Ni kwanini katika maisha ya siku hizi kumekuwa na hali ya ndugu kwa ndugu kutoelewana?

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,683
Wakati tunakuwa tukiwa watoto kulikuwepo na yale maisha ya ndugu kupendana na kuelewana lakini pia kutembeleana ndugu kwa ndugu.

Miaka ya enzi hizo kulikuwa na ile hali ya watoto wa mjomba au watoto wa baba mdogo au baba mkubwa kutembeleana lakini kulikuwa na hali ya ndugu pia wa tumbo moja kuelewanaa.

Lakini katika uchunguzi nilioufanya tangu mwaka 2016 kumekuwepo na hali ya ndugu wa either familia moja au ukoo mmoja kutokuwa na maelewano hadi kuchukukiana. lakini pia kusemana vibayaa.

Sasa swali langu kuna tatizo gani linalosababisha ndugu kwa ndugu kutokuelewana, kuchukukiana tofauti na enzi zile za miaka ya 80 na 90 watu waliishi kwa amani na upendo
 
Zamani wanawake wengi walikuwa under control ya wanaume
na wanaume hawana kuewekeana vinyongo na kununiana

Siku hizi wanawake wameenda shule na wana kazi nzuri na wengine ni single moms
so wana uamuzi....na hatuishi kimila.....huwafanyi kitu

Anaweza kuwapiga marufuku watoto kwenda kwa baba mkubwa au kwa mama mdogo
just like that undugu ukaanza kufa
 
Mambo ya kuoa kwa kuangalia mapenzi badala ya mikakati ndio shida yake, Wahindi unaweza kuta vizazi viwili wanaishi pamoja, Dhubutu sisi useme wewe na kaka yako muishi pamoja au mradi mmoja, wake zenu wanatoana macho
 
hahaaaa ebana eheee
 
Zamani wanawake wengi walikuwa under control ya wanaume
na wanaume hawana kuewekeana vinyongo na kununiana

Siku hizi wanawake wameenda shule na wana kazi nzuri na wengine ni single moms
so wana uamuzi....na hatuishi kimila.....huwafanyi kitu

Anaweza kuwapiga marufuku watoto kwenda kwa baba mkubwa au kwa mama mdogo
just like that undugu ukaanza kufa
undugu ukishaanza kufa na hapo unakuta wengi sasa wanashidwa hata kusalimiana njiani
 
wakati tunakuwa enzi tukiwa watoto kulikuwepo na yale maisha ya ndugu kupendana na kuelewana lakini pia kutembeleana ndugu kwa ndugu.

miaka ya enzi hizo kulikuwa na ile hali ya watoto wa mjomba au watoto wa bamdogo au bamkubwa kutembeleana lakini kulikuwa na ile hali ya ndugu pia wa tumbo moja kuelewanaa.

lakini katika nilioufanya tangu mwaka 2016 kumekuwepo na hali ya ndugu wa either familia moja, ukoo mmoja kutokuwa na maelewano hadi kuchukukiana.
lakini pia kusemana vibayaa.

sasa swali langu kuna tatizo gani linalosababisha ndugu kwa ndugu kutokuelewana kuchukukiana tofauti na enzi zile za miaka ya 80 na 90 watu waliishi kwa amani na upendo
Mkuu observation yako ni sahihi kabisa.

Sababu ya msingi ni kuongezeka kwa uovu na watu kumwacha Mungu kwa kuwa Shetani ameongeza his assault on humanity.Anajua sasa kwamba siku zake zimekwisha and he is soon facing the eternal hell of fire,so he is trying by hooks and crooks to get partners.

Katika kitabu cha 2Timotheo 3:1-4 tunasoma maneno haya "1 Lakini ufahamu neno hili, ya kuwa siku za mwisho kutakuwa na nyakati za hatari,2 maana watu watakuwa wenye kujipenda wenyewe,wenye kupenda fedha,wenye kujisifu,wenye kiburi,wenye kutukana,wasiowatii wazazi wao,wasio na shukrani,wasio safi,3 wasiowapenda wa kwao,wasiotaka kufanya suluhu,wasingiziaji,wasiojizuia,wakali,wasiopenda mema,4 wasaliti,wakaidi,wenye kujivuna,wapendao anasa kuliko kumpenda Mungu." Frankly uovu wote uliotajwa katika mistari hiyo umetimia katika kizazi cha sasa na haiwezekani mtu mwovu kiasi hicho awe na uhusiano mzuri na ndugu zake.Hata hivyo katika mstari wa tatu kuna sehemu ya msingi ambayo ina address your query directly,"wasiowapenda wa kwao."Biblia iliona ukweli huo zaidi ya miaka 1500 iliyopita!How incredible. No wonder it is happening now.
 
tumeacha tamaduni zetu sasa hivi kila mtu anafikiri familia yake ni mke wake na watoto wake mbaya zaidi wengi wanaofanya hivyo ndio walisomeshwa ama na baba zao wadogo au wakubwa, shangazi zao au wajomba zao, mama zao wadogo au wakubwa, dada zao au kaka zao lakini baada ya kupata hiyo elimu wanasahau kule walikotoka.
Pia wengi wamekuwa wanathamini pesa zaidi kwao ndugu wa maana ni yule mwenye pesa nyingi asiye na chochote wanamuona hana maana
 
rodrick nakubaliana na wewe lakini pia usisahau pia kuna kasumba imejengeka miongoni mwa ndugu kama ukienda kumsalimia au kumtembelea unaonekana unaenda kutangaza shidaa hivi hili nalo unalizungumziajeeee
 
Unasema njiani?
kuna ndugu wanakutana nje ya nchi na wanakaushiana
au wanapanda ndege moja na wamekaushiana
hii ni hatua moja mbayaa sana katika maisha ivi hii hali ya ndugu kutokusalimia au kuongea kwa muda mrefu ivi ikitokea tatizo inakuwajeeee
 
Ndugu kuchukiana imeanza enzi za Abel na Kaini.
Sababu ni nyingi ikiwemo maleZi.
Watoto wanakuzwa kibaguzi na wanakuwahivyo mpaka the next next generation.
Ubusy wa maisha kutoka Na Hali ya uchumi
Kukua kwa teknolojia watu wanaonawakishakuwa na Whatsap group la familia inatosha ,mwisho wa siku wanatengana na kufarakana kabisa.
 
mleta mada siyo pia Tanzania tu had ulaya . David Miliband na Ed Miliband ni ndugu wa damu kabisa katika Chama cha labor uingereza lakini hawasalimiani walk kuongea kwasabab Ed alimpindua kaka yake David kuwa mgonbea wa labor tangu siku Iyo awapatani kabisa.
 
Masamaki bosi wa TRA aliyetumbuliwa mwanzonimwanzoni ana nyumba za kisasa Zaid ya sabin. Lakin mdogo wake wa dam anauza samaki Tandale na kuish kwenye chumba cha kupanga.
hapo ndipo tunaposema kizuli kula nduguyoo ila hii ngumu mtu kuamini
 
Ndugu kuchukiana imeanza enzi za Abel na Kaini.
Sababu ni nyingi ikiwemo maleZi.
Watoto wanakuzwa kibaguzi na wanakuwahivyo mpaka the next next generation.
Ubusy wa maisha kutoka Na Hali ya uchumi
Kukua kwa teknolojia watu wanaonawakishakuwa na Whatsap group la familia inatosha ,mwisho wa siku wanatengana na kufarakana kabisa.
mkuu nadhani hii inatokana na ile roho ya kisasii sasa huu mtindo wa ndugu kwa ndugu kubaguana na wote ni ukoo wa baba na mama mmojaa
 
rodrick nakubaliana na wewe lakini pia usisahau pia kuna kasumba imejengeka miongoni mwa ndugu kama ukienda kumsalimia au kumtembelea unaonekana unaenda kutangaza shidaa hivi hili nalo unalizungumziajeeee
kipimo chetu cha ndugu tumeweka kwenye pesa, kuna kipindi nilikuwa naishi kijitonyama ila nilikuwa napandia bus mwananyamala ilikuwa jumapili nikakutana na mzee mmoja anaulizia njia ya kutokea mwananyamala nikamwonyesha wakati tunaenda akanisimulia kuwa ametoka kanisani akaona bora apitie kwa ndugu yake amsalimie maana hawajaonana muda mrefu, lakini alipofika body language aliyoiona pale ilimkatisha tamaa kwa hakukuwa na hali inayoonyesha kama ndugu waliokuwa hawajaonana muda mrefu alichogundua ni kuwa walifikiri yupo pale kuomba msaada wakati yeye alipita kuwajulia hali. Ilibidi aage mapema kuliko muda aliopanga kukaa
 
Ugumu wa maisha , roho mbaya na umimi ndiyo chanzo! Siku hizi mtu anaifikiria nafsi yake na watoto wake, hata akiwa na uwezo kidogo wa kusaidia ndugu hafanyi hivyo....na malezi nayo yanachangia, mtoto anakua anaona kabisa wazazi hawana ushirikiano na ndugu usitegemee yeye atakuja kupenda ndugu zake. Tuwafunze watoto kuwa na upendo na kila mtu haijalishi ni ndugu, jirani au rafiki, tuwafunze kugawana kidogo walichonacho na wenzao ambao hawana ....tabia ya mtu inaanza toka utotoni.
 
Mfumo wa capitalism ndio upo hivyo

Kila mtu na chake ,kila mtu kivyake

Mtu wa hali ya chini anazidi kukamuliwa

So ni mfumo tu umesababisha hivyo

Kabla ya USA kuondoa ukomunisti na ujamaa ,kulikuwa na umoja na ushirikiano

Lakini saizi "ubepari" hakuna kuomba kaa la moto au chumvi kwa jirani
 
Back
Top Bottom