ni nani huwa anatoa taarifa za kufeli kwa majaribio ya korea kaskazini

Robert James Masunga

JF-Expert Member
Mar 28, 2017
414
395
vyombo vya magharibi vimeripoti kwa mara nyingine tena kuwa korea ya kaskazini imefanya jaribio la kurusha kombora la masafa marefu lakini jaribio hilo limefeli. na hii ni kwa mara ya nne mfululizo.

jambo hili linafikirisha. korea kaskazini inatajwa na watu wa magharibi kama 'secretive regime' kwamba ni utawala wa siri. naa tunaelewa maana ya siri: ni ile hali ya kufanya mambo kwa uficho ili usiotaka wajue wasijue.

ni kweli korea kazkazini imekuwa ikitoa 'alert' kuwa itafanya jaribio la kurusha kombora na hakuna wa kumzuia. na kweli wanafanya hivyo. lakini inapotokea jaribio likafeli serikali ya kim hawatoi alert badala yake wanaotoa alert wanakuwa wabaya wao marekani na washirika wake.

je, ni nani anayetoa siri za kufeli kwa majaribio haya?

maxresdefault.jpg
 
Back
Top Bottom