Poleni sana!Waumini tunalipa, kwetu tumepangiwa laki mbili kila muumini. .
Tatizo siku hizi michango inasuasua kutokana na Ukata wa wananchi. ....Muda uliobaki ni kidogo sana. .........Mungu tuhurumie
Uchochezi hahahaahaaaNyie waumini mnaolipa hilo deni mna roho ngumu hatari, pesa ale mwingine alafu gharama alipe mwingine daaaah
Sina uhakika kama huu uzi uliwai kuwepo au laaah.Kama mtanzania mpenda kujua nini kinaendelea katika nchi yangu ikiwemo kisiasa, kiutamaduni, kiuchumi na kijamii pia, leo nikiwa Arusha nikakuta story inayohusu dayosisi ya kaskazini ikijumisha majimbo ya Arusha na Manyara kama sijakosea kuwa wanadaiwa na benki ya CRDB KIASI CHA BILIONI 13 NA NUSU
Katika hizo story nikasikia kuwa wasipo timiza hilo deni , mali za dayosisi zitapigwa mnada ikiwemo hospitali ya Selian, na hilo deni nasikia limetokana na watu kufanya ufisadi katika moja ya vitega uchumi vya dayosisi hiyo ya hoteli inaitwa Corridor spring,.
So kutokana nilikuwa na haraka sikuweza kujua kisa kizima, nimeleta hapa kwq wanaojua sakata hili, imekuweje mpaka dayosisi inadaiwa kiasi kikubwa hivyo ni nini kilito
kea hasa...nawasilisha
Poleni sana!
Waumini tunalipa, kwetu tumepangiwa laki mbili kila muumini. .
Tatizo siku hizi michango inasuasua kutokana na Ukata wa wananchi. ....Muda uliobaki ni kidogo sana. .........Mungu tuhurumie
Kondoo wa bwana wafanyaje?Wengine wafisadi,nyie mlipe? Kweli elimu inatakiwa.
Ndio mmedanganywa hivyo? Wengine wale nyie mlipe?Kondoo wa bwana wafanyaje?
Mimi nimeleta kile nilicho kisikia kama wewe unaangalia namna ya uandishi hilo halinihusu cha msingi mimi nilitaka kujua zaidi kwa hicho nilichokisikia,,,, na sorry ni kaskazini kati, mimi sio mtaalamu wa ugawaji wa dayosisi.Dayosisi mtu au taasisi?
Na kama ni taasisi, basi sema inajihusisha na nini kwa watu gani
Samahani lakini.
Ila ukweli ni kuwa umepost hii kitu kana kwamba umemtumia rafiki yako "private message" huku mkijuana ninyi kwa ninyi mnaongelea nini!!
Kumbuka hii ni "public forum" na unapoanzisha mada, basi iweke ktk namna ambayo kila mtu ataielewa kwa urahisi ili ipate response tarajiwa.
Else, mada yako haiko kamili....jisome tu utaelewa !!