Ni sawa kuweka nguzo Mita 5 kutoka kwenye nyumba?

Kimla

JF-Expert Member
Jun 8, 2008
1,811
2,000
Nisaadieni, watu wa umeme vijijini wameweka nguzo ya umeme Mita 5 kutoka kwenye nyumba. Je ni sawa? Je standard ya nguzo ya umeme inabidi iwe mita Ngapi kutoka eneo husika?
 
mwasu

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
10,208
2,000
Hawaeleweki, kuna majirani huku kwetu wamegombana sasa kila mtu kavuta umeme kila mmoja ana nguzo kwenye nyumba yake wakati nguzo moja ingeweza kutumika na wote, ajabu tanesco nao wameunganisha umeme hivyo hivyo, kila mmoja na nguzo yake na hataki ushirika na mtu..
 
Mgodo visa

JF-Expert Member
Nov 1, 2016
3,243
2,000
Nisaadieni, watu wa umeme vijijini wameweka nguzo ya umeme Mita 5 kutoka kwenye nyumba. Je ni sawa? Je standard ya nguzo ya umeme inabidi iwe mita Ngapi kutoka eneo husika?
Ni sawa....au unataka kushindana na MTOTO wa IKULU...!!

Changamkia FURSA hiyo..jivutie Umeme kiulaini..tayari umesogezewa Nguzo, bado unaanza kulalamika...!

Wabongo bwana...!! Sijui nani ameturoga..!!
 
marxlups

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
13,222
2,000
Hawaeleweki, kuna majirani huku kwetu wamegombana sasa kila mtu kavuta umeme kila mmoja ana nguzo kwenye nyumba yake wakati nguzo moja ingeweza kutumika na wote, ajabu tanesco nao wameunganisha umeme hivyo hivyo, kila mmoja na nguzo yake na hataki ushirika na mtu..

Tanesco wana shida kwenye mambo ya survey na engineering hasa kwenye nguzo, kama kungekuwa na eneo la wazi la kutolea kero zikafanyiwa kazi ingesaidia sana, kuna hii link hapa TANESCO Special thread: Tupe maoni, maswali, malalamiko na hata ushauri hata ukiwaandikia usitegemee watachukua hatua naona ipo kama danganya toto kwamba wapo kumbe hawapo
 
Kabisa wanafanya kazi kizamani mno, hivi inaingia akilini kweli kila nyumba iwe na nguzo?! Halafu mikoani hata ukiomba mita ya luku ni shida kupata unaambiwa subiri, subiri, ukiomba mita mpya kwenye nyumba nyigine ni shida unaambiwa weka nguzo wakati kuna nguzo uliyokuwa una share umeme na nyumba nyingine wanakera sana, nadhani hili la nguzo limekuwa biashara sasa.
 
Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
6,692
2,000
KWA MIPANGO MIJI IPI TULIYO NAYO MKUU,HUKU KWETU KUNA NGUZO IMEUNGANA NA UKUTA WA NYUMBA
 
Qurie

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
3,163
2,000
Hawaeleweki, kuna majirani huku kwetu wamegombana sasa kila mtu kavuta umeme kila mmoja ana nguzo kwenye nyumba yake wakati nguzo moja ingeweza kutumika na wote, ajabu tanesco nao wameunganisha umeme hivyo hivyo, kila mmoja na nguzo yake na hataki ushirika na mtu..
Hahahah sijui kama ina ukweli lakini haya ni maajabu
 
mwasu

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
10,208
2,000
Hahahah sijui kama ina ukweli lakini haya ni maajabu
Sina sababu ya kuongea uongo, hata mimi niliporudi kutoka mihangaiko yangu nikakukuta nguzo mpya niliuza tu Tanesco walikuwepo au jamaa kajichimbia nguzo mwenyewe nikaambiwa walikuwepo, sasa kituko kikubwa ni kuwa kwenye nguzo ambayo jirani mmoja alichukulia hapo huyu mwingine kaenda kuomba KANYIMWA kisa, alimzuia kuweka nguzo katikati ya eneo maana wao walitangulia kujenga kabla ya huyu mwenye nguzo yenye umeme amekomaa nguzo yenye umeme itolewe iweke katikati ya wote kisa pale alipowka imebana gate, na Tanesco wakaona sawa hao wakasepa wakaacha mzozo, hivi viwanja vya kupimiwa na miguu umasaini ni shida.
 
Ila tanesco hawan cha kupoteza maana hiyo nguzo hawakupi bure ni wanauza
 
kinjumbi one

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,647
2,000

kinjumbi one

JF-Expert Member
May 27, 2015
1,647
2,000
Inategemeana na lalamiko pia seriousness ya Meneja wa eneo husika Mkuu
Lalamiko langu lilihusu eneo letu lilikua halina Umeme na tanesco waliokua wanazunguka zunguka tu tangia 2015, Baada ya lile bandiko langu yani fasta tu walinitaka niende pm yao ili niwaelekeze vizuri na nitume namba ya simu. Nashukuru siku iliyofuata akanipigia meneja wa eneo la ukonga na kunisikiliza live, lkn issue ilikua si ya eneo lake, ila aliahidi suala hili atafuatilia kwa karibu yeye mwenyewe kwa meneja wa eneo husika na kuahidi atanipa mrejesho siku inayofuatia. Kweli bwana siku aliyoahidi mchana na mapema akanipigia na kunieleza suala langu ameshughulikia meneja wa eneo langu atanitafuta lkn pia alinipa namba ya simu wa meneja wa hilo eneo. Wakaniita ofisini kwao, nami nikawashtua wananchi km sita hivi tukaenda kuwaona. Tunashuru ndani ya wiki mbili tu kwa sasa eneo letu lote lina Umeme.lkn shukrani za kipekee zimuendee meneja tanesco wa ukonga. Kwakweli simfahamu jina wala sura lkn alijtolea sn ktk hili. Ktk utumishi wa umma wa ki Africa huwa kuna longo longo sana lkn yeye amejitahidi, Mungu amuangazie kila lilo jema kwake.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom