Ni salam Tu kwako wewe

ngalyas_t

Senior Member
Joined
Dec 5, 2012
Posts
175
Reaction score
58
Kama ni Kweli yanayotokea huko DUNIANI, yaani tumeamua
-kupiga
-Kutesa
-Kunyanyasa
-Kufanya hila
-Kuua
Kwa hakika hatutafuti uongozi wa kuletea watu maendeleo, bali ukwasi na umaarufu.
Huo uongozi wa dhuluma hauwezi kuwa na baraka za Mungu.

KWA WALIOHUSIKA
1. Ili muishi vizuri ongezeni kiwango cha ubaya kusudi mwogopwe kama mtakavyo., maana mkilegeza tu ubabe wenu, mmekwisha.
2. Kwa wale waliopokea fedha(Rushwa), wewe ndiye LOFA, maana huna mpango na kizazi chako, bali tumbo lako kwasasa ( MYOPIC VISION)
3. Mliotiii amri ya kupiga watu, kwa sababu tu mna vitendea kazi, hivi mkirudi nyumbani mnajisifu kwamba kazi ilikuwa ngumu, halafu mnapewa pole?
Kwa taarifa yenu hamna tofauti na wazazi wanaobeba madawa ya kulevya eti kutafuta pesa kwa ajili ya maisha mazuri ya watoto wao, [emoji35][emoji35]
4. Wewe uliye na unayetoa amri ya kutekeleza dhuluma na hila ili kupindisha ukweli, ni kwamba kwa mtazamo wako; unaona umefika highest level na kana kwamba hakuna kama wewe. Ila umesahau hauna amri katika PUMZI unayotumia

UJUMBE KWENU
- Mungu asiwaondoe duniani hivi karibuni, ili baadaye watoto wa watoto wenu washuhudie aibu yenu.
- Jifanye hamuishi Duniani, maana yatakayotokea baadaye hayatawahusu ninyi na jamaa zenu.
-Ukweli ni kwamba hamjiulizi siku hizi nafasi mlizonazo zikitoweka, maisha yenu yatakuwaje.
- Hamna maono,
- Mnawaachia nini watoto wenu? Je, na wao waue ili kupata nafasi.?

MAAMUZI YA SASA NI MBEGU YA MATUNDA YA BAADAYE.
MWISHO
-Damu ya Habili haikumwacha Kaini Salama.
-Damu ya Uria haikumpa raha Daudi.
-Damu ya Stephano haikumuimarisha Sauli.
Tukimaliza kupiga na kupata majeruhi wa kutosha, Basi tuwaandalie na PF3 kisha tupeleke na dawa hospitalini. Nasi wahusika wa hujuma hizi tusisahau KUKATA BIMA YA KUISHI MILELE.

Wasalaam!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…