Ni nani hasa walipaswa kuwepo ktk orodha ya wauza unga kama waliotajwa wanatetewa kwa ushabiki?

Shukrani A. Ngonyani

JF-Expert Member
Feb 23, 2014
1,182
2,015
Mwaka 2014 niliandika mada nyingi hapa jamvini nikiwa naungana na akina EMT na wengineo juu ya madawa ya kulevya tukitoa mwongozo tofauti kwa serikali namna ya kukabiliana na hili.

Niweke maslahi binafsi mbele; "sijawahi kuwa mwanachama, mpenzi, wala sijawahi kupigia kura mgombea wa CCM ktk uchaguzi wowote".

Ila Kitendo Cha serikali kupitia mh. Paul Ciprian Makonda kuanzisha vita hii ni moja ya mafanikio kwangu na kwa taifa kuwa sasa kuna juhudi ktk kumaliza tatizo hili. NAIPONGEZA SERIKALI.

Ila nataka kuchokoza mjadala hapa, kumekuwa na sintofahamu toka majuzi mara baada ya kutawa watuhumiwa wanaojihusisha na madawa ya kulevya, hasa wasanii, Mwanasheria wa CHADEMA kaka yangu Tundu Antipas Lissu akaja na kejeli kuwa Makonda kataja dagaa, ataje na papa pia

Mh. Makonda akaona isiwe tabu, kataja mapapa akiwemo bosi wa mh. Lissu.

Leo imegeuka vita ya CCM vs CHADEMA, badala ya vita ya wauza unga na wananchi.

MBOWE anatafuta huruma, kwa vile CHADEMA wanaonewa kwa sasa(huu pia ukweli pia) basi ionekane na Mbowe Pia anaonewa kama mwenyekiti wa CHADEMA na mwenyekiti mwenza wa UKAWA.

Wauza madawa ya kulevya ni watu wenye heshma ktk jamii na wenye pesa zao, kama si Mbowe Na Manji tukitaka atajwe nani?
 
Naamini ungetajwa wewe ingeaminika zaidi!

Hao waliotajwa zaidi ya mia, wamekutwa na msokoto mmoja tu bangi!
 
Umeanza vizuri lakini busara imepotea mwishoni unapoonekana kushabikia washukiwa, watuhumiwa na wahalifu kutajwa hadharani wakati utaratibu wa kuwaita polisi bila kwenda mbele ya vyombo vya habari ndiyo ulio sahihi.
Inawezekana wakawa wanajihusisha au la, kinachopigiwa kelele ni upumbavu wa kutaja watu hadharani kana kwamba imethibitika ni wahalifu. Unawezaje kutumia tetesi za mabaunsa bila kuzithibitisha halafu unautangazia umma hadharani.
Jitathmini kiwango chako cha fikra mkuu.
 
Hatupingi watu kukamatwa,tunapinga utaratibu uliotumika wa kuwaita watuhumiwa kupitia media ili khali bado uhakika wa uhusika wao haupo bado
 
Naamini ungetajwa wewe ingeaminika zaidi!

Hao waliotajwa zaidi ya mia, wamekutwa na msokoto mmoja tu bangi!
akili za bavicha hizo.kwa hiyo kukutwa na msokoto mmoja kwa sio tatizo?una uhakika gani kama jana yake alimaliza kuuza gunia zake 100 za bangi akabakiza msokoto wa kuburudisha akili?
 
wale walikuwa watumiaji(mateja) sasa hivi anadeal na mapapa makubwa akina Kanjibai, Mchunguzi Gwajemali, Zungu la Sembe na Mboye
 
Kma ktumia vyombo bya habari ndio ksa bc na wao wacngewaita waandishi wa habari kukanusha hzo taarifa
 
Watanzania ni watu wa ajabu sana. Leo hii badala ya kumuunga mkono makonda wao wanakuwa wakwanza kumkatisha moyo.
Huko bungeni ndio kabisa wamegeuka na miungu wasikosolewi. Kweli nimeamini hii vita ni kubwa sana lakin tulio wengi kwenye ukweli tutashinda.

Wapinzani nao waajabu kabisa. Katuhumiwa mbowe kama mtu binafsi ila sasa wanalidaka na kulifanya la chama, je tuamini sasa kuwa mbowe ndiye chama ama? Kwanini asijitetee yeye kama yeye na sasa analifanya jambo lionekane la kisiAsa kuliko uhalisia wake?

Kila wakati tunachukizwa na tabia ya baadhi ya viongozi serikalini kushindwa kutofautisha serikali na chama. Sasa leo hii hata hao wapinzani wanashindwa kutofautisha mbowe kama mtu mwingine yeyote na chama, hii ni aibu kabisa.

Bila kujali kama tuhuma ni za kweli ama la lakini hapa wapinzani kwa ujumla wamechemsha na hapaswi kurudia tena makosa hayo. Mbowe pia ajifunze kutenganisha ishu binafsi na zile za chama vinginevyo kuna wakati italeta shida.
 
Amini amini nawaambia, Makonda atashindwa vibaya sana kwani hakuwa na strategies ktk hili, kwanza hakushirikisha vyombo vya dola na wakuu wake ili wawe na mkakati wa pamoja. pili ametaja watu bila hata kupata ushahidi ili aweze kuwataja rasmi. huko mbeleni wote watakwenda mahakamani ili kusafishwa na kudai fidia za kufa mtu.
 
Hatupingi watu kukamatwa,tunapinga utaratibu uliotumika wa kuwaita watuhumiwa kupitia media ili khali bado uhakika wa uhusika wao haupo bado
Makonda aviache tuuu kwani vinamuhusu nini??
Haya maazimio ya bunge hayoooooooooo...

Akizubaa atatoka kwa aibu na mwisho wa siku atajikuta jera miaka kadhaaa

Nchi hiii... Ningekuwa mi ni makonda walahi wakili wangu angekuwa tundu lisu

Lisu msaaada wako na ushauri wako kijana anauhitaji zaidi kajidai kuheshimu mawazo yako ili ataje wauza unga sasa dom kimenuka
 
Amini amini nawaambia, Makonda atashindwa vibaya sana kwani hakuwa na strategies ktk hili, kwanza hakushirikisha vyombo vya dola na wakuu wake ili wawe na mkakati wa pamoja. pili ametaja watu bila hata kupata ushahidi ili aweze kuwataja rasmi. huko mbeleni wote watakwenda mahakamani ili kusafishwa na kudai fidia za kufa mtu.
Hivi alimshirikisha sirro kama chombo cha dola au kama jamaa yake wa karibu??
Makonda madhara ta vyeo vya kupewa kutoka mfukoni mwa mtu usiinue kichwa, sasa ona yaliyojiri aseee

Utajieleza kwa yale majamaaa na hivi huko ni kimya kimya!! Sijui kitakachotokea
 
Back
Top Bottom