Ni ligi ipi inamvuto na ngumu kuliko zote ulaya

Willy T

JF-Expert Member
Mar 21, 2016
253
91
Habari muda huyu wanajamvi,
Naomba kujua ni nini mtazamo wako juu ya ligi za wenzetu maana umekuwa gumzo sana kwamba ligi nzuri na bora ni Fulani kisa wanafunga magoli mengine

Au nyingine kwasababu inashinda sana pia inatangazwa sana sasa
IPI ni nzuri inavutia ipi ni ngumu?
 
Kuna moja ni timu tatu tu zinagombania ubingwa,
Kuna nyingine, timu ni moja utmost mbili.,
Kuna nyingine, timu ni moja tu.
Kuna nyingine timu ni mbili tu.
Kuna nyingine timu zote zinagombania ubingwa.

Chagua mwenyewe ipi bora hapo
 
Nitajie ligi ambayo timu zote zinagombania ubingwa with evidence
 
Hebu tucheck hiz ligi za
Mbona EPL wakienda out wanafungwa sanaaaa
Hebu tucheck hizi ligi tano kubwa duniani,
Bundesliga, hii ligi ni timu mbili tu yaani Buyern Munich na Borrusia Dotmund timu nyingine zinapiganiana kutoshuka daraja. Haina mvuto sana.

Laliga, Hii ligi ina timu 3 ambazo zinaoneshana upinzani yaani Real Madrid, Barcelona na Atl Madrid, sio mzuri sana kuiona kwasababu timu inaweza kufungwa hadi goli 9-0 mfano msimu huu Madrid kuna waliibamiza kama goli 8-0. Nayo ni ligi ya timu mbili Barca na Madrid.

Epl, Hii ndio ligi yenye amsha amsha ya ukweli, hakuna timu ambayo ina uhakika kupata matokeo mbele ya timu nyingine. Kuna Timu kama Nane hivi zenye nguvu kimpira, Man u, Chelsea, Arsenal, Man city, Liverpool, Totenham, Everton na mbishi Leicester city. Ni ligi bora kuingalia

Ligue 1, Huku tayar bingwa kashapatikana huku zikiwa zimebaki game kama 9 hivi. Ligi hii haina upinzani.

Serie A, Huku nako hukueleweki, ligi haina mvuto kama zamani, ni mara chache sana watu kutazama hii ligi.
 
Etii kuna mtu anasema LA liga ni nzuri kisa wanafunga magoli mengi.......

Ila sawa uingereza ni ngumu vipii mbona UEFA hazifanyi vizuri au ndio huko kucheza michuano mingiiii
 
Mimi naamini kipindi cha hivi karibuni Ligi ya Uingereza timu zake hazijapata makocha wa maana, kocha kama Van Gaal, Arsenal na hata huyu Wa Man city Pellegrin ni makocha wanaoziangusha timu zao. Arsene Wenger tatizo lake kubwa ni Usajili, Pellegrin Hajui usajili, Vaan Gaal huyu sijui kwanini!!!!
Ila Wakirudi tena makocha kama Fegurson enzi hizi lazima timu za ligi nyingine zilie. Makocha tu ndio wanaoiangusha Epl.
 
Etii kuna mtu anasema LA liga ni nzuri kisa wanafunga magoli mengi.......

Ila sawa uingereza ni ngumu vipii mbona UEFA hazifanyi vizuri au ndio huko kucheza michuano mingiiii
Ligi kuu bongo, Geita na Polisi waliwapa watu dozi za kutosha mechi za mwisho kuingia VPL.
Hii ndo ligi bora, magoli kwenda mbele. Mtu anakula sita, saba!
 
Mbona EPL wakienda out wanafungwa sanaaaa
Mleta mada kauliza ligi ngumu sio ligi bora
League ya EPL ndio League ngumu na yenye msisimko

Inapokuja kweny ubora FA ya England wana invest kweny finance kuliko ubora wa league
Mgao inayopata timu inayoshika nafasi ya tano ya La liga haufikii hata nusu ya mgao inayopata timu inayoshika mkia EPL
 
Hebu tucheck hiz ligi za

Hebu tucheck hizi ligi tano kubwa duniani,
Bundesliga, hii ligi ni timu mbili tu yaani Buyern Munich na Borrusia Dotmund timu nyingine zinapiganiana kutoshuka daraja. Haina mvuto sana.

Laliga, Hii ligi ina timu 3 ambazo zinaoneshana upinzani yaani Real Madrid, Barcelona na Atl Madrid, sio mzuri sana kuiona kwasababu timu inaweza kufungwa hadi goli 9-0 mfano msimu huu Madrid kuna waliibamiza kama goli 8-0. Nayo ni ligi ya timu mbili Barca na Madrid.

Epl, Hii ndio ligi yenye amsha amsha ya ukweli, hakuna timu ambayo ina uhakika kupata matokeo mbele ya timu nyingine. Kuna Timu kama Nane hivi zenye nguvu kimpira, Man u, Chelsea, Arsenal, Man city, Liverpool, Totenham, Everton na mbishi Leicester city. Ni ligi bora kuingalia

Ligue 1, Huku tayar bingwa kashapatikana huku zikiwa zimebaki game kama 9 hivi. Ligi hii haina upinzani.

Serie A, Huku nako hukueleweki, ligi haina mvuto kama zamani, ni mara chache sana watu kutazama hii ligi

:DHapo kwenye Red naona unamchokoza Gang chomba
 
Back
Top Bottom