Ghiti Milimo
JF-Expert Member
- Jul 18, 2011
- 5,157
- 7,701
Duh! UngewaulizaWadau, wote tunafahamu kuwa, Serikali(Rais)ilitangaza kuwa, kila Jumamosi ya mwisho wa mwezi, itakuwa ni siku ya usafi kitaifa.
Wananchi, wakalipokea agizo hili, kwa mikono miwili. Lakini, ki-uhalisia, imekuwa ni kero kubwa!
Maisha kwa sasa yamekuwa magumu, wateja nao wamekuwa ni wa shida, patikana yao japo ni wachache, ni asubuhi, pamoja na mzigo wa kodi, lakini siku hii tunalazimishwa kufungua shughuri zetu saa nne na tano asubuhi! Ukifungua kabla ya hapo, unakamatwa!
Cha kushangaza, hao WAKAGUZI, wanachokagua, si USAFI, bali nani kafungua Duka/biashara yake kabla ya muda waliojipangia!
Mimi nawashauri, wangeturuhusu, tuwe tunafanya usafi kwa wakati wetu. Ila wao, wawe na muda maalumu, wa kukagua huo usafi. Kama mimi nitafanya usafi, usiku, alfajiri, hiyo iwe ni juu yangu!
Sina shaka hili tatizo lipo Nchi nzima! Mimi nipo Shinyanga mjini!
N kufunga maduka na sio usafi maana hata usafi wenyewe haufanyiki,Za asubuhi wana bodi.
Nipo najiuliza hapa hili suala la usafi kila jumamosi ya mwisho wa mwezi, najiuliza pesa ambazo wafanyabiashara wanazipoteza kwa kutofanya biashara kwa hayo masaa mawili, najiuliza kodi ambayo serikali inapoteza kwa hayo masaa mawili ambayo shughuli zinazimama kabisa, najiuliza jinsi ambavyo viongozi wa serikali za mtaa wanavyofuatilia kuhakikisha maduka hayafunguliwi ili hali mitaani kwao kuna mambo chungu nzima, mitaa kwao kuchafu mpaka jumamosi ya mwisho wa mwezi, najiuliza jinsi ambavyo polisi wanavyofanya patrol mitaa kuangalia maduka yaliyofunguliwa,najiuliza hivi usafi ni jumamosi ya mwisho wa mwezi tu, hivi usafi ni ratiba ya mwezi au.ni tabia, mila na desturi?
Kuna ndugu Leo asubuhi alikuwa ana shida ya hela ya haraka aiseee naenda vibanda vya kuwekea hela nakuta vimefungwaImenikuta Leo tanga.yaaan in kelo.unaweza kua na Shida mhimu sana ukashindwa kupata huduma.yaan SAA mbili mji maduka yote yamefungwa.kwa kweli hili suala liangaliwe kwa jicho LA tatu.tunaleteana kero zisizo na msingi.very stupid..nmekereka leo adi nikahisi kupasuka kwa hasira