mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,588
- 11,668
Ni matusi mazito kwa intelijensia ya nchi kwamba kuna mteule wa Rais ambaye alighushi vyeti vya Elimu, kitendo ambacho ni kosa la jinai.
Tunatambua kuwa Viongozi ni kioo cha jamii. Wao ndio taswira ya jamii yetu, na ndio haswa wanapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa matendo yao katika maisha yao ya kila siku.
Kwa hivyo ingependeza viongozi wawe watu safi na makini, Ili watoto wetu wajifunze kwao. Lakini pia waweze kuwa na ushawishi kwa watu wa aina zote, wazee, vijana, watoto, wasomi, wajinga na wanafunzi. Ndio kusema kuwa, vyombo vya kiintelijensia (intelligence body) vina wajibu wa kumjua mtu kiunaga ubaga kabla ya kupata nafasi kubwa ya uongozi. Ile dhana ya kwamba Rais ni taasisi, isisahauliwe linapkokuja suala la Rais kuteua viongozi, ni lazima kuhusisha intelligence body/Body intelligence, katika kujua taarifa muhimu za hao wateule.
Sasa inapotokea Rais anateua cheti feki cha Elimu, wakati ni kosa la jinai ujue kwamba kuna shida katika 'body intelligence'; kwamba hiyo body ni 'incompetent' au imepuuzwa!!!, moja wapo ni sahihi.
Hata hivyo, kwa kutambua umasikini wa kimfumo katika shughuri za vyombo vyetu vya dola, ambavyo vimewezeshwa zaidi kudhibiti kuliko kuhudumia, tunaweza kuwasamehe. Lakini baada ya watu wengine kuibua kashfa za vyeti feki, halafu intelijensia zipo bize kukamata wabunge, that's shame and unforgivable.
Itoshe tu kusema kuwa kwa sakata hili la vyeti feki vya DAUDI, intelligence imetukanwa.