Ni kwanini watu huonekana wabaya pale wanaposhidwa kusaidia hata kama walikuwa wanasaidia?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,682
jamani wana jf nilikutana rafiki yangu mmoja alikuwa ananieleza yeye kwa miaka mingi kuna ndugu yake huyo kila akimuomba hela yeye huwa anajitahidi kumtumia hivo hivo.

sasa jamaa amefikia hatua kama vile kachoka siku hizi akiombwa hela yeye humjibu sasa hivi ana hali ngumu hana pesaa.

lakini tangu amjibu hana pesa yule ndugu yake anamuona ameshakuwa mtu mbaya wakionana anakuwa amekasirika haonyeshi ile furaha yake ya zamaniii,

sasa hapa ndipo nikaulizaa ivi ni kwanini mtu akuone una roho mbaya pale unaposhidwa kumtimizia mahitaji yake wakati kipindi cha nyuma ulijitahidi kumsaidiaa
 
Ulimsaidia kitu.ulipaswa kumsaidia mawazo jinsi ulivyo pata.
Kosa lilikuwa hapa, ungemfundisha kuvua samaki na ukampa nyavu, ungekuwa umemaliza tatizo, sasa wewe ulijifanya father xmass. Kaka usipate shida, hilo tatizo linatukumba wengi sana, wengine hatusemi. Mswahili akiona nduguye kimeeleweka yy anaacha kufanya kazi.

Kaza buti, na hata hali yako ikirudi kwenye ubora wako, usirudie kosa. Mungu akinijalia, sadaka huwa natoa kwenye elimu, ugonjwa, msiba basi. maeneo mengine nimeomba wanisamehe.
 
Kwenye hii picha chini, mtu akiulizwa anaona nini;
bila shaka majibu mengi yatakuwa ni; naona kidoti cheusi
watu wachache mno watazungumzia rangi nyeupe inayokizunguka kidoti cheusi.

hivyo ndivyo binadamu wengi tunavyotazama maisha ya wenzetu, huwa tunaangalia kasoro zaidi kuliko mazuri waliyofanya.
kidot.png
 
Kosa lilikuwa hapa, ungemfundisha kuvua samaki na ukampa nyavu, ungekuwa umemaliza tatizo, sasa wewe ulijifanya father xmass. Kaka usipate shida, hilo tatizo linatukumba wengi sana, wengine hatusemi. Mswahili akiona nduguye kimeeleweka yy anaacha kufanya kazi.

Kaza buti, na hata hali yako ikirudi kwenye ubora wako, usirudie kosa. Mungu akinijalia, sadaka huwa natoa kwenye elimu, ugonjwa, msiba basi. maeneo mengine nimeomba wanisamehe.
mkuu hapa umeleweka ila ni kweli wengi yanatukumbaa sana
 
Back
Top Bottom