Ni mungu pekee

Ni mungu pekee

Joined
Mar 25, 2013
Posts
10
Reaction score
2
(((( Ni MUNGU Pekee ))))

Kitu kimoja kuhusu Mwenyezi Mungu.

Mwenyezi Mungu hana upendeleo hata kidogo.. Unaweza kudhani kuna watu fulani anawapendelea
na kuwaonea baadhi. Lakini kamwe hayuko hivyo!

Fikiria Mchawi na Jambazi, kabla hajaenda kuwanga/kuiba anawaza na kumuomba Mungu ili kazi yake ifanyike salama na
anafanikiwa. Mungu hajalala ameona kila kitu... Wewe unalalamika kuibiwa mwenzio ameshapata mkate wa kila
siku...Ingawa hukumu yake Mungu anayomkononi.

Lakini umewahi kuwaza hili??
Una mgonjwa hospitali yuko
mahututi ni mtu wa muhimu sana maishani mwako. Ni mke/mme na unampenda kweli.. Au pengine ni Mlezi wako, Mama au Baba. Unamwomba Mungu na kusali sana kwamba apone na kurejea...

Wakati wewe unasali na kuomba
apone, Kuna mtu yuko huko mtaani ana wiki nzima hajauza Jeneza hata moja...Ana mke na watoto wa kulipa ada... Anafunga na kusali sana Mungu amuangazie baraka kwenye biashara yake...

Kipenzi chako,uliyemuombea sana Anafariki. Unakwenda kwa Muuza
Jeneza kununua ili umzike...Kwake yeye ni zaidi ya Biashara...Mungu amejibu Maombi yake...Amepata hela ya kula na kulipa Ada ya watoto..au hata kulipa kodi with
expense ya kifo cha mpenzi
uliyemuombea...

Huyo ndio Mungu sio tu Athumani wala sio Sadiki....

Muuza Jeneza anapiga sala ya Shukrani na anatoa sadaka kanisani kwa kujibiwa maombi yake kwa muda muafaka wakati wewe uko Msibani unalia kwa Majonzi..

Mwacheni Mungu aitwe Mungu..
 
Acha tu ndugu yangu mambo ya Mungu ni magumu sana ukiyatafakari, Hunyeshea mvua wema na wabaya, Kwa kweli acheni Mungu aitwe Mungu, ni yy pekee anastahili cheo hicho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom