchuzi?

Wanapata first class treatment kwenye kila kitu ila wanaipata kwa kuongea vema na mabana kokoroni ......acheni nao wale jamani wameteseka mno
Kadiri mapapa yanavyozidi kudakwa (wengi wakiwa ni wapendwa wa chama chetu) ndio mabwana korokoroni wanavyozidi kuneemeka na kupandisha dau...

Ama kweli kufa kufaana.....
 
Kumbe!
Kwahyo,El the Don,naye akipelekwa Segerea,wale maafisa magereza wataneemeka enhe?
 
Yani nlivyosoma kwanza kichwa cha habar Ngashtuka mie daaah ila wacha wao waisome namba lupango
Sisi twaisoma namba ulaian
 
Mahabusu nako ili uishi vizuri lazima uwaonge maaskari walio zamu hivyo nahisi kuna maafande wa mahabusu sasa hivi wanaomba hawa wawili walio mahabusu sasa hivi wasitoke, wanapiga ndefu!!
 
Mshana Jr.
Kufa kufaana au sio
Wacha askari wetu nao wapate hata za vocha
Nasikia siku hizi vijana wanagombea shift hasa za usiku! Sijui usiku kuna nini? nasikia pia siku hizi kukuta magari ya kifahari kama kwenye hotel za nyota tano ni kawaida kabisa
Mshana Jr.
Kufa kufaana au sio
Wacha askari wetu nao wapate hata za vocha
Nasikia siku hizi vijana wanagombea shift hasa za usiku! Sijui usiku kuna nini? nasikia pia siku hizi kukuta magari ya kifahari kama kwenye hotel za nyota tano ni kawaida kabisa
 
Back
Top Bottom