Villky_J
JF-Expert Member
- Mar 14, 2017
- 492
- 609
Habari wanajamiiforum.
Leo tushirikiane katika hili. Kumekuwa na utata mkubwa sana kwa pande zote mbili husasani siku ya kwanza kukutana na mpenzi wako, ambae labda kwa muda mrefu mlikuwa mkiwasiliana bila kuonana ana kwa ana.
Wengi wetu huwa tunazidisha madoido mpaka tunaboa kiasi kwamba badala ya kupendeza ndio tunaharibu hususani kwa dada zetu. Unakuta mwanadada kajipodoa mpaka sura imebadilika inafanana na mwanasesere.
Upande wa wanaume mtu kajipigilia mpaka dada hata kuongozana nae anaona aibu. Sio macheni, makoti, mara makofia humohumo mpaka hajulikani kwamba anataka kuwa gentleman au bishoo yaani haeleweki.
Karibuni wadau tupeane uzoefu.