Ni nani aliyemtuma Balozi Juma Mwapachu?

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,903
Petro Magoti


ALIYETUKANA na Kumdhalilisha Mama Maria Nyerere na Mh Mzee Alli Hassani Mwinyi.
Wahenga walisema kuwa ukimwona Mbwa juu ya mti ujue kapandishwa!

Balozi Juma Mwapachu ametangaza kurudi ndani ya Chama cha Mapinduzi. Amesema ameamua kurudi ndani ya chama hiki baada ya kuondoka na kukikana kikiwa katika uchaguzi mkuu tarehe 13.10.2015. Balozi anasema aliondoka kwa sababu alichukizwa na chama kumuondoa Mh. Lowassa katika kinyang'anyilo cha Urais.

Juma Mwapachu anachagiza sababu yake hiyo kwa kusema kuwa walikubaliana wao wiki mbili kabla ya kupiga kura waondoke ndani ya chama kwa mkupuo ili chama kiweweseke na kushindwa vibaya.

Kwa kauli yake hii Balozi Mwapachu anasema kuwa alidhamiria kukiangusha chama hiki ili kishindwe katika uchaguzi mkuu. Kwa maana nyingine anasema kuwa kama matarajio yake haya yangalitimia hakuwa na mpango na Chama cha Mapinduzi kwani angeteuliwa kuhudumu kama waziri wa mambo ya nje kupitia serikali ya upinzani.

Nani kamtuma Balozi Mwapachu kusema kuwa ameamua kurudi katika chama cha Mapinduzi ili kunusuru biashara zake na rafiki zake? Nini maana ya maneno haya?

Ukimsikiliza vema Juma Mwapachu utaona kuwa swala la kuondoka ndani ya chama na kurudi ni uamuzi wao kwa maslahi binafsi kana kwamba CCM na serikali hii ni mali yake na rafiki zake.

Mwapachu amesema ameamua kurudi ndani ya Chama cha Mapinduzi leo. Kwa kauli yake ni kwamba hakuomba kurudi ndani ya chama isipokuwa ameamua tu kurudi na akapokelewa kama shujaa!

Kwa uamuzi huo Mwapachu anadhihirisha kuwa bado anao uwezo mkubwa yeye na washirika wake wa kuamua watakavyo ndani ya CCM.

Jambo muhimu kuliko yote katika filamu hii Mwapachu ni kuwa yeye ameamua kuwataja wasaliti wengine ambao alishirikiana kuhujumu chama wakati wa uchaguzi. Viongozi wa CCM Kata ya Mikocheni waliompokea katika kipindi ambacho Mwenyekiti wa Chama Taifa ametangaza kiama dhidi ya wasaliti wa chama. Wamempokea kwa kuvunja taratibu za chama, hawa wamedhihirisha kuwa wamekua na ushirikiano wa karibu na Balozi Mwapachu hata baada ya yeye kukihama chama.Balozi ametoa pesa sh. milioni moja ya ukarabati wa ofisi ya Kata ambayo waliitumia kupanga mipango ya kukihujumu chama cha Mapinduzi. Nitunze nikutunze!

Kwa mujibu wa kanuni ya UONGOZI NA MAADILI ya chama cha Mapinduzi toleo la 2012, katika FUNGU LA NNE, Ibara ya(8)Ibara ndogo ya (2) kipengele namba (ix) inalitambua kosa la Balozi Mwapachu,kosa la usaliti kama kosa kubwa kuliko yote ndani ya Chama cha Mapinduzi na adhabu yake ni kufukuzwa uanachama. Adhabu hiyo imefafanuliwa vizuri katika kipengelele hicho cha tisa sehemu ya (a-c).(Tafadhari rejea)

Balozi Juma Mwapachu alikisaliti chama wakati ambapo chama kilihitaji zaidi msaada wake,akakiacha kiangamie kwa bahati kikanusurika kwa mapenzi ya Mungu.

Kwa mujibu wa Katiba ya CCM Toleo la 2012,Juma Mwapachu alipoondoka CCM na kujiunga na chama kingine akawa amejifukuzisha mwenyewe uanachama wa CCM.

Mwapachu ameamua kurudi CCM kwa namna ya pekee! Amewaita waandishi wa habari,akatangaza kuwa ameamua kurudi CCM na Viongozi wa Kata ya Mikocheni wakampokea na kumkabidhi kadi ya Chama.

Kwa maneno mengine ni kuwa hakuna vikao vya chama vilivyoketi kumjadili Mwapachu pamoja na uzito wa jambo lenyewe. Mwapachu ana jeuri kubwa!

Kimsingi Mwapachu ameonesha jeuri kubwa,kiburi na dharau kubwa katika chama kikongwe na Imara kama CCM. Mtu mmoja aliwahi kuniambia kuwa Lowassa ana nguvu kubwa na jeuri ya ajabu,sikuelewa maana yake kwa wakati huo,baada ya tukio hili la Mwapachu naanza kuona maana ya maneno yale. Ni imani yangu kuwa Lowassa ameanza mikakati rasmi. Anajiandaa na ushindi kama alivyoahidi ktk balaza kuu la chama chao. Hii ndio tabia yake!

Ni nani aliemtuma Balozi Juma Mwapachu?
Sijaelewa ni kwa namna gani Mwapachu amekua na jeuri kubwa kiasi hiko dhidi ya chama tawala na hata apate nafasi kubwa ya kukidhihaki chama mbele ya waandishi wa habari. Zamani hapakua na michezo kama hii maana baada ya kauli yake hatua kali zingefuata nyuma yake.

Balozi Juma Mwapachu ametudhihaki vya kutosha!
Ametudharau vya kutosha!
Ametuonea vya kutosha.
Hivi ni nani aliemtuma Balozi Juma Mwapachu?
Na;
HAPA KAZI TU
 
Teh teh nasubiria Mkwere akimpigilia nyundo ya kichwa kwa kumfuta uanachama ,Maskini Mzee wangu Mwapachu sijui uso wako utauweka wapi
 
Waliompokea alipohama niliwashangaa na bado ninawashangaa wanaompokea sasa anaporudi hasa kwa kauli hizi "kuwa ameamua kurudi katika chama cha Mapinduzi ili kunusuru biashara zake na rafiki zake.
 
Labda anaweza kuwa ni mmoja wapo wa wenye CCM kwa sababu Mwenyekiti alishasemaga CCM ina wenyewe
 
Hii Movie ni kali sana, wacha tuchukue popcorn tusubiri, Hivi Ukawa mtajisikiaje mkigundua hata LOWASA alitumwa tu ni pandikizi??? Nakumbuka katuni ya kipanya. CCM wanakuwa na mikakati ya miaka 10 mpaka 20 ijayo ndo mana kinashidna miaka yote lol..
 
Hii Movie ni kali sana, wacha tuchukue popcorn tusubiri, Hivi Ukawa mtajisikiaje mkigundua hata LOWASA alitumwa tu ni pandikizi??? Nakumbuka katuni ya kipanya. CCM wanakuwa na mikakati ya miaka 10 mpaka 20 ijayo ndo mana kinashidna miaka yote lol..
Angekua pandilizi hao nusu kijiko wasinge haha kama nzi aliyesikia arufu ya kinyesi
 
Waliompokea alipohama niliwashangaa na bado ninawashangaa wanaompokea sasa anaporudi hasa kwa kauli hizi "kuwa ameamua kurudi katika chama cha Mapinduzi ili kunusuru biashara zake na rafiki zake.
Alipotoka CCM alihamia chama gani
 
Baadhi ya viongozi wa kisiasa waliopo na waliopita uwezo wao wa kutumia akili ya kuzaliwa ni mdogo sana.
Mfumo tu unawabeba na kupewa heshima wasizostahili. Hili pia lina uhusiano na umaskini wa nchi kwa ujumla!
 
Si nasikia amekanusha kuwa ile hotuba ya karatasi iliyotoka jana sio yake? Kwamba ilitengenezwa na wabaya wake? Yeye hakutoa hotuba ya karatasi, inasemekana kasema hivyo.
 
Sijasema pandikizi, nimeuliza tu mtajisikiaje??
Lowassa ni pandikizi lililo pandikizwa kitaalam alipandikizwa bila ya yeye kujijua kama ni pandikizi, sema Mbowe anaogopa kumtimua, Mbowe sijui ataweka wapi uso wake! Alivyo kutana na Maalim Seif alimwambia aachie Zanzibar wakina Kingunge na Suma wote ni ma mafia
 
Back
Top Bottom