Ni Mimba ndio inamfanya awe hivi mpenzi wangu?

247

Senior Member
Mar 29, 2016
188
197
Habarini wana Jf

Wiki kama tatu zilizopita Mpenzi wangu amebadilika ghafla baada ya kushika ujauzito,
Nimejaribu kuvumilia hiyo hali sana kwasababu nimeshasikia kuwa wanawake wakiwa na Mimba huwa wanakuwa na mambo mengi mengi ya ajabu kama kumchukia mpenzi wake na mengineyo.

Ila leo ndio nimeshindwa kumuelewa kabisa baada ya kunitumia message na kunimbia kuwa anataka atoe mimba yangu tuachane.

Kabla ya kupata ujauzito alikua kawaida na mambo mengine yalikuwa yanaenda sawa, sasa ni kwamba hataki tena tuendelee kuwa na mahusiano au ni mimba ndio inamtuma hivyo?
 
Sasa na wewe ndo jifanye mwehu zaidi yake, mtumie pesa kisha mwambie nimekupa kwa ajili ya kutoa mimba, kisha uone jinsi atakavyo kufurumishia matusi utafikiri sio yeye alotaka kutoa mimba.
 
Sasa na wewe ndo jifanye mwehu zaidi yake, mtumie pesa kisha mwambie nimekupa kwa ajili ya kutoa mimba, kisha uone jinsi atakavyo kufurumishia matusi utafikiri sio yeye alotaka kutoa mimba.
Kuhusu kipato yupo vizuri, bila hata kumtumia hela anaweza akaitoa hata mwenyewe.
 
Kuhusu kipato yupo vizuri, bila hata kumtumia hela anaweza akaitoa hata mwenyewe.

Basi mwambie atoe haraka maana hata wewe hukua na mpango wa mtoto kwa sasa.
Kisha sikilizia jibu ulete mrejesho tujue pa kuanzia.
 
  • Thanks
Reactions: 247
Ana kuchekecha huyo...

Pia kipindi kuwa Muelewa na Mwenye Busara na Hekima.

Kumbuka Wanaume wenye Busara na Hekima ndio Wanaoweza ishi na Mke.
 
  • Thanks
Reactions: 247
Ana kuchekecha huyo...

Pia kipindi kuwa Muelewa na Mwenye Busara na Hekima.

Kumbuka Wanaume wenye Busara na Hekima ndio Wanaoweza ishi na Mke.
Nmejaribu kuwa muelewa mkuu ila kauli yake ina utata sana ndo maana nmekuja hapa kupata ushauri.
 
Mheshimiwa pole sana mkuu.
Hio n mimba tu inamchanganya na kama ni ya kwanza bas ishamtia hisia tofauti tofauti mwilini so we mvumilie mpe maneno matam atatulia tu.
 
Mheshimiwa pole sana mkuu.
Hio n mimba tu inamchanganya na kama ni ya kwanza bas ishamtia hisia tofauti tofauti mwilini so we mvumilie mpe maneno matam atatulia tu.
Shukrani Mkuu, ngoja nimvumilie tuu labda anaweza akatulia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom