Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 48,684
- 149,887
Hivi hii serikali kweli imeshindwa kubuni sera na kuweka mikakati ya kukusanya kodi kutoka kwa watu wanaofanya biashara ya nyumba na majumba ya kupangisha?
Watu tumeshatoa mawazo yetu humu mara kadhaa ni namna gani TRA inaweza kukusanya kodi katika eneo hili kwa kuzishirikisha serikali za mitaa. Kinachokisekana hapa ni dhamira kwani huenda viongozi wa serikali na hata wabunge wanaoishauri serikali ndio wamiliki wakubwa wa majengo /nyumna hizi za kupangisha hivyo wanahofu kodi ya aina hii itagusa maslahi yao.
TRA,badala ya kunyang"anyana na Halmashauri kodi ya property tax, nawashauri kwa kushirikiana na serikali mfikirie kuwa na kodi ya aina hii ambayo naamini mnaweza mkatengeneza hela nyingi tu pengine kuzidi hatab hayo mapato yanayotokana na kodi za majengo.
Kuna frame za biashara, apartmens, hostel za wanafunzi mitaani,nyumba za kupangisha,vyumba vya kupangisha,n.k. Hata vyuo navyo ikiwezekana vitozwe kodi kwani mbali na kutoza wanafunzi ada,bado vinafanya biashara ya kupangisha wanafunzi katika hostel za vyuo na kuna baadhi ya vyuo vinatoza wanafunzi gharama kubwa ya vyumba kuliko hata kodi za vyumba vya mitaani.
Hivi kweli ni haki na ni sahihi kwa serikali kumtoza kodi kila mwezi mfanyakazi mwenye mshahara wa shilingi 360/= huku mfanyabiasha au kigogo wa serikali anaemiliki majumba /apartments /frame akiishi kulipa property tax tu ambayo kama sikosei hulipwa mara moja tu kwa mwaka?
Serikali ije na sera na sheria ya kutambua rasimi biashara hii na ikibidi iweke udhibiti wa hii biashara kama inavyofanya katika sekta nyingine kama vile kwenye nishati,n.k.