Dr Orb
Member
- Aug 4, 2019
- 10
- 40
Mambo vp wanajamvi, je unatamani kuwekeza katika tekinolojia lakini bado unasuasua, au ww ni Technopreneur na unahitaji kuongeza faida?
Hata mpango uko hivi, kuna tekinolojia hii inayotrend kwa kasi ya ajabu "IoT" yaan internet of thing. Kama umewahi sikia hii kitu au unaijua basi komaa mchongo ndo Upo huko sasa na kwa baadae.
Ngoja tudadafue kidogo mchongo wenyewe uko vp !
IoT ni tekinolojia ambayo inalenga kumuunganisha mwanadamu na mazingira yake kadri iwezekanavyo. Mazingira ikimaanisha mambo yote ambayo binadamu anaweza kuingiliana nayo na akayafanyia maamuzi. Mfano kilimo, mambo ya afya, usafiri, vifaa mbalimbali na mengine yote.
Hii ikiwa na lengo la kumrahisishia kazi binadamu na aweze kufanya mambo mengi na magumu kwa kutumia rasilimali chache tu.
Lengo kuu la tekinolojia hii ni kufanya kila kinachokuzunguka na unakitumia kuwa kifaa janja yaani "smart device" kwa mtazamo huu utaweza kuviratibu vitu hivi popote ulipo kwa kutumia kifaa kimoja tu kama vile simu, utepe, saa au mawani!!.
Ili kufanikisha hili msingi mkuu wa tekinolojia hii ni DATA/ taarifa ambazo zitakiwa zikikusanywa na vifaa hivi janja. Taarifa hizi zinachakatwa na kuhifadhiwa katika mfumo unaoweza kuleta manufaa kwa binadamu. Na taarifa hizo katika mfumo wa kuchakatwa zinaweza kutumika na kifaa chochote kati ya vifaa vyako ulivyoounganishwa navyo.
Mfano unaweza kuwa umevaa utepe ambao unaratibu mzunguko wa damu, utepe huo unakusanya taarifa kuhusu afya yako ya mzunguko wa damu na kuuhifadhi mtandaoni na taarifa zilizokusanywa na utepe zinaweza kutumika kumjulisha daktari popote alipo bila hata we we kujua, na daktari anaweza wasiliana na ww ikiwa kaona shda yeyote.
Hii imekaaje?... Iko poa eee, huu ni mfano mojawapo lakini kuna mamb mengi na makubwa unaweza kuyafanya hapa.
Tekinolojia hii sio mpya INA takribani miaka 20 tangu kuletwa mezani lakini utendaji kazi wake bado hauna umri mrefu.
Hii n fursa kwako ewe mdau wa tekinolojia kwa kuwa unaweza kuwekeza katika maeneo mengi mno, kumbuka tekinolojia hii INA lengo LA kumuunganisha binadamu na mazingira kwa hivyo fursa hapa sio lazima uwe Computer guy!!!! Unaweza kuwa na fani yeyote cha msingi ubunifu.
Internet ndio msingi mkuu wa yote haya kwa hivyo fursa yeyote utakayoibuni lazima iendane na internet...
Tuangalie baadhi ya maeneo unayoweza kuwekeza katika tekinolojia hii ya IoT.
1. Fursa za utengenezaji au uzaaji wa vifaa vya kielectroniki kama vile sensors, actuators, SIM cards, chips na vifaa vingine. Mfano wa makampuni katika eneo hili ni Huawei, Intel, Sumsung na mengineyo.
2. Kama kutengeneza na kuuza vifaa ni ngumu unaweza kufaidika kwa kuuza vifaa janja hapa mfano smartphone, smart watches, smart glasses,smartv na vinginevyo vingi.
3. Kama zote hapo huu ni ngumu kwako basi unaweza chukua fursa ya uunganishaji wa vifaa na data katika mtandao. Yaani anzisha huduma za kuunganisha vifaa na internet. Simply internet communication services. Mfano wa makampuni hapa kuna Vodacom, Airtel, Smart, Safaricom na mengineyo.
4. Hizi ngumu? Bado fursa zipo kibao nyingine ni hii ambayo ndio imebeba maana nzima ya tekinolojia hii ya IoT, huduma za kukusanya, kuhifadhi, kuchakata data/taarifa. Hapa ndio kwenye mkwanja wa hatariiiii. Mfano wa makampuni hapa ni Oracle, Google, IBM na Datalab(hawa jamaa nimeona ofisi zao Dar vingunguti lakin sijui wanajihusisha na nn hasa) na mengineyo.
5. Kama haya yote huyawezi IPO hii, kutoka huduma za kuwaunganisha wateja na kuratibu mifumo yote ili kufanikisha tekinolojia hii ya IoT inafanya kazi. Yaani system Integrators. mfano Our Company ( Orb Tech. LLC), IBM, na mengineyo.
6. Bado tu hujaona fursa hapo! OK ya mwisho hii kuwa mtaalamu au kutumia wataalamu wa kutengeneza program mbalimbali zitakazofanya kazi na mfumo huu wa IoT. Yaani Software programmers mfano ni Orb Tech LLC, ellipsis IBM, Oracle, Microsoft, Apple inc na Mimi Mwenyewe Niko hapa.
Kama hujaona fursa yyte hapo basi usijari unaweza kucheza kipengele cha mteja yaani kununua bidhaa na kutumia kwa manufaa yako binafsi. Hata hivyo kipengele hili kinawahusu wengi sana hata hauko peke yako.
Kwa wale wote ambao wameshawekeza katika tekinolojia nawashauri kwanzia sasa muanze kuufikiria na kuangalia namna gani mnaweza kuingiza uwekezaji wenu katika tekinolojia hii ya IoT kwa kuwa ndio future ya tekinolojia ya mwanadamu. Unaweza kupata msaada sehemu mbalimbali mfano hapa Orb Tech LLC.
Mwisho tumalize na ujuzi ambao ni wa lazima katika kufanikisha tekinolojia hii ya IoT.
1. Computer skills hususa ni Programming, Databases.
2. Electronic engineering.
3. Data Science.
4. Creativity
5. Ujuzi mwingine kama biashara, ujasiliamali, mawasiliano na vinginevyo.
Ni hayo tu kwa Uzi huu. All the best