Ni sawa mke kulazimisha mume amsomeshe?

shalet

JF-Expert Member
Feb 12, 2013
3,430
3,529
Habari zenu wakuu,
Hivi mtu umeoa mke toka nyumbani kwao kabisa kakaa na wazazi wote wawili mpaka unamuoa, unazaa naye mtoto mmoja baada ya miaka miwili unamwambia mama tuongeze mwingine wa pili analeta drama kuwa hataki kuzaa anataka asome kwanza kama vile ulimkuta yuko shule na hataki kusikia kitu. Ukimuuliza rengo la yeye kusoma ni nini manake umri umeenda anadai wake wenzake kwenye familia wamesoma yeye tu hajasoma kama vile kuna mashindano.

Elimu ni jambo zuri ila inakuaje mtu umlazimishe akusomeshe mtu mwingine ambaye kakuchukua kwa ajili ya lengo la kujenga familia na hata hiyo elimu haitaleta faida yoyote kwenye familia.

Hebu tusaidiane ndugu zangu ni sawa mke akulazimishe umsomeshe wakati umemuoa kwa shughuli nyingine.
 
We nae utakua MJINGA Kama utaki mkeo asome Ila ILA asitoke nje ya mkoa /asome na kurudi nyumbani
mkuu kusoma ni jambo zuri imagine wewe umetumia miaka mingi kusoma mpaka kuapta kazi unaamua sasa uanze kujenga familia mwenzako tena anataka kwenda shule hii haiko sawa/
 
Sio sawa mke kulazimisha kusomeshwa...

Huyo mke kwanza inaelekea hajitambui anasoma kimkumbo..

Vinginevo kama anania ya kusoma basi atumie hekima
 
Sio sawa mke kulazimisha kusomeshwa...

Huyo mke kwanza inaelekea hajitambui anasoma kimkumbo..

Vinginevo kama anania ya kusoma basi atumie hekima
huyu anataka kulingana na wenzake anaona hajasoma pekeake.
 
Sio sawa kukulazimisha ila ni sahihi kumsomesha hata kama haikuwa katika makubaliano ya ndoa yenu

Sema sasa alichokosea mke ni sababu aliyotoa kwako ya yeye kutaka kusoma . . .iko tu

Ila mkuu kama uwezo wa kumsomesha unao ,mpeleke tu akasome
 
Hivi kuolewa ndio mwisho wa maisha? Wengine mnauliza eti ooh kwani hujamtolea mahari, kwani mahari ni kitu kikubwa cha kufanya mtu asifurahie maisha yake? Kama anataka kusoma, hiyo ndio raha yake! Muache asome. Kwani akisoma na mimba ni tatizo?.
 
Sio sawa kukulazimisha ila ni sahihi kumsomesha hata kama haikuwa katika makubaliano ya ndoa yenu

Sema sasa alichokosea mke ni sababu aliyotoa kwako ya yeye kutaka kusoma . . .iko tu

Ila mkuu kama uwezo wa kumsomesha unao ,mpeleke tu akasome
Unamshauri mwenzako vibaya Aiseee!!

Ameshaambiwa hata mtoto mwanamke kagoma we unadhani nini kinaendelea hapo.
 
Kama ulimuahidi kumsomesha baada ya ndoa jibebe jikusanye umsomeshe. Kama haukumuahidi kuwa ngangari tishia utaenda tafuta wa kukuzalia mtoto nje. Lazima ajishushe

Hapo dawa ni kukubaliana arudi home asomeshwe na wazazi wake akimaliza arudi kwenye ndoa.

Kwenye ndoa tunajiendeleza, siyo kusomeshana kuanzia mwanzo.
 
Back
Top Bottom