karv
JF-Expert Member
- Dec 26, 2019
- 1,801
- 3,272
NI WAKATI GANI USITUMIE DAWA
Habari wana jf natumaini mnaendelea vyema na majukumu yenu ya ujenzi wa taifa
Watu wengi wanaamini kuwa kuna vitu hawawezi kufanya au kula wakati wanapotumia dawa. Kwa sababu hii wanaweza kuacha kutumia dawa ambazo inawabidi watumie. Ukweli ni kwamba hakuna dawa ambayo inaweza kuleta madhara eti kwa sababu inanywewa wakati wa kula chakula fulani hata kama ni nyama ya nguruwe, pilipili, mapera, machungwa au chakula cha aina yoyote. Lakini vyakula vyenye mafuta au viungo vinaweza kukuletea tatizo la tumbo hata kama hukumeza dawa. Kuna dawa nyingine zinaweza kudhuru iwapo mtu atakunywa pombe.
Kuna nyakati si vizuri mtu kutumia dawa kwa mfano :-
1)Mjamzito au mama anayenyonyesha hana budi kuepuka dawa ambazo si lazima atumie (lakini anaweza kutumia vitamini na vidonge vya damu bila kudhuru chochote)
2)Kwa upande wa watoto wachanga ni vizuri kuwa waangalifu sana kwa kuwapa dawa. Ikiwezekana afadhali upate ushauri wa wataalamu wa afya kabla ya kuwapa dawa yoyote pia hakikisha huzidisha kipimo.
3)Mtu yeyote ambaye amekwisha pata matatizo kama kuvimba, kuwashwa, n.k baada ya kutumia dawa inambidi aacha kabisa kutumia dawa hiyo kwa muda wa maisha yake yote kwa sababu inaweza kumletea adhari kubwa.
4)Mtu mwenye vidonda vya tumbo au kiungulia lazima waepuke dawa zenye asprin.
5)Kuna dawa maalumu ambazo ukitumia zinadhuru wakati ukiwa na ugonjwa fulani. Kwa mfano mtu mwenye ugonjwa wa ini hatibiwi na dawa za za kuua vijidudu au dawa zozote kali, kwa sababu ini halifanyi kazi, hivyo dawa hizi zinaweza kudhuru ini.
6)Watu ambao wamepungukiwa maji ya mwilini au wanamagonjwa ya figo ni lazima wawe waangalifu kwa dawa wanazotumia. Usitoe zaidi ya kipimo kimoja cha dawa ambayo kudhuru mwili mpaka uwe na uhakika kama mgonjwa anakwenda haja ndogo kama kawaida. Kwa mfano mtoto mwenye homa na upungufu wa maji mwilini, usimpe zaidi ya kipimo kimoja cha asprin mpaka ameanza kukojoa. Usimpe mtu sulfinamide ambaye ana upungufu wa maji mwilini.
FUATA USHAURI WA DAKTARI
Samahani kwa matatizo ya kiuandishi
Naomba kuwasilisha