Ni USALITI ULIOKITHIRI... Tutoe Amri sasa.. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ni USALITI ULIOKITHIRI... Tutoe Amri sasa..

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eng. Y. Bihagaze, Jul 6, 2012.

 1. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #1
  Jul 6, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Bunge ( Chombo Muhimu Kama Mwakilishi wa mwananchi) linaendeleza vikao vyao vya kawaida wakati Mwananchi wanayemwakilisha anakufa Kwa kukosa matibabu ni USALITI ULIOKITHIRI

  Kwanini Bunge mmesaliti Mwananchi aliyewatuma mkamtetee.. Mipango, Sera, Sheria Na Bajeti mnazopitisha ni Kwa ajili ya nani Kama si mwananchi.. Sasa wakati mwananchi huyu mnayempangia mipango yote hiyo anakufa Kwa kukosa matibabu mtampangia nani mipango yenu hiyo .. MAITI!!???!!..

  Kwanini kuweka propaganda kwenye uhai Wa Mtu ?. Bajeti ikiwa mbovu, isopotekelezeka, yamkini mwaka mwingine itafikiriwa Lakini si maisha ya Mtu. Si Busara Bunge likafumbia macho sakata Hili la mgomo wa madaktari Kwa propaganda za kipumbavu..

  We Tanzania, Mimi Sijui Tanzania itaendelea kuwa kichwa kibovu hata lini, tunaheshimu taratibu za Mahakama ya Kazi, Lakini hadi lini kwani homa, operation au magonjwa ya ghafla yanajua hiyo mahakama ya kazi???

  Mbona Inshu iko wazi kwamba mnasema Doctors wamegoma kinyume Na maagizo ya mahakama kuu and mahakama ya kazi, Kwa hiyo mgomo ni batili, fine.. But yet unaendelea huo mnaouita batili sasa what mahakama ya Kazi can do kwenye ubatili huo??? Kama si propaganda kwenye pumzi ya mtanzania..

  Nimetembelea Leo Muhimbili utadhani Sekondari ambayo wanafunzi wako likizo, unakutana Na wanafunzi wachache walioko zam..nimeenda mwananyamala watu wapo kazini but wapo Kama 'hawapo.. '

  Nadhani Kwa Upeo wa Bunge letu, wangeacha mambo mengine mezani na kujadili Kwa kina kadhia Hili Na kuishauri serikali nini cha kufanya haraka kunusuru maelfu ya wagonjwa hasa waliotoka mikoani Kwa ajili ya tiba Muhimu MHML.

  Poa wabunge, mawaziri Na wengineo wasijione kwamba wao tu ndio viongozi wa kitaifa, Dr. Ulimboka Kama Mwenyekiti Wa Jumuia ya Madaktari naye ni kiongozi Wa kitaifa Na si ka-mtu-tu.. Jambo lililompata Na linalompata lazima lijadiliwe Kwa mapana Kama kiongozi Wa kitaifa Na mwananchi wa JMT..ili kuhakikisha dhana ya ulinzi wa kila raia ndio msingi wa serikali yoyote Duniani..
   
 2. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #2
  Jul 7, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Tunayo kila sababu ya Kutamka jambo Kama raia.. Na Jukwaa Tunalo ambalo ni mitandao yetu yote
   
 3. m

  mullay Member

  #3
  Jul 7, 2012
  Joined: Apr 4, 2012
  Messages: 79
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hata tukiongea unadhani wanatuelewa basi, maana kusikia wanasikia. Mnyika kila siku analia bungeni, kwanini isijadiliwe bungeni ile ripoti ya wabunge zaidi ya kusikiliza upande mmoja wa serikali.
   
 4. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #4
  Jul 7, 2012
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  Sii busara kuamini/kuheshimu mahakama isiyojiheshimu
   
Loading...