Ni kweli serikali inapuuza madai ya walimu?

mwalimumwema

Member
Joined
Dec 7, 2012
Posts
16
Reaction score
1
Katika kongamano la kuadhimisha miaka 51 ya uhuru wa Tanzania bara swala la walimu na elimu limegusiwa sana na wachokoza mada na wachangiaji waliowengi. Lakini jambo lililonishangaza ni tuhuma kwamba eti 'serikali ya Tanzania inapuuzia madai ya walimu' naamini tunao walimu hapa, je ni kweli madai ya walimu yanapuuzwa na serikali yao tukufu? Pia naamini wawakilishi ama SERIKALI yenyewe inapitapita maeneo haya, Je ni kweli katika uongozi wao wanapuuza madai ya walimu?
KWA HALI HIYO BASI WALIMU WAFANYEJE SASA IWAPO MADAI YAO YA MSINGI YANAPUUZWA NA SERIKALI.
 
Mimi kama mwalimu serikali yangu imeniaminisha kuwa inapuuza madai ya waalimu mana kama isingalikuwa hivyo basi wangeyalipa kwa wakati husika.
 
CWT iendelee kuwasemea walimu zaidi. Lakini kubwa nililonote kutoka kwenye kongamano la UDSM ni kwamba, kwanini waliofeli ndo wanakuwa walimu?
 
Ni kweli serikali inapuuza madai ya walimu hilo halikwepeki, rejea kauli ya rais baada ya mgomo wa walimu "madai ya walimu hayalipiki". Kwa nini madai ya walimu hayalipiki wkt ya watumishi wa kada nyingine yanalipika. Kitu kinachotakiwa kufanyika ni walimu kuuza bidhaa "elimu" kulingana na uwezo wa wanunuzi wao.
 
Tatizo sio Serikali, Ishu iko kwa Chama cha walimu na walimu wenyewe, Walimu wenyewe ikiitishwa mgomo utawakuta wengine wako Madarasani wanapiga chaki kama kawaida, sasa hapo unategemea nini?

Vyama vya wafanyakazi Tanzania ni vya kisanii, Kuanzia TUCTA na wanachama wake, Katika nchi yeyete ile dunini vyama vya wafanya kazi vinaheshimiwa sana make vinao uwezo wa hata kufanya Mapinduzi ya kuondoa UTAWALA madarakani.Cheki mfano wa South Africa au Kenya vyma viko Strong sana,

Bongo eti wanagoma huku wakisema tunawahurumia wanafunzi wasio kuwa na hatia huu ni ujinga, CWT ni wasanii tupu na walimu ni waoga kuliko,

So Serikali isalaumiwe bali walimu na chama chao pamoja na TUCTA ndo walaumiwe
 
kwahyo ww hauoni serikali ina tatzo bali CWT?hivi CWT ndo inawaajiri waalimu mpaka ilaumiwe? poor ward school product
 
Walimu tulishapuuzwa siku nyingi,tunaonekana wapuuzi ktkk nchi hii,Anglia juzikati serikali imeongeza mishahara kwa vigogo lakini walimu hata mia hakuna pamoja na kwamba ndo wanasoliwa kiduchu kuliko kada nyingine.
 
Nimeshasema humu jamvini kwamba kulalamika hakutasaidia kitu.Unatakiwa utambue kwamba ualimu is a low paying job! Lakini ukiwa mwalimu you have a lot of ample time to do your own business.Ukishalielewa hilo hautasumbuka na serikali pamoja na jamii isiyojali na kuheshimu walimu. Ieleweke kuwa ualimu ni profession kama nyingine e.g uanasheria,udaktari etc kwa hiyo mi nachofanya ni kuwa baada ya darasani kinachofuata ni business,e.g any consultation lazma ilipiwe zaidi ya hapo kazi haifanyiki.Kunifuata nyumbani au muda tofauti na wa darasani lazma uje na consultation fee vinginevyo niache nihudumie wengine wanakuja kwa ajili ya kupata elimu ya ziada kwa malipo.Hapo ndo heshima ya kazi ya ualimu utaiona kwa sababu wanafunzi wa wazazi huwa wanajua kumwona mwalimu anayejiita mheshimiwa lazma ujipange.Hivyo ndo namna mambo yanavyotakiwa kwenda,mi nawashauri walimu mnaopitia hapa jamvini kuwa you have to value yourself vinginevyo utaendelea kuwa ngazi ya wengine tu ya kupandia.Ukiwa na msimamo hela wanazileta wenyewe na vigogo wanakuwa wanakuita uwafundishie watoto wao nyumbani kwa mambo yaleyale wanayoyasema hayaruhusiwi yaani tuition.Mi nawakumbusha ndg zangu kuwa bill gates aliwahi kusema kuwa UKIZALIWA MASKINI SIO KOSA LAKO,LAKINI UKIFA MASKINI NI KOSA LAKO.Kwa hiyo una wajibu kuhakikisha maisha unayaweka sawa
 
Mimi ni tcha. Kweli cjui pakuanzia maana matcha wenzangu ni majinga, CWT naTUCTA ni wahuni na SIRIKALI ni dhalimu.
 
kwahyo ww hauoni serikali ina tatzo bali CWT?hivi CWT ndo inawaajiri waalimu mpaka ilaumiwe? poor ward school product

Wewe ndo Umesoma Shule za Kata na kukarii mapaphulet ya Nyangwine, Udhaifu wa CWT na TUCTA ndo unasababisha Serikali iwe hivyo, kungekuwa na Strong CWT na TUCTA kusingekuwa na aina ya kupuuzwa, tembelea KENYA oune chama chao cha walimu kilivyo strong, wakitangaza Mgomo ni Mgomo hakuna cha Amri ya Mahakama, sasa hapa Mukoba anazuga kuitisha mgomo ili aonekane anafanya kazi kumbe ni usanii walio panga na Serikali,

Na walimu nao ndo wanasababisha Serikali iwapuze, Huwezi itisha Mugomo then wengine wanaingia Darasani kufundisha, Migomo ya Kenya huwa ni walimu wote Nchi nzima wanagoma lakini Tanzania Nusu hugoma na Nusu huendelea na kazi, huu ni ujinga,

So jifunze usipendele kukariri mambo, Tafuta chanzo cha Serikali kupuuza Walimu ni nini?
 
Mimi ni tcha. Kweli cjui pakuanzia maana matcha wenzangu ni majinga, CWT naTUCTA ni wahuni na SIRIKALI ni dhalimu.

Ni kweli mkuu walimu ni Mazuzu hakuna mfano, wanabakia kulalamika wakiwa Ofisini lakini ikija kwenye Vitendo hakuna kitu, na CWT ishajua walimu nu Mazuzu na wao imebidi wafanye Usanii, kile chama hakiwezi wasaidia walimu hata siku moja,
 
Tatizo sio Serikali, Ishu iko kwa Chama cha walimu na walimu wenyewe, Walimu wenyewe ikiitishwa mgomo utawakuta wengine wako Madarasani wanapiga chaki kama kawaida, sasa hapo unategemea nini?

Vyama vya wafanyakazi Tanzania ni vya kisanii, Kuanzia TUCTA na wanachama wake, Katika nchi yeyete ile dunini vyama vya wafanya kazi vinaheshimiwa sana make vinao uwezo wa hata kufanya Mapinduzi ya kuondoa UTAWALA madarakani.Cheki mfano wa South Africa au Kenya vyma viko Strong sana,

Bongo eti wanagoma huku wakisema tunawahurumia wanafunzi wasio kuwa na hatia huu ni ujinga, CWT ni wasanii tupu na walimu ni waoga kuliko,

So Serikali isalaumiwe bali walimu na chama chao pamoja na TUCTA ndo walaumiwe

Unatakiwa ufanye utafiti wa kutosha kabla ya kusema haya! Ni kweli matatizo ya walimu yamesababishwa na CWT na TUCTA?
 
Hawa si ndo watetezi wao? Mkuu kikiwa na Trade Union Legelege matatizo hayawezi kuisha, lakini kama CWT na TUKTA wangekuwa strong kabisa walimu wasingekuwa wanalia kama hivi, Mbona Kenya huwa kinaeleweka? TRADE UNION ZA south africa au Kenya zinaogopwa kuliko hata vyama vya Upinzani,

imagine inaitishwa mugomo usio kuwa na kikomo then baada ya siku mbili unasikia tumesitisha mugomo kwa kuwahurumia wanafunzi, huu nu usanii wa hali ya juu,

KWA KIFUPI TANZANIA HAKUNA TRADE UNION KUNA USANII TU WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NA WANACHO JALI NI MATUMBO YAO NA WANATUMIKIA SERIKALI
 
Katika kongamano la kuadhimisha miaka 51 ya uhuru wa Tanzania bara swala la walimu na elimu limegusiwa sana na wachokoza mada na wachangiaji waliowengi. Lakini jambo lililonishangaza ni tuhuma kwamba eti 'serikali ya Tanzania inapuuzia madai ya walimu' naamini tunao walimu hapa, je ni kweli madai ya walimu yanapuuzwa na serikali yao tukufu? Pia naamini wawakilishi ama SERIKALI yenyewe inapitapita maeneo haya, Je ni kweli katika uongozi wao wanapuuza madai ya walimu?
KWA HALI HIYO BASI WALIMU WAFANYEJE SASA IWAPO MADAI YAO YA MSINGI YANAPUUZWA NA SERIKALI.

mwalimumwema wewe unaonaje?inawajali inawapuuza?
 
Last edited by a moderator:
Nimeshasema humu jamvini kwamba kulalamika hakutasaidia kitu.Unatakiwa utambue kwamba ualimu is a low paying job! Lakini ukiwa mwalimu you have a lot of ample time to do your own business.Ukishalielewa hilo hautasumbuka na serikali pamoja na jamii isiyojali na kuheshimu walimu. Ieleweke kuwa ualimu ni profession kama nyingine e.g uanasheria,udaktari etc kwa hiyo mi nachofanya ni kuwa baada ya darasani kinachofuata ni business,e.g any consultation lazma ilipiwe zaidi ya hapo kazi haifanyiki.Kunifuata nyumbani au muda tofauti na wa darasani lazma uje na consultation fee vinginevyo niache nihudumie wengine wanakuja kwa ajili ya kupata elimu ya ziada kwa malipo.Hapo ndo heshima ya kazi ya ualimu utaiona kwa sababu wanafunzi wa wazazi huwa wanajua kumwona mwalimu anayejiita mheshimiwa lazma ujipange.Hivyo ndo namna mambo yanavyotakiwa kwenda,mi nawashauri walimu mnaopitia hapa jamvini kuwa you have to value yourself vinginevyo utaendelea kuwa ngazi ya wengine tu ya kupandia.Ukiwa na msimamo hela wanazileta wenyewe na vigogo wanakuwa wanakuita uwafundishie watoto wao nyumbani kwa mambo yaleyale wanayoyasema hayaruhusiwi yaani tuition.Mi nawakumbusha ndg zangu kuwa bill gates aliwahi kusema kuwa UKIZALIWA MASKINI SIO KOSA LAKO,LAKINI UKIFA MASKINI NI KOSA LAKO.Kwa hiyo una wajibu kuhakikisha maisha unayaweka sawa
vijana wooote tunapaswa kulibeba hili
 
unataka kutuaminisha kisa cha waalimu kuthaminiwa enzi za serikali ya Nyerere ni kwa sababu ya CWT pia?kajifunze mkuu.
 
Kama kweli tunawapenda watoto ni bora kugoma kweli, ili maboresho yafanyike.
kuliko kuwa vuguvugu tunaangamiza masikini.
 
Asanteni wana jamvi kwahiyo kulingana na michango yenu tatizo si serikali as such bali UDHAIFU wa CWT pamoja na WALIMU wenyewe inapelekea SERIKALI KUPUUZA MADAI YA WALIMU.
  • Kwanini CWT inakuwa dhaifu hadi kushindwa kusimamia maslahi ya WALIMU?
  • Kwanini WALIMU wanakuwa dhaifu/waoga hadi kushindwa kuiwajibisha CWT pamoja na SERIKALI?
  • Matokeo ya mvutano huu wa chini chini kati ya CWT na WALIMU pamoja na SERIKALI nini hatma ya ELIMU ya nchi hii? ( Elimu dhaifu kwa wanafunzi--- matokeo mabaya ya mitihani--wahitimu hawaajiriki (kutokana na poor qualifications)--wanaojiriwa hawawezi kutimiza majukumu yao (kutokana na less qualifications)--Taifa DHAIFU.
  • Nini nafasi ya mtanzania wa kawaida kwenye swala hili la kupuuzwa kwa madai ya walimu
  • Nini kifanyike
 
Hawa si ndo watetezi wao? Mkuu kikiwa na Trade Union Legelege matatizo hayawezi kuisha, lakini kama CWT na TUKTA wangekuwa strong kabisa walimu wasingekuwa wanalia kama hivi, Mbona Kenya huwa kinaeleweka? TRADE UNION ZA south africa au Kenya zinaogopwa kuliko hata vyama vya Upinzani,

imagine inaitishwa mugomo usio kuwa na kikomo then baada ya siku mbili unasikia tumesitisha mugomo kwa kuwahurumia wanafunzi, huu nu usanii wa hali ya juu,

KWA KIFUPI TANZANIA HAKUNA TRADE UNION KUNA USANII TU WA VYAMA VYA WAFANYAKAZI NA WANACHO JALI NI MATUMBO YAO NA WANATUMIKIA SERIKALI

Kumbe nyie hamjui; hao viongozi wanaogopa MABWEPANDE ndo maana wako weak namna hiyo.
 
Back
Top Bottom