Ni sawa mimi kumsaidia mwanae mwingine?

torondo

Member
Feb 21, 2016
89
93
Ilikuwa miaka kumi na moja iliyopita.Nilifapata mtoto na dada mmoja sasa sikuwa na mipango ya kuoana nae, nae pia alinipotezea sababu dada zake walikuwa na uwezo mkubwa na wakamshauri kuwa mimi siyo future boy kwake wakaninyima hata kumuona mtoto.

Miaka imeenda Mungu mkubwa mambo yamebadilika dada wamekosa jinsi ya kumsaidia mwanangu nikaingia kwenye majukumu yangu.Shida ni kwamba alizaa mtoto mwingine na jamaa mwingine mpaka leo nikimuuliza ni nani hajawai kuniambia tatizo ni kwamba sababu anaona natimiza wajibu wangu kwa mwanangu na matatizo ya huyu mwingine ananiambia mara ada,anaumwa sijui nguo za shule za sikukuu.

Je hii ni sawa wadau?
 
Kama unamsaidia basi ni sawa tu na kukutana na mtu njiani akakueleza shida zake ukaamua kusaidia. Lakini sio jukumu lako. Na mwanao ni vizuri ukamchukua maana kile unachompa mama lazima atakigawa kwa wote wawili
 
Nazani ushauri wako unafaa kuzingatiwa ipasavyo..!
 
Kama uko vzr its OK! Kama hauko vzr unamwambia, kikubwa asizoe tukusaidia ikaja baadae kugeuka wajibu wako! So unamsaidia halafu sometimes hata kama uko vzr unamwambia siko poa, unamsaidia mwanao pekee!

Akishazoe, itakuwa poa tu! Utatoa msaada utakapoweza at the same majukum yako unatimiza kama kawaida
 
Kumsaidia mtoto wa mzazi mwenzio ni jambo jema sana kwan utajenga mahusiano yao mema na watapendana kila siku na kubwa zaid atakupenda sana na utakuwa wa thamani kubwa kwao siku zote
 
sio lazima ni msaada tu hata kama anyuma laikunyima haki ya mtoto...hapokazi kwako, sio suala la sawa au si sawa ishu ni sio lazima sio wajibu wako yupo baba yake au mama yake yupo..mtot wako ni lazima na sawa...so kwa huyomwingine ni msaada tu hata akiomba si lazima so kama unayo na una uwezo fanya hivo ila kwa hiari kama huna uwzo unasita potzea...the choice is yours
 
Ilikuwa miaka kumi na moja iliyopita.Nilifapata mtoto na dada mmoja sasa sikuwa na mipango ya kuoana nae, nae pia alinipotezea sababu dada zake walikuwa na uwezo mkubwa na wakamshauri kuwa mimi siyo future boy kwake wakaninyima hata kumuona mtoto.

Miaka imeenda Mungu mkubwa mambo yamebadilika dada wamekosa jinsi ya kumsaidia mwanangu nikaingia kwenye majukumu yangu.Shida ni kwamba alizaa mtoto mwingine na jamaa mwingine mpaka leo nikimuuliza ni nani hajawai kuniambia tatizo ni kwamba sababu anaona natimiza wajibu wangu kwa mwanangu na matatizo ya huyu mwingine ananiambia mara ada,anaumwa sijui nguo za shule za sikukuu.

Je hii ni sawa wadau?
Kama uwezo unao sio mbaya ukimsaidia ila usijikalifishe,kama ulivyoona mambo hubadilika basi somo lilowapata dada zake baby Mama wako huenda na wewe likakupata,mwenyezi mungu akunusuru,kama uwezo upo fanya kama unatoa sadaka
hujui huyo mtoto kesho atakua nani huenda asikusaidie wewe lakini akijisaidia mwenye na ndugu yake ambae ni mwanao
pia sio mbaya...
 
Kiaina ni sawa yeye kukushirikisha. Cuz changamoto anazopitia kwa huyo mtoto mwingine, zinamuathiri mwanao pia kwa namna flani.
 
Kusaidia siyo lazima, ila kama umeamua kusaidia kwa moyo mmoja (in good faith) endelea tu na moyo huo huo.

NB: ni muhimu kumuweka wazi kuwa siyo jukumu lako, hivyo na yeye ajipange kwa namna yake. Kwani unaweza kuta anachomfanyia huyo baba mwingine ni sawa na alichokufanyia wewe miaka hiyo ila tu kwa sasa wewe ndiyo umechukua nafasi ya Dada zake.
 
Back
Top Bottom