Ni nani aliemuua huyu tajiri? Ni mchepuko wake, Mke wake au business partner wake?

ELI COHEN

JF-Expert Member
Joined
Jun 19, 2023
Posts
9,375
Reaction score
28,484
Tajiri Victor, alipatikana akiwa amekufa katika chumba chake cha kusomea, risasi moja ikapita moyoni mwake.

Kwanza, kulikuwa na elena, mke wa Victor wa miaka ishirini. Umaridadi wake ulifunika hasira kali ndani yake Alijua ufuska na usaliti wa Victor lakini aliishi hivyo hovyo akiwa ameunganishwa nae na ufalme ambao walikuwa wamejenga pamoja.
Ni mwanamke ambae kiasili ana kisilani sana ingawa ni mpambanaji sana kupelekea kuwa chachu ya mafanikio ya victor.

Usiku huo, kama isivyo kawaida, alionekana akitembea kwenye veranda iliopo karibu na ofisi ya victor, yeye anadai alikuwa pekee yake akitembea tembea akiwa na wakati wa kipweke wa kuwaza mambo mabovu ambayo victor anamfanyia.

Kisha kulikuwa na Aisha, mchepuko wa victor, alio uthamanisha sana kupelekea aisha kujiona maza house, ni binti mchanga mchanga, mrembo na wa kuvutia , ila pia na yeye ndani aliificha hasira kutokaana na ahadi za Victor za kumwacha Elena zilikuwa zimepunguza uvumilivu wa aisha ulikuwa umepungua lakini kikubwa zaidi inasemekana aisha aliziona meseji za victor aki order malaya kutoka telegram.

Kama isivyo kawaida, aisha alienda nyumbani kwa victor na mkewe bila ya kualikwa, mlinzi wa geti alimuita victor akutane na bibie huyo nje kwenye garden maana hakumruhusu aingie ndani , walionekana wakibishana sana hadi victor kumpiga makofi kumuambia aondoke hapo ila binti alilala chini bila kuondoka, hii ilikuwa ni saa chache kabla ya kifo chake cha victor.

Hatimaye, kulikuwa na Martha, mshirika wa biashara wa Victor. Akiwa mwenye hasira, yeye pia alienda nyumbani kwa victor bila kualikwa.

Uvumi ulienea kwamba Victor alipanga kumtenga kibishara baada ya miaka 15 ya kujenga wote himaya zao na mradi mpya wa victor haukumjumuisha. Ndani ya hii miaka 3 martha aliyumba sana kifedha baada ya biashara zake binafsi kufeli vibaya mno.

Martha alikuwa ndani ya nyumba hiyo usiku huo, aliingia ofisini mwa victor, ofisi ambayo alikuwa akiingia na victor kudiscuss mambo ya kazi. Usiku huo alipitia mikataba ile kwa hasira kali sana.

Askari mpelelezi, alichunguza eneo la tukio. Bunduki, iliyofutwa kabisa, ilikuwa imetupwa kwenye droo. Hakuna alama za vidole, hakuna mashahidi.

Camera za security zinaonesha hakuna mwingine alieingia nyumbani na kwa bahati mbaya eneo la veranda ya ofisi ya victor hakuna camera ila mlinzi anathibitisha wote walionekana maeneo ya ofisi ya victor.

Ni Huzuni ya Elena?
Wivu wa kimapenzi wa aisha?
Kupigwa kibuti kwa martha?

Mpelelezi akawakusanya chumbani. Macho ya kila mwanamke yalitazama kwa mwingine.
 
Huyo ni HELENA mkewe,kwa sababu tayari aisha alishazuiwa kuingia ndani ya nyumba halikadhalika martha ahusiki
 
Back
Top Bottom