Ni Kwa nini Israel ina Jeshi la kisasa na teknolojia Duniani

benghlasis

Member
Nov 29, 2016
49
54
[http://raiamwema]
50a047d0ae92ca0ac4f1254451dc766d.jpg

[https://aka-cdn]

Ni kwa nini Israel ina jeshi la kisasa zaidi kwa teknolojia duniani

FEB 01, 2017by MWANDISHI WETUin MAKALA

[Hébergement Internet, Cloud, et Serveurs dédiés - OVH]

Israel ni miongoni mwa nchi zinazoongoza kwa mauzo ya silaha duniani, ikiwa inauza silaha zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 6.5 kwa mwaka.

MWAKA 1950, miaka miwili tu baada ya taifa la Israel kuanzishwa, ujumbe wa kibiashara wa nchi hiyo ulifunga safari kwenda bara la Amerika Kusini.

Nchi hiyo ilikuwa inahitaji wenza kibiashara. Tofauti na adui zake wa Kiarabu, Israel haikuwa na maliasili kuendesha uchumi wake. Haikuwa na mafuta wala madini. Haikuwa na chochote.

Ujumbe huo ulikuwa na mikutano kadhaa lakini ulikutana zaidi na vicheko. Waisraeli walikuwa wanajaribu kuuza machungwa, taa zinazotumia mafuta na meno ya bandia. Kwa mataifa kama Argentina, ambayo inapanda machungwa yake na imeunganishwa katika gridi ya umeme, bidhaa hizo hazikuwa na maana yoyote.

Ni vigumu kufikiria aina ya bidhaa ambazo nchi hiyo ilikuwa inasafirisha nje miaka 67 iliyopita. Leo, Israel imeendelea kiteknolojia na ni miongoni mwa mataifa yanayoongoza kwa mauzo ya silaha nje ya mipaka yake ikiwa inakadiriwa kuuza silaha zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 6.5 kwa mwaka.

Tangu mwaka 1985, kwa mfano, Israel imekuwa inaongoza kwa mauzo ya ndege zisizotumia rubani, yaani drones ambazo zinachukua kiasi cha asilimia 60 ya soko lote duniani, ikiizidi hata Marekani, ambayo soko lake ni asilimia 25 tu. Wateja wake wapo kila mahali – Urusi, Korea Kusini, Australia, Ufaransa, Ujerumani na Brazil.

Mwaka 2010, kwa mfano, wanachama watano wa NATO walikuwa wanatumia ndege zisizoongozwa na rubani huko Afghanistan. Haya yote yamewezekana vipi? Ni kwa namna gani nchi hiyo, ambayo haina hata umri wa miaka 70, imegeuka na kuwa mbabe ikiwa na jeshi lenye teknolojia ya kisasa zaidi duniani ambalo mapinduzi ya namna vita vinavyopiganwa leo?

Jibu, ni majumuisho ya tabia kadhaa za kitaifa ambazo zipo Israel pekee.

Kwanza, pamoja na udogo wa eneo la nchi hiyo, kiasi cha asilimia 4.5 ya pato la mwaka hutumiwa katika utafiti na mipango. Katika kiasi hicho, asilimia 30 hupelekwa kwenye bidhaa zenye asili ya kijeshi. Kwa kulinganisha, ni asilimia 2 tu ya fedha kwa ajili ya utafiti na maendeleo nchini Ujerumani na asilimia 17 tu ya fedha hizo nchini Marekani hutumika kwa ajili ya utafiti wa masuala yanayohusiana na jeshi.

Pia utamaduni wa uvumbuzi na ubunifu nchini humo. Waisrael hawana kawaida ya kuogopa kushindwa ukilinganisha na watu wa mataifa mengine. Wanapata hili kutokana na mafunzo ya kijeshi ya lazima kwa kila raia. Wakiwa katika umri mdogo, kushiriki katika operesheni za hatari.

Wakati kijana wa miaka 19 akishiriki katika operesheni hatari za kijeshi, wale wa nchi za magharibi wanakuwa salama mabwenini katika vyuo wanavyosoma.

Mwisho, nchi hiyo imekuwa katika mkao wa kivita tangu ilipoanzishwa, ikipigana vita karibu kila baada ya miaka michache. Ukweli huu, wa kuzungukwa na adui, unafanya ubongo ufanye kazi zaidi. Inawalazimu kuwa wabunifu na kutafuta njia nzuri na silaha ili kuweza kuishi.

Hii ni habari ya Israel….

Ulinzi wa mpaka kwa kutumia roboti

Guardium ni aina mpya ya silaha inayofahamika kama Unmanned Ground Vehicle au UGV. Haya ni magari yasiyo na dereva. Israel ni nchi ya kwanza duniani kutumia roboti za aina hii ikiwa na nia ya kuwaondoa wanajeshi katika ulinzi wa mpaka.

Tayari, magari ya Guardium yamewekwa katika mpaka wa Israel na Syria kaskazini mwa nchi hiyo na katika Ukanda wa Gaza kwa upande wa kusini.

Gari hilo linaweza kuendeshwa na askari ambaye yupo umbali wa maili kadhaa kutoka lilipo au likapewa amri mapema, juu ya maeneo yapi litakwenda kufanya doria, na kulifanya kuwa na uwezo wa kujitegemea kabisa.

cc0af2467bf36b9c7de24755f1a01954.jpg


Gari la Jeshi la Israel, yaani IDF, ambalo halina dereva, linalofahamika kama Guardium, likifanya doria katika mpaka wa Israel na Ukanda wa Gaza.

Kuongezeka kwa matumizi ya roboti katika jeshi la Israel ni sehemu ya mpango mkubwa wa kupunguza hatari kwa askari wake pale inapowezekana. Pia, askari wanahitaji kupumzika, wanahitaji chakula na maji. Kitu ambacho magari ya Guardium yanahitaji ni mafuta ya kutosha. Magari mengine yasiyo na dereva yanayotumiwa na jeshi la Israel ni pamoja na Segev.

Ikiwa inakabiliana na magaidi ambao hutumia mahandaki kuingia nchini humo kutoka maeneo kama Ukanda wa Gaza, Israel inategemea roboti zinazofanana na nyoka kuingia ardhini na kutafuta mahandaki hayo na pia makao makuu ya adui, kabla ya askari kuvamia eneo hilo.

Baharini pia haijabaki nyuma. Meli isiyoendeshwa na nahodha inayofahamika kama Protector inatumiwa na Israel katika kulinda bandari zake na kufanya doria katika pwani ndefu ya bahari ya Mediterania.

Mpango wa ulinzi dhidi ya makombora

Mwaka 2000, Jeshi la Israel lilipokea betri yake ya kwanza ya ulinzi wa makombora unaofahamika kama Arrow, na kuifanya nchi hiyo kuwa taifa la kwanza duniani kuwa na mfumo unaofanya kazi na ambao una uwezo wa kutungua kombora lolote kutoka kwa adui.

Wazo la kuundwa kwa Arrow lilizaliwa katikati ya miaka ya 1980 baada ya Rais Ronald Reagan kutangaza mpango wake wa vita ya angani na kuwataka washirika wake kushiriki katika kuunda mfumo ambao unaweza kuilinda nchi na makombora ya kinyuklia ya Urusi.

Hilo lilikuwa ni wazo la kimapinduzi. Kutokana na udogo wa emeo lake, mabomu yote katika Mashariki ya Kati – huko Syria, Iraki na Iran – yanaweza kufika sehemu yoyote nchini Israel na kusababisha hatari kubwa. Wanasayansi wa nchi hiyo wakasema kwamba mfumo wa ulinzi wa anga unaweza kuzuia hilo kutokea kwa kulitungua katika anga ya nchi jirani na kutoa ulinzi kwa taifa dogo la Israel.

50a047d0ae92ca0ac4f1254451dc766d.jpg


Betri ya kombora la kujihami ya Arrow

Mpango huo ulikumbwa na changamoto kadhaa lakini baada ya vita ya kwanza ya Ghuba ya Uajemi ya mwaka 1991 wakati Saddam Hussein alipofyatua bou ya scud kuelekea nchini Israel na kuwalazimu mamiliani ya Waisrael katika mahandaki ulipata fedha kutoka kwa Marekani.

Huo ulikuwa ni mwanzo.

Leo Israel inamifumo kadhaa ya ulinzi wa makombora ukiwemo ule wa Sling ambao ni maalumu kwa ajili ya kutungua makombora ya masafa ya kati na pia ule wa Iron Dome, ambao ulitungua roketi na makombora mengi kutoka Ukanda wa Gaza katika miaka ya hivi karibuni.


,,,,,,,,,,,,,,Itaendelea
Source; Yaakov katz (mwandishi na mhariri mkuu wa gazeti la Jerusalem post) na Gazeti la Raia mwema

~benghlasis
 
Back
Top Bottom