Tayukwa
JF-Expert Member
- Dec 11, 2014
- 2,171
- 4,398
Mada tajwa hapo juu yahusika,
Wakuu kuna baadhi ya watu huenda kwa waganga wa kienyeji wa aina mbali mbali ili kutatuliwa matatizo yao. Wapo wanaofanikiwa na wapo wanaoendelea kupoteza pesa kwa waganga hao.Kutokana na imani zao ziwe za kidini au vinginevyo lakini watu hufuata njia hii mbadala ili kutatua changamoto zao zinazowakabili.
Natoa mifano kadhaa kutoka kwa baadhi ya mambo niliyoyashuhudia kuna familia moja ya jirani hapa wao kila siku hulalamika kuwa wanamuona baba mwenye nyumba huwajia usiku ili kuwafanya wasiwe na maendeleo yoyote yale, hivyo huangaika sana ili kupata manusura. Katika hangaika zao hizo walienda kwa mganga mmoja ambae aliwatoa nyoka, misumali na baadhi ya vitu km hirizi n.k
Kwani mmoja wao alikuwa anasumbuliwa na mguu hivyo vitu hivyo alitolewa mguuni. Mganga aliwaambia kuwa kwa sasa wapo safi kwani tatizo walilokuwa nalo limekwisha na kama kutatokea jipya basi wataenda tena. Lakini ajabu ni kwamba baada ya kutolewa vitu hivyo walienda sehemu nyingine baada ya kusikia kuwa huko ndio kuna mtaalamu bingwa wa mambo hayo hivyo walipofika huko wakaambiwa kuwa wamerogwa na wanahitaji tiba kubwa hivyo wakafanyiwa tiba nyingine baada ya ile ya kwanza.
Kuna ndugu yangu mmoja hivi ana elimu ya kutosha tu katika upande wa dini na shule lakini amekuwa muumini sana wa haya mambo ya kwenda kwa waganga lakini sijayaona maendeleo yoyote kimaisha aliyoyapata hata kama ana kazi nzuri.
Binafsi naamini uchawi upo kupitia mambo mbalimbali, lakini nina mashaka na hawa waganga na baadhi ya wateja wao juu ya mambo yao yote. Sijaona mtu anaenda kwa mganga na kuambiwa hana tatizo, maagizo ya ngozi za simba, chui, kupeleka ng'ombe, mbuzi au kondoo, kuku, bata nk ni jambo la kawaida kwa mganga kuagiza ukishindwa kuvipeleka vitu hivyo basi muachie kiasi cha pesa ili avitafute yeye atajua anavitoa wapi. Wapo waganga wanaoaminiwa na wapo wale waganga njaa.
Vipi kwa upande wako wewe umefurahia jambo gani toka kwa mganga au waganga wa kienyeji ambalo unaona faida yake ni kubwa kuliko mtaji ulioutoa kwake na mafanikio yako yapo vipi baada ya kwenda kwa sangoma.
NB: Sina nia nao mbaya au ugomvi na hao waganga ila naomba tusaidiane ufahamu ktk hili kwani nashindwa kutofautisha uganga na mazingaombwe hasa ule wa kutoa vitu mwilini.