Anayelikubali jina hilo ndiye ametangaza ugomvi na mtukufu mwenyewe.Unaweza kumkandamiza mtu kwa mamlaka na uwezo ulio nao na akawa hana kabisa uwezo wa kujitetea,basi akafika mahali akaona akuite mungu nisamehe,ee mtukufu!Wewe unayeambiwa maombi hayo kwa kiburi ukaukubali utukufu huo,Mungu atakishusha kiburi chako bila shaka.Kuna siku utasikia maumivu halisi na malipo ya maonevu uliyofanya yatakurudi.Mungu ataliinua jina lake dhidi yako,maana hakuna aliye mtukufu zaidi yake.Mwl Nyerere mzee wa watu alilikataa jina hilo na hakuwa mtu wa kiburi na kujikweza.