Ni kodi kwa ajili ya wajinga, wabunge na wakuu wa serikali hawataki uzalendo

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
16,559
41,075
Sikuwahi kufahamu kuwa wabunge, mawaziri, Rais, Makamu wa Rais, Spika na Waziri Mkuu, mishahara na posho zao, vyote havikatwi kodi!!

Uko msemo unaosema kiongozi, "walk the talk".

Kiongozi "walk the talk" maana yake utembee juu ya maneno yako, uwe wa kwanza kutenda unayowahubiria wengine kutenda, au usitende yale ambayo unawazuia wengine kutenda.

Hao niliowataja hapo juu ndio wanaotuhamasisha sisi tulipe kodi lakini wao hawataki kulipa kodi. Wanatuambia kuwa kulipa kodi ndiyo uzalendo kwa Taifa letu, ina maana wao hawautaki uzalendo? Huu ni unafiki mkubwa wa hawa wasiotahili hata kuitwa waheshimiwa wala kuitwa viongozi wetu. Kiongozi anatakiwa awe wa kwanza kuonesha mfano katika kutenda kile anachotaka anaowaongoza, watende.

Kwa hiyo kodi imewekwa na hawa watu kwaajili ya watu wajinga? Kodi imewekwa kwaajili ya wasio viongozi? Kama kodi imewekwa kwaajili ya wajinga, tuukatae huu ujinga. Kama ujinga ni mzuri, wabaki nao wao wenyewe. Sisi tuseme kuwa hatutaki kufanywa kuwa wajinga.

Wanufaika wa kwanza wa kodi zetu ni hawa wabunge, wakuu wa mikoa na wilaya, mawaziri, spika, Waziri Mkuu, Makamu wa Rais na Rais. Hawa ndiyo watumiaji wakubwa wa kodi zetu. Kuanzia kuamka kwao mpaka kulala kwao, ni kodi zetu. Kwa nini wao walio wafaidika wa kwanza wa kodi, hawataki kulipa kodi?

Nimekereka sana kusikia hawa watu mishahara yao haikatwi kodi. Kama kodi ni uzalendo, wananchi tuwatake wao watuoneshe uzalendo wao. Au watuambie kuwa wao siyo wazalendo bali ni watafunaji wa Taifa. Kama watasema wao ni wazalendo, basi uzalendo maana yake ni kutolipa kodi, na kwa sababu na sisi tunaupenda uzalendo, tutafanya kila tuwezalo tusilipe kodi ili tuwakaribie wao kwa uzalendo.

Vinginevyo tujue kuwa tuna bunge la watu wanafiki, tuna viongozi wanafiki, wanaopenda kuhubiri wasiyotenda. Wanatutungia sisi sheria za kodi ambazo wao hawazitaki. Huu ni unafiki wa hali ya juu.

Wananchi tuamke. Tusipoamka, hawa watu wataendelea kututenda mambo mengi ya ajabu. Hakika kama hawa watu hawatakatwa kodi kwenye mapato yao yatokanayo na kodi zeru, kila mwenye akili atafute namna ya kufuata yale wanayotenda. Kama kodi ni nzuri, wao wawe mfano wa kutuonesha uzuri wake. Kama kodi ni muhimu, wao wawe wa kwanza kutuonesha umuhimu wake. Kama kodi siyo nzuri kwao, haitakuwa nzuri kwa wengine wote.

Tuache ushabiki wa aina yoyote, tujiulize, hivi hawa wanaotaka tutende ambayo wao hawataki, wanastahili kuitwa waheshimiwa au walaaniwa? Wanastahili kusimama mbele yetu kutuhubiria habari ya kodi? Kama sivyo, tuwaambie kwa maneno na vitendo kuwa ninyi ni wanafiki. Ni maadui wa Taifa. Maana hamna uadilitu mioyoni mwenu. Mmejaa ghiliba na ubinafsi.

Mwigulu unajisikia kabisa kuwa unafaa kuwa kiongozi kwa kula kodi ya mama anayeuza genge pale Misigiri au Ulemo, halafu wewe usilipe kodi yoyote kutoka kwenye mshahara na marupuruou yako?

Tuukatae unafiki wa viongozi wetu.
 
Umeongea ukweli mtupu, Bila katiba mpya hawa watu wataendelea kutunyonya mpaka kiama.
 
Wakikatwa kodi mtajua mishahara yao halafu mtakuwa na maswali.
Nani anajua mishahara ya hao hapo juu.
Nchi hii hata shetani anatukana kwa matabaka.
Mfano Mbunge anakatwa kodi kwenye 3,800,000 tu
Zingine eti posho.
Mwl kwa mwezi 450,000 anakatwa kodi.
 
Yote haya ni matokeo ya Katiba mbovu tuliyonayo.
Kwa ujumla ni matumizi mabaya ya madaraka.

Tunataka Katiba Mpya. Katiba mpya itamke kuwa kila anayepata mapato yoyote ni lazima alipe kodi. Raia wote wana wajibu sawa katika ulipaji kodi. Taasisi yoyote ambayo ilikuwa katika nafasi ya kufanya maamuzi ya kodi halafu yenyewe ikajipa uhalali wa kutolipa kodi, yalikuwa ni matumizi mabaya ya madaraka. Na hivyo kodi yote iliyokwepa kwa kutumia nafasi yako ya uongozi ni lazima ilipwe kama kodi iliyokwepwa.
 
Back
Top Bottom