njundelekajo
JF-Expert Member
- Dec 26, 2012
- 310
- 227
NI UPUUZI KUSHANGAA NYUMBA NA MAGARI YA WABUNGE
Nguzo Noel .R.
Nianze kwa kumnukuu Mbunge wa kawe Halima Mdee (tar 3/4/2016 jumapili) katika viwanja vya sokoni mkoani Lindi"Sisi wabunge mshahara wetu katika hati ya Misha hara inasomeka sh million 3,lakini posho na Pesa ya mambo ya kiutendaji inafikia million 10" mwisho wa kunukuu.
1.KWA mwaka
Ml 10×12=ml120
2.KWA miaka 5
Ml120×5=ml 600.
Nje ya mambo mengine ni ml600 kwa awamu moja ya ubunge(miaka 5)
Hivi mtu anayepokea million 600 KWA miaka 5 nje ya posho nyingine anashindwa kujenga nyumba gani ya kuishi TANZANIA? kwa magari yanayouzwa TANZANIA gari gani la kutembelea utashindwa kununua?
Bwa Adam Sicinsk mtaalam huyu wa masuala ya akili,kufikiri na founder wa IQ10 matrix anasema mtu kufikiri sawa sawa ni kufikiri kwa kutoa majawabu,tatuzi za changamoto ( Solution oriented thinker)
Tulichotakiwa tufikiri kama solution oriented thinkers ni KWA NINI TUMEIFANYA SIASA IWE INALIPA ZAIDI na sio magari na manyumba ya wanasiasa wanaolipwa Zaidi.
Hata mjadala WA mshahara wa rais tatizo lake ni hilihili tumeruhusu siasa kufanana na mgodi wa madini na sio mfumo wa kutupatia viongozi na watawala
Mitandaoni kumesambazwa picha ya nyumba na MAGARI yanayodaiwa ni mali za Mbunge wa mbeya "SUGU", Tabia hii inaanza kua sugu sababu hapo nyuma kulisambazwa (katika namna ya kushangaa utajiri) picha za NYUMBA ya marehem Deo Firikunjombe, mjadala wa Gari la Mbunge WA Iringa mjini (Peter Msigwa), picha za Gari la Mbunge WA korogwe(Prof Majimarefu) nk
Unaupima ubunge wa sugu kwa uzuri wa nyumba yake?unaupima ubunge wa sugu kwa bei ya Gari yake? Unaijua Mbeya kabla na baada ya Sugu?.Unapataga muda wa kumwangalia sugu bungeni?
Hivi sifa ya Mbunge mzuri ni kuishi kwenye nyumba ya udongo?Sifa ya msingi ya Mbunge ni kutembelea "bodaboda"
Madhara ya mtazamo huu utayaona wakati wa kampeni za uchaguzi. Wanasiasa kupiga picha wakila ugali na maharagwe,wakipanda daladala, wakinywa maji ya mtoni n.k
Tutaendelea kufanyiwa maigizo na wanasiasa kama tunaamini Umaskini ni sifa sahihi ya uongozi.
by Nguzo Noel .R.