Kang
JF-Expert Member
- Jun 24, 2008
- 5,692
- 2,576
Hili ni kumbusho kuwa karibia hifadhi zote za data zinaoza baada ya muda fulani, kitu ambacho ni muhimu kuzingatia.
HDD (Hard Disk Drive)
Zile mechanical ambayo haitumiki zinaoza baada ya miaka 2-20 kutegemea na ubora wa drive na hasa mazingira iliyohifadhiwa, mazingira ya TZ ya joto na humidity kubwa yanaathiri HD zaidi. Data humu zimehifadhiwa kwa usumaku na nguvu hii inapotea pia zina mechanical moving parts ambazo zanaharibika. Pia ni rahisi kuharibika kwa ujumla hasa ukiigonga.
SSD (Solid State Drive)
Kwa ujumla flash, NVMe na SSD ambazo hazitumiki data inaweza kupotea hata chini ya mwaka mmoja!
Na kwa kawaida mika 2 hadi 5 kama imehifadhiwa vizuri.
Hii ni kwa kuwa data humu zimehifadhiwa wa "charge" ya electrons na hii inapotea haraka zaidi kama battery vile.
CD/DVD/BRay
Za kurekodi mwenye CD-R etc, miaka 2-10 kutegemea na ubora wa CD na utunzaji hasa mazingira.
Hizi zinatumia dye/rangi ambayo inabadilishwa na laser wakati wa kuirekodi baada ya muda hizi dye zinaanza kupoteza rangi yake na kushindwa kusomeka hasa zinapopata joto au kupigwa na jua.
Kuna ambazo zinatumia dhahabu badala ya dye hizi zinaweza kukaa miaka 10-30.
CD/DVD ambazo zinatengenezwa kiwandani zinakaa muda zaidi mika 20-50 hizi zinatumia layer ya chuma kama aluminium kuhifadhi data, baadha ya muda unyevu unaingia ndani kwenye chuma na kusababisha oxidation (kutu) ya chuma cha kuhifadhi data.
M-DISK disk maalumu kwa uhifadhi wa data kwa muda mrefu miaka 20-100. Inatumia materia ya carbon kuhifadhi data ambayo haipati oxidation na haiharibiwi na mwanga kiurahisi.
Tape
Miaka 10-30.
Karatasi
Za kawaida mika 30-100 kutegemea na mazingira na muhimu pia imechapishwa vipi wino etc.
Archival paper, zinatengenezwa maalumu bila kutumia chemicali kama acid mika 500 na zaidi. Kuna makaratasi ya mika 2,000 iliyopita bado yanasomeka.