mr mkiki
JF-Expert Member
- Sep 22, 2016
- 5,588
- 11,668
Ni kiwewe cha watumishi wa serikali ya Magufuli hadi kupoteza muelekeo au ni mpango wa kumuhujumu Rais ili achukiwe na umma? Mwanafunzi amedahiliwa na chuo kikuu, kwa utaratibu rasmi wa udahili, akaanza mwaka wa kwanza, akafaulu kwa mujibu wa taratibu za chuo husika; Mwaka wa pili, wa tatu, nne, tano nk. Bodi ya mitihani ya chuo kikuu imejiridhisha kuwa mtu huyu amefaulu na hivyo anatunukiwa degree yake, au diploma yake ya cheti chake. Halafu jamaa moja hivi, linaamka asubuhi libadai eti huyu mwanafunzi hakuwa na sifa? Foolish.
Hivi ni nani hana sifa katika mazingira hayo? Ni chuo kikuu husika kilichomuhitimu huyu mwanafunzi au mwanafunzi aliyefaulu mitihani na kufikia hapo alipo? Tena ukute huyo anayeitwa hana sifa anaweza kuwa na ufaulu mkubwa kuliko hao wenye sifa.
TCU mjitathmini. Tafuteni namna ya kushurukia makaburi mliochimba wenyewe huko nyuma. Msigharimu maisha ya watu! Kwa muktadha huu, mnaandaa kizazi kinachochukia taifa lao. Kizazi cha wasaliti walioandaliwa kuwa wasaliti.