Mwalimu Nyerere aliwahi kusema kwa miaka 26 madarakani alifanya mambo mengi mazuri na mengine ya kijinga na akaendelea kusema "Shida ninayoiona wanaacha mazuri na kuendeleza ya kijinga" Nadhani ni kauli ya mtu aliyejaa busara na ni msingi kwa viongozi waliofuata kama Mungu akiwajalia busara.
Kama watanzania bila kujali itikadi zetu tunajua Kikwete kuna vitu alifanya vizuri na kuna alivyofanya vibaya. Ni mazuri yapi tunamshauri Magufuli ayaendeleze? Nimeamua kuleta uzi huu baada ya rais wetu kusema jana anapata muda kupitia maoni yetu mitandaoni.
Mnajua msimamo na itikadi yangu lakini thread hii ni kwa faida ya taifa letu pendwa la Tanzania. Ningeomba tumshauri rais kufuata na kuendeleza mambo mazuri ya JK bila kufuata misimamo yetu kisiasa. KARIBU!