Ni ujinga ulioje kumlaumu Ruge(Clouds Media Group) kwani ni dhahiri kuwa kamwe cha kuazima hakistiri makalio ! Ni jambo lililo wazi kabisa kwamba kiu ya wasanii wengi hususan wachanga ni kusikika Clouds! Lakini sidhani kama wamewahi kujiuliza kwa nini wanatamani kusikika mahali hapo kwa ukubwa zaidi na si kwingineko? Hili linanirejesha msemo wa wahenga wakiosema,"usione vyaelea ujue vimeundwa" Umahiri wa Clouds haukuja kama pepo za bahari ziletwazo na kupwa na kujaa kwa maji yake.Bali kwa machozi,jasho na damu vya wanaClouds wenyewe ndio yaliyoweza kujenga mpaka kufika pale.
Wasanii wanapaswa watambue kuwa Ruge Mutahaba ni mfanyabiashara,na kanuni kuu ya biashara ni kutengeneza FAIDA.Pasi na faida hiyo si biashara ni chuma ulete....Hasara si ajabu..Sasa wakati Ruge anatimiza kanuni hii wengine tunampa tuhuma za unyonyaji.Siwezi kusema sio kweli kwa sababu sina ushahidi.Yamkini ni kweli akawa mnyonyaji lakini je,ni nani anayependa kuona haki ya mwenye haki inadhurumiwa? Je mwenye haki ameshindwa kufikisha shauri hili mbele ya mabaraza ya waamua haki(mahakama)?
Hakuna bure,ukiona umepewa bure,ni wazi kuna mtu sehemu amegharamia hicho upewacho.Wakati nafsi yako inajiongopea mwenyewe kuwa unasaidiwa,na kwa makusudi ukijisahulisha kuwa Clouds si mali ya serikali na wala Ruge sio Waziri wa sanaa,utamaduni na Michezo.Na hata kwa bahati mbaya hautaki kukumbuka kuwa Clouds Media ni kampuni binafsi inayoendeshwa kibiashara na Ndugu Ruge ni Mkurugenzi wake wa vipindi na uzalishaji(ni jukumu lake la kila siku kuongeza uzalishaji ambao utaleta tunu kwa kampuni)
Hadithi inaanzia pale unaposogea katika viunga vya Clouds na kuomba usaidiwe,na kurugenzi ya uzalishaji inajiridhisha kuwa kuwekeza kwako haitakuwa kazi bure,unaondoka na tabasamu lenye bashasha ukijihisi una bahati ya mtende (kumea jangwani)! Lakini ujinga unatawala ufahamu wako kuona si busara kuhoji kuhusu makubaliano yenu,Wao(Clouds) watakupa utakacho,Je umeshafikiri jinsi gani wao watanufaika na uwepo wako ? (Bure gharama)
Taharuki huja pale ambapo wewe umekwishatimiziwa mahitaji yako na muda wa Ruge kurejesha mtaji wake pamoja na faida umewadia(Biashara)..Ghafla unajitia uhayawani na kupiga kelele za kuomba msaada kwa jamii.Na kwa kuwa sisi nasi tumeamua kujitia upofu wa mawazo tusiokuwa nao,tunaanza kulishikia bango swala hili na kumpa Ruge ushetani(kutoka kuwa malaika mkombozi mpaka malaika muhasi (Lucifer) ambaye hastahili tena) TUACHE UNAFIKI
Fahamu kuwa unaruhusiwa kuvunja mkataba muda wowote,endapo tu utaona kuna haja ya kufanya hivyo na hautakiuka kifungu chochote cha mkataba huo ( Rubby aliamua kuvunja kwa ulimi wake)
"Baniani mbaya kiatu chake dawa"
Umeomba/kuombwa uimbe bure,baadae unasema umeimbishwa bure.Huku ukitoa tuhuma zako zilizosheheni maelezo kedekede.Acha unafiki hakuna aliyekuimbisha bali uliimba mwenyewe bure.Kwa kuwa uliona fursa ya kufanya hivyo,ulifikiri kibiashara faida ambayo ungepata siku za usoni.Sasa umekwishaipata hiyo faida unaona aliyekupa jukwaa la kuimba alikunyanyasa (mnyonge, mnyongeni haki yake mpeni)
"Fahari wawili hawakai zizi moja"
WCB imekuwa chapa kubwa ya biashara (kongole).Na hiki hasa ndio kiini cha mgogoro,kwa kuwa tayari misuli ya fahamu za WCB imetanuka vya kutosha na kujizolea uzoefu katika biashara..Hivyo katika kila kazi watakayoifanya wanatanguliza mbele kanuni kuu ya biashara (faida).Hivyo basi wakati Ruge anataka kutengeneza faida kutoka WCB,na WCB wanataka kutengeneza faida kutoka kwa Ruge(Zogo) kila mtu anataka kumzidi kete mwenzie!!
"Mtenda akitendewa huisi kaonewa"
Ruge naweza kusema ni mbobezi katika biashara,kwani alivyoona hawezi kutengeneza faida kutokana na WCB akaamua kuachana nao.Lakini sasa WCB wakaona kuwa wameonewa na Ruge kwa kuwa hawatasikika tena Clouds.Dhambi ya kujisahaulisha kuwa Clouds ni kampuni binafsi na inajiendesha kibiashara inawatafuna.Wanadhani ni haki yao kuendelea kusikika (Ujinga).Badala yake wanaomba msaada kwa jamii kupitia mitandao ya kijamii wakitishia kuweka bayana maovu ya Ruge katika muziki.Kama kuna maovu ambayo yamefanywa na Ruge nadhani huu ni wakati muafaka wa WCB na wasanii wote wanaomshutumu Ruge kwenda kwenye mabaraza ya haki na kudai haki zao.....Swali je,siku zote Sallam alikuwa wapi kutoa huo uovu? Au ndio sizitaki mbichi hizi?
Tizneez