Ninajaribu kutazama namna tunavyoendesha kampeni za uraisi (jopokuwa si rasmi) kwa msaada mkubwa wa vyombo vya habari, huwa naumwa na kichwa. Moyoni nasononeka na kujiuliza, hivi anayefaa kuwa Raisi ni lazima awe/amewahi kuwa Waziri Mkuu, Waziri au Naibu Waziri tu.
Je Makatibu wakuu wa Wizara, Manaibu Katibu wa Wizara, Wakurugenzi wa wizara, Makamishna wa wizara, Wakuu wa mashirika mbalimbali, Wabunge, Watendaji wa NGOs n.k. Je vyomba vya habari vimeshindwa kumnadi au kuwanadi hawa ambao sio mawaziri?
Tuseme vyombo vyetu vya habari ni fuata upepo tu kwamba mtu ambaye anajigamba waziwazi au kwa kificho ndiye tu anafaa kuwa Raisi. Kwanini watanzania wenyewe kwa kushirikiana na vyombo vya habari wasijaribu kutafuta NJE YA BOKSI Mtanzania anayeweza kuomgoza nchi na kumnadi.
Inavyo onyesha hoja kubwa au kigezo kikubwa ili kuwa Raisi mwaka huu ni uadilifu. Ni sawa kabisa kwamba kiongozi lazima awe mwadilifu, lakini uadilifu peke yake unamfanya mtu awe kiongozi bora? Mbona mambo mengine kama uchapa kazi, ujasiri wa kusimimia mipango na kuelekeza, busara, hekima, huruma kwa wananchi wa kawaida, ubunifu, n.k havipewi kimbaumbele? Ilitakiwa kipindi hiki ambapo muda uliobaki ili kupata serikali mpya ni mfupi sana, tuwe tumechuja tunaotaka (sio wanaotaka) kuwa Raisi wa nchi.
Ni kweli ufisadi umelididimiza taifa na unaendelea kulididimiza hivyo tunataka kiongozi ambaye atakemea na kushughulika na ufisadi kwa dhati na vitendo, lakini baada ya hapo tunatakiwa twende mbele zaidi na wala sio kwa kutomasatomasa tu bali kuingia kiundani.
Nahitimisha kwa kurudia kwamba Raisi sio lazima awe amewahi kuwa Waziri Mkuu, Waziri au Naibu Waziri tu. Tufikirie na kutafuta NJE YA BOKSI. Wengine watasema muda haupo wa kutafuta NJE YA BOKSI, lakini mbona hadi sasa kati ya hao waliotangaza nia inaonyesha bado hakuna ambaye ameaminika kwamba atatutoa hapa tulupokwama kiuchumi, kimaadili
na kimaendeleo? ILI KUPATA KIONGOZI BORA " WE HAVE TO THINK BIG AND OUTSIDE THE BOX"
Mwenyezi Mungu kwa enyenyekevu tunakuomba Ibariki Tanzania.