Ni makosa kumualika Kaimu Jaji Mkuu kwenye matukio ambayo tunajua yataishia katika mahakama zake!

chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
5,678
2,000
Jaji Mkuu naona anaalikwa katika kila tukio tena mengine kitaratibu yana ishara zote za kuishia mahakamani ambako yeye ni kiongozi wa mahakama

Je atatenda haki? Kwa maoni yangu,Jaji Mkuu anapoonekana pale kwenye vikao vile vinavyorushwa laivu inamuweka katika upande mmoja dhidi ya wale wanaotuhumiwa!

Sijui na yeye huwa anapiga makofi au anashangilia pale anapoalikwa,au ana ushiriki kiasi gani,ila uwepo wa Kaimu Jaji Mkuu,Spika,na Rais,ni ishara au hisia kwamba ni uamuzi wa pamoja na hakuna pa kukimbilia,kwa kuwa hata mahakama ya kukimbilia,Tayari Jaji Mkuu alikuwa sehemu ya tukio!

Jaji Mkuu si mwanasiasa,mumuepushe na mgongano wa kimaslahi,hapo hajathibitishwa kazini
 
fattys

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
669
500
Mihimili yote Mikuu ya Dola ilikuwepo
(1) Serikali- Rais
(2) Bunge - Speaker
(3) Mahakama- Judge
 
chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
5,678
2,000
Mihimili yote Mikuu ya Dola ilikuwepo
(1) Serikali- Rais
(2) Bunge - Speaker
(3) Mahakama- Judge
Hapo ndipo panaleta tatizo,bora wangekuwa wanamwalika mtendaji mkuu wa mahakama pale wanapoandaa tukio la kutuhumu watu,kuna yale matukio ya kitaifa kama siku ya muungano,Uhuru,mapinduzi,ni matukio chanya,yasiyoegemea upande wowote,hayo yanamfaa Jaji Mkuu
 
Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,427
2,000
Yaani kwa wanasheria nguli kama LISSU hilo la Jaji kuwa meza moja na mshtaki ni ushindi tosha kwa mteja wake. Hiyo ni kupriemt matokeo ya hukumu. Ndiyo maana serikali hushindwa kesi mahakamani kwa kuingiza siasa kwenye weledi.
 
Watu watamtilia shaka kama tayari hana pre-conceived judgment,na kama huwa anapiga makofi na kufurahia watu wanamwekea video na kumkataa kwenye kesi zao
 
fattys

JF-Expert Member
Jan 1, 2014
669
500
Inategemea na maudhui ya Kikao yalikuwa ni nini? Kama lengo ni Utaifa yupo sahihi maana mihimili hii yote inafanya kazi kwa independently lakini kwa pamoja. Bunge linatunga sheria, Mahakama inatafsiri sheria jinsi zinavyosimamiwa na Serikali. Maudhui hapo ili kuwa siyo kwenda kumwatuhumu watu. Maudhui ilikuwa ni Mikataba mibovu iliyotungwa na Bunge kwa mujibu wa tafsiri ya Mahakama( wanasheria) na Kusimamiwa Vibaya na Serikali hivyo kuliletea hasara Taifa. Hivyo uwajibikaji wa pamoja kwa Wananchi
 
iparamasa

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
13,440
2,000
Good!

Mahakama lazima sio tu iwe huru,bali ionekane ikiwa huru,!

Wamuache jaji mkuu awe nyutro,wasimu-influence na kumjengea opinion mapema,

Anatakiwa awasikilize wote, wote ni wake,sasa kila Siku anakaa upande uleeeee!!! Kwenye vikao vya kuwananga waleeee!
 
chinembe

JF-Expert Member
May 16, 2015
5,678
2,000
Inategemea na maudhui ya Kikao yalikuwa ni nini? Kama lengo ni Utaifa yupo sahihi maana mihimili hii yote inafanya kazi kwa independently lakini kwa pamoja. Bunge linatunga sheria, Mahakama inatafsiri sheria jinsi zinavyosimamiwa na Serikali. Maudhui hapo ili kuwa siyo kwenda kumwatuhumu watu. Maudhui ilikuwa ni Mikataba mibovu iliyotungwa na Bunge kwa mujibu wa tafsiri ya Mahakama( wanasheria) na Kusimamiwa Vibaya na Serikali hivyo kuliletea hasara Taifa. Hivyo uwajibikaji wa pamoja kwa Wananchi
Hujaelewa nini?
 
cocochanel

JF-Expert Member
Oct 6, 2007
25,223
2,000
Duh kabisa umeandika hayo!!! Jisikitikie

Mnaboa hata sijui kwanini nimeandika humu ila naiposti tu,
 
Perfectz

JF-Expert Member
May 17, 2017
7,215
2,000
LABDA NI UTARATIBU TU WA KIUTAWALA MKUU,JAPO SIJAONA MANTIKI YA KUITWA KILA SEHEMU
 
Kihava

JF-Expert Member
May 23, 2016
4,427
2,000
Huyu Kaimu Jaji Mkuu aepuke vikao vinavyoagiza watu kushughulikiwa kisheria. Mbona wenzake tulikuwa hatuwaoni kwenye hivi vikao vya kisiasa? Halafu nasikia naye ni Professa Ibrahimu. Hawa maprofessa wamekuwa wa hovyo kuliko darasa la saba.
 
Kabisa,yaani maprofesa hawa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom