JAMOS
Member
- Jul 7, 2016
- 84
- 35
Naomba ushauri ndugu zangu Kuna tabia ambayo siipendi kabisa, mtu kuja nyumbani kwangu bila kunijulisha au sababu ya msingi. Tabia hiyo inatokea mara kwa mara kwa watu wachache ambao nafahamiana nao lkn baada ya kuja nyumbani hawana suala la msingi la kueleza. Unakuta nimetoka kazini nimechoka Nahitaji nipumzike au Nina kazi ya kufanya ya muhimu lazima niikamilishe. Jambo hili linanikarahisha sana. Niwafanyeje watu hawa.