Ni kwanini hamasa ya siasa za upinzani imeshuka kiasi hiki

Bata batani

JF-Expert Member
Nov 11, 2011
3,215
3,682
Kuna utafiti nimeufanya baada ya kumalizika chaguzi ndogo za udiwani na CCM kushinda kwa kishindo, nimegundua ya kwamba kipindi hiki ile hamasa ya watu kupenda upinzani imeshuka sana.

Kipindi cha nyuma enzi za upinzani wakiamua kuitishaa maandamano basi ujue ni maandamano kweli kweli.

Kipindi cha nyuma kulikuwa ukisikia upinzani wanaenda kwenye kampeni basi ujue kwenye kampeni kwelikweli.

Kipindi cha nyuma ukisikia uchaguzi hata kama uchaguzi mdogo basi ujue upinzani walikuwa wamejipanga kweli kuchukua jimbo au kataa.

Kipindi cha nyuma ulikuwa haupiti mwezi utasikia wana harakati au wapinzani wameandaa kongamano na linarushwa kwenye t.v livee.

Lakini kipindi hiki siku zinavyozidi kwenda ile hamasa na harakati kuhusu siasa za upinzani zinazidi kudororaaa hapa ndo ninapojiuliza tatizo liko wapi

Mbona enzi zile za jk upinzani ulikuwa upinzani kweli kweli sasa hivi kuna tatizo gani
 
Unajua hii kitu sio kwa wapinzani tu, ni kwa watanzania walio wengi
TUNASHINDWA KUBISHANA KWA HOJA ILI KULETA MIJADALA CHANYA kila siku CHADEMA walizoea kutengeneza POROJO ambazo kwakiasi kikubwa walipata publicity kwakuwa walikuwa wakipuuzwa ivyo kutojibiwa na serikali iliyo kuwepo, ivyo kupelekea wananchi wengi kuamini POROJO zao.
Safari hii tumepata watu ambao hawawezi kufumbia macho Aina yoyote ya UONGO utakao enezwa, wengi hujibu MADAI ya CHADEMA kwa HOJA ivyo UPINZANI kupoteza NGUVU AUTOMATICALLY kwa kuwa hawana hoja za msingi.
 
acha uongo, anaejibu hoja za wapinzani sasa ni nani kwa mfano?
 
Ruhusuni siasa za jukwaani uone kama hamasa imeshuka au la, kinyume na hapo unajitekenya na kucheka mwenyewe.
 
Unajua hii kitu sio kwa wapinzani tu, ni kwa watanzania walio wengi
TUNASHINDWA KUBISHANA KWA HOJA ILI KULETA MIJADALA CHANYA kila siku CHADEMA walizoea kutengeneza POROJO ambazo kwakiasi kikubwa walipata publicity kwakuwa walikuwa wakipuuzwa ivyo kutojibiwa na serikali iliyo kuwepo, ivyo kupelekea wananchi wengi kuamini POROJO zao.
Safari hii tumepata watu ambao hawawezi kufumbia macho Aina yoyote ya UONGO utakao enezwa, wengi hujibu MADAI ya CHADEMA kwa HOJA ivyo UPINZANI kupoteza NGUVU AUTOMATICALLY kwa kuwa hawana hoja za msingi.
Umeingia chaka ndugu, kaa ujitathini. Hoja zipi zinazojibiwa kwa ushahidi usio na shaka? Zaidi ya kuzusha na kusaka watu kisa wasema ukweli? Kuna kauli inasema " ukweli huuma" " kweli hukuweka huru"fikiria hizo kauli halafu uniambie hizo hoja mnazozijibia zinakuwaje
 
kwa iyo cybercrime act na media bill sheria zilizotungwa kunyima ushindan wa hoja na kufanya vyombo vya habari viogope kureport taarifa sahihi kwa sababu ni mbaya kwa serikali wawe wana report za upande mmoja wa serikal na chama chake ndio wapinzan wanajibiwa kwa hoja? acha ubwege wewe!!!

pale ambapo mtu anashindwa kujibu hoja na kukimbilia nguvu tu kwa sababu ana power iyo kwa muda ule si kigezo cha kukufanya mshindi, kubambikia wapinzan kesi za ajabu ajabu na mahakama kugeuzwa kangaroo court( kwa jinsi ninavyokupima uwezo wako sijui hata kama unajua maana yake hili).

ukitaka kushindnana kwa hoja ni wana ccm hapa na sehem nyinggine pote wamekua wakikimbia au kushindwa vibaya badala yake wakaona njia pekee ni kutumia nguvu tu kwa sababu wana uwezo huo, kama hivyo ndio unavyodhan ur deluded ndugu.
 
yuko wapi mnyika na lissu mabingwa wa propaganda, hoja ipi haijajibiwa ?
 
Nafikri hauna taarifa sahihi ya kile unachokisema na wewe ni wa kupuuzwa kama walivyo wakuubb wako
 
Kama hakuna hamasa hizo nguvu mnazotumia kupambana nao zinatoka wapi?
 
Sasa unaonekana hauelewi kinachoendelea Tanzania. Kwa taarifa yako maandamano marufuku,mikutano marufuku,makongamano marufuku na mpaka sasa wanne wameshafungwa na wengine wanaozea mahabusu,sasa wewe unatafuta nani aahamasishe upinzani wakati hata bungeni uhuru wa kuongea umebanwa na bunge mubashara ni marufuku
 
1. Ni dalili za wananchi kumkubali Rais Magufuli
2. Rais Magufuli kutekeleza ahadi yake aliyotoa wakati wa uchaguzi haswa vita dhidi ya ufisadi
3. Wananchi kuona vyama vya upinzani sio za kuaminika kutokana na migogoro isiyoisha ndani vyama hivyo kwa mfano mgogoro ndani ya CUF
4. Ni kwa utendaji mzuri wa Rais Magufuli katika kurejesha heshima na nidhamu katika serikali.
5. Baada ya wananchi kugundua kuwa vyama vya upinzani si vya kuaminika kupewa madaraka.
6. Wananchi kugundua huyu mdudu ufisadi upo pia ndani ya vyama vya upinzani
7. Vyama vya upinzani kutoonyesha demokrasia ndani ya vyama vya katika kuchagua viongozi waandamizi.
 
Ccm Kama wanajiamini wafanye haya

/-wasitumie polisi kukamata wapinzani

/kutumia mahakama gulio la katerero

/-kutisha wan ajiunge na upinzani

/- wakubali tume huru ya uchaguzi
/-waache kutisha vyombo vya habari kuripoti habari ya upinzani

/-waachie bunge liwe huru upinzani kuwakilisha bajeti Yao vizuri bila kuifuta futsa
/-waachie mikutano ya adhara wananchi waonane na viongozi wao

/- waondoe sheria ya uchochezi wanaitumia vibaya kunyamazisha upinzani
/-waache kutukana viongozi wa upinzani
/-
 
Hakuna kitu kilichokuwa kinawasumbua US na nchi za Ulaya magharibi kama USSR mpaka ukakapelekea kuwapo kwa vipindi 5 vya kile kilichojulikana kama cold war lakini kipindi cha 5 Cha cold war kati ya mwaka 1985-1991 kilikuwa ni kipindi kigumu sana kwa USSR na kilikuwa kipindi kizuri sana cha US na wenzie sasa najiuliza Mikhail - Gorbachev wa upinzani pandikizi la US na wenzie ni nani????
 
Back
Top Bottom