Ni nini kinaendelea Manispaa ya Ilala, Imeisha uzwa?

Ni nini kinaendelea Manispaa ya Ilala, Imeisha uzwa?

Magano

Member
Joined
Nov 19, 2012
Posts
18
Reaction score
6
Jana majira ya mchana nilikuwa katika ofisi za manispaa ya Ilalahapo katika Sehemu ya kufanyia malipo, meya kijana alikuwa ameongozana na akina mama wawili staff wa benki NMB walikuwa ni kama wanafanya makabidhiano mbele ya waandishi wa habari ambao walikuwa wakipiga picha mfululizo kwakuwa tulikuwa kwenye foleni ya kulipia sikuweza kusikia sawasawa makabidhiano yale ila yule mama mkabidhiwa alikuwa anaelezea uzoefu wake wa kukusanya mapato na jinsi atakavyo boresha huduma za hapo mahali baada ya meya na wageni wake kutoka akatuacha wateja tuliopo hapo na maswali mengi vichwani mwetu kwamba hivi inakuwaje makabidhiano wanafanya kienyeji namna hiyo kwa taasisi ya serilali maana hata makubaliano yaliyo kuwa yakifanyika hapo ni sawa na muuza genge sokoni anapo kubaliana na mnunuzi wake.kilicho tushangaza sie tulio kuwapale ni kwamba hivi sikuhizi meya an uwezo wakuamua tu kuanza kugawa tenda za kuendesha halmashauri kwa uamuzi wake tu maana kwa jinsi mjadala ulio kuwa unaendelea pale haioneshi kama kuna tenda inayoweza kutangazwa pale meya huyo alidiriki hata kunipokonya fomu yangu ya malipo ili awaoneshe wale akina mama nadhani ili wavutiwe na kiasi nilicho kuwa nalipia ili biashara iende haraka haraka nahakukua na kibaya zaidi upande wa halmashauri alikuwepo meya pekeyake bila kuwa na muhusika mwingine wa halmashauri yaani diwani mwenzie wala mtumishi wa halmashauri kwa niaba ya mkurugenzi kwakweli hali hii inatisha sana, kwa habari zilizopo vianzio karibu vyote vya mapato vya ilala vimebinafsishwa na huyo meya kijana amekamata baadhi ya tenda muhimu kwa kutumia kampuni ya TIRIMA! (ANGALIZO : 2015 karibu kila mwanasiasa ana malengo nayo, hivyo tukiwafumbia macho hawa wanasiasa wataziua hizi halmashauri zetu tutakosa huduma muhimu). Naomba kuwasilisha.
 
Back
Top Bottom