Ni kweli hakuna kizuizi?

Ni kweli hakuna kizuizi?

dawambili

Member
Joined
Nov 28, 2024
Posts
28
Reaction score
19
Hili ni Shairi la Mshairi Bora Wa Taifa Mwaka 2025 na mshindi wa Kwanza Wa Tuzo Ya Taifa Ya Uandishi Bunifu Bwana Daruweshi Mkulu Wanyika anasema hajaona kizuizi kushiriki uchaguzi .
Je ni kweli hakuna kizuizi?

SIJAONA KIZUIZI

N'nazitambua haki, na mazuri maamuzi
Kuchaguliwa sitaki, waso bora viongozi
Nanena n'tashiriki, pasipo kigugumizi
Sijaona kiziuzi, nashiriki uchaguzi

Nakataa ushabiki, wa mbwa kwenye miluzi
Kwasasa sidanganyiki, na sera za ubaguzi
Ugomvi wanipa dhiki, ya shari siyatukuzi
Sijaona kiziuzi, nashiriki uchaguzi

Urongo sitosadiki, piya hawaniburuzi
Yote ya wasaka kiki, nakataa mchambuzi
Kwani hayakubaliki, na wasaka mageuzi
Sijaona kiziuzi, nashiriki uchaguzi

Nitenda ipiga tiki, simngoji bilikizi
Nyuma tena sitobaki, kwa uyinga na ajizi
Ili hizo mamlaki, iwe nami mteuzi
Sijaona kiziuzi, nashiriki uchaguzi

Pasipo sheria feki, uzalendo ja mavazi
Ashindwae haridhiki, thama akiwa bazazi
Fitina atadiriki, keki aite andazi
Sijaona kiziuzi, nashiriki uchaguzi

DARUWESHI MKULU WANYIKA
MWENESESEME NOGAYA WA SABA (VII)
MAGOMENI MWEMBECHAI, DAR ES SALAAM
 
Hili ni Shairi la Mshairi Bora Wa Taifa Mwaka 2025 na mshindi wa Kwanza Wa Tuzo Ya Taifa Ya Uandishi Bunifu Bwana Daruweshi Mkulu Wanyika anasema hajaona kizuizi kushiriki uchaguzi .
Je ni kweli hakuna kizuizi?

SIJAONA KIZUIZI

N'nazitambua haki, na mazuri maamuzi
Kuchaguliwa sitaki, waso bora viongozi
Nanena n'tashiriki, pasipo kigugumizi
Sijaona kiziuzi, nashiriki uchaguzi

Nakataa ushabiki, wa mbwa kwenye miluzi
Kwasasa sidanganyiki, na sera za ubaguzi
Ugomvi wanipa dhiki, ya shari siyatukuzi
Sijaona kiziuzi, nashiriki uchaguzi

Urongo sitosadiki, piya hawaniburuzi
Yote ya wasaka kiki, nakataa mchambuzi
Kwani hayakubaliki, na wasaka mageuzi
Sijaona kiziuzi, nashiriki uchaguzi

Nitenda ipiga tiki, simngoji bilikizi
Nyuma tena sitobaki, kwa uyinga na ajizi
Ili hizo mamlaki, iwe nami mteuzi
Sijaona kiziuzi, nashiriki uchaguzi

Pasipo sheria feki, uzalendo ja mavazi
Ashindwae haridhiki, thama akiwa bazazi
Fitina atadiriki, keki aite andazi
Sijaona kiziuzi, nashiriki uchaguzi

DARUWESHI MKULU WANYIKA
MWENESESEME NOGAYA WA SABA (VII)
MAGOMENI MWEMBECHAI, DAR ES SALAAM
Wakati wa uchaguzi wa wenyeviti wa Serikali za mitaa akitunga shairi hili lifuatalo na Sasa anasema hajaona kizuizi.

HODARI KAENGULIWA

Nalipanga kudamka,siku itapowadia
Foleni kuziepuka,kwani huleta udhia
Kura npige haraka,bila kuzua ghasia
Hodari kaenguliwa,kura yangu ni hapana

Hamasa imetoweka,amekatwa mgombea
Ambaye nlikitaka, kura yangu kumgea
Hamu imenchujuka,mwanzo ilo nkolea
Hodari kaenguliwa,kura yangu ni hapana

Kituoni nitafika,haki yangu kutumia
Hapana ntaandika,kwa uchungu na hisia
Kwani nnayo hakika,hafai alobakia
Hodari kaenguliwa,kura yangu ni hapana

Yazamani nakumbuka,vile tulivyozoea
Wengi wasoelimika,fomu hawakukosea
Sasa imezoeleka,kuwa ni patapotea
Hodari kaenguliwa,kura yangu ni hapana

Mzalendo sitochoka,bado nimeazimia
Kuepuka kudhurika,kura sitozisusia
Ndio njia isoshaka,ya kukomboa jamia
Hodari kaenguliwa,kura yangu ni hapana

DARUWESHI MKULU WANYIKA
MWENE SESEME NOGAYA WA SABA (Vll)
MAGOMENI MWEMBECHAI DAARUSSALAAM
0689969098
 
Back
Top Bottom